Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Mfumo wa elimu unaopendekezwa na Elon Musk uitwao 'Ad Astra' likiwa neno la kilatini likimaanisha kuelekea kwenye nyota ni mfumo ambao aliuanzisha kwa siri mwaka 2014 baada ya kamua kuwatoa watoto wake kwenye Shule za kawaida akiamini kuwa shule za kawaida hazifundishi watoto namba ya kufikiri na kutatua changamoto za uhalisia. Baadae shule hii ilihamia kwenye mtandao na kujulikana kama 'Astra Nova School'. Misingi ya mfumo huu ni:
- Hakuna madaraja, vidato au umri- Watoto wa umri tofauti mathalani kuanzia miaka 7-14 kusoma pamoja. Elimu inatolewa kama kiwanda cha uzalishaji ambapo mwanafunzi anaendelea kulingana na uwezo na kasi ya kuelewa.
- Zingatio la utatuzi wa matatizo- Hapa mwanafunzi anafundishwa tatizo kwanza ndipo ajifunze njia za utatuzi kwa mfano anapatiwa injini iliyoharibika aifungue badala ya kupatiwa vifaa vya kuifungua.
- Msisitizo ,kubwa katika sayansi, teknolojia na maadili- Wanafunzi wanafundishwa masomo ya kisasa kama akili unde, sayansi ya kompyuta, roboti, uchumi na maadili.
- Mijadala mizito ya kimaadili- Mijadala inayoendana na masomo ya kisasa kama "NI NANI ANASTAHILI KUWAJIBIKA IKIWA GARI LINALOJIENDESHA LENYEWE LITAPATA AJALI".
- Kuotokomeza masomo ya sanaa na lugha za kigeni- hapa mwanafunzi anafundishwa na kutumia kuwa teknolojia ya sasa ya akili unde kutafsiru lugha mbalimbali.
- Kujifunza kupitia michezo ya kuiga 'gamification' kwa kutumia Kompyuta.