Mfumuko wa bei Zanzibar sasa imekuwa gumzo. Ni wakati sasa Rais Dkt. Mwinyi kujitafakari

Ndivyo hali ilivyo Zanzibar, watu walianza kuvimilia vumilia sasa kila mzanzibar analia na vitu vya chakula kupanda bei tena kwa speedi ya kutisha sana.

1. Mkate wa Boflo ambao ndio mkate kila mzanzibar anakula sasa ni Tshs 250/- badala ya 200/=

2. Mchele ambao ndio chakula kikuu kwa maisha ya Wazanzibari Rais Mwinyi alivyoingia madarakani ilikuwa 1kg ni Tshs 1600 wa bei ya chini wanaita mapembe mchele mbovu sana huu sasa umepanda hadi ni Tshs 2000/= per kilo

3. Mchele wa mbeya ambao ni standard kule bara hauzidi Tshs 2000/- per kilogram, Lakini ukiuliza mchelewa mbeya zanzibar utakuta bei zinaanzia 2200/- per kg ambao huu ni chenga tupu, unafuata mchele mwengine wa kawaida 2400/- per kg., unafuata mwengine hadi 2800/- per kg ni tofauti sana maisha haya na awamu iliyopita ya Dr. Ali Mohamed Shein.

4. Sukari ilikuwa Tshs 2000/- per kg sasa wanauza 2400/-

5. Mafuta ya kupikia nusu lita ilikuwa 1000/- sasa ni Tshs 2000/=

6. Sahani ya chips plain ikiuzwa 1500/- sasa wamelazimika kupandisha hadi 2000, ambapo chips mayai ikiuzwa 2500/- sasa ni Tshs 3000/=

Huu ni mfano wa bidhaa kwa vyakula fulani fulani lakini takriban hali ni hiyo hiyo kwa vyakula vilivyobakia kama maharage, kunde nk.

Lakini kama haitoshi adha ya maji imerudi ambapo sasa unaweza kukaa mwezi mieizi miwili ama wiki 3 kwa kiwango cha chini maji hayatoki kwenye mabomba watu inabidi wayafuate maji maeneo ya mbali sana tofauti na awamu ilyopita ya Dr. Mohammed Ali Mohamed Shein ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kuondoa kero ya maji visiwa vya Zanzibar.

Lakini kama haitoshi mahospitali dawa hamna inabidi ununua hadi bomba ya sindano baadae urudi kwa daktari akuchome sindano. nadhan haileti picha nzuri sana kwa Mhe, Rais wetu mpendwa hali imekuwa ni tete sana Zanzibar katika maisha ya watu

Nimeona niilete hapa hii kwenu wadau na labda Mhe. anaweza kulijua hili na kujitathmini kwa muda ambao sasa ameingia madarakani

Wazanzibar walikuwa na matumaini sana baada ya kuunganisha tofauti zilizokuwepo na kumpa mioyo yao Dr. Mwinyi lakini sasa hali imeanza kuwa tete kutokana na maisha ya watu.

Wazanziri wamekuwa wakepewa maneno laini laini lakini sidhani kama hii hali itawapeleka mbele zaidi.

Kwenu wadau katika hili.

Kaishi kongo
 
Mimi nashangaaa , unasherehekeaje Mapinduzi wakati wananchi hawana maji? hizo bilioni mlizotumia kwa sherehe kwa nini msiwatatulie wananchi kero ya Maji?

Mji mchafu lakini kila unapopita ofisi za Serekali zimewekwa matambara. ukija Malindi ambako ndio downtown kuna vumbi kama Afghanistan
Serikal ya Zanzibar sijui kodi zina tumika wapi maana ukiangalia mji umechoka Barabara mbovu zime choka Yani Una weza kuondoka Zanzibar maiaka 7 ukija kurudi hakuna mabadiriko Yan kupo vile vlle
 
machogo hamjawahi kufika Zanzibar ,mnafananisha mkate na Boflo.
hio boflo ishikie hivyohivyo teshti yake iko kivyingine kabisha unawezha kuimalizha bila ya shai. aishee
Ilinganisheni Zhanzhibar kama na sheemu ambayo haujawahi kufika kama vile peponi.
Tanganyika naifananisha na Motoni ,huo mfano tu.
Zanzibar kubaya Zanzibar makaz ya wananchi ni duni vijumba vibovu yani Zanzibar ni kama Tandale, keko, magomeni, Mwanyamala Yani ni sehem ya hovyo hakuna mipango miji
 
Serikal ya Zanzibar sijui kodi zina tumika wapi maana ukiangalia mji umechoka Barabara mbovu zime choka Yani Una weza kuondoka Zanzibar maiaka 7 ukija kurudi hakuna mabadiriko Yan kupo vile vlle
Mkuu uko sahihi, Kodi zinaliwa na wajanja wachache na wake zao
 
Call spade a Spade !! Mnawaita wajanja ?? Yaani wanaokula kodi za wananchi ni wajanja ??!! Mimi naamini Hao ni wezi tu kama wezi wengine !! Kama ni kweli wapo !
 
Waziri wa fedha alisema billion 230 za mkopo wa corona zimeenda Zanzibar lakin kiuwalisia mitaan hatuon zime tumika sehem gani
 
Call spade a Spade !! Mnawaita wajanja ?? Yaani wanaokula kodi za wananchi ni wajanja ??!! Mimi naamini Hao ni wezi tu kama wezi wengine !! Kama ni kweli wapo !
Mkuu hawa watu wanakula pesa vibaya mno kisheria na kinyume na sheria

Kisheria ni hivi
a. wanajilipa marupurupu manono pamoja na posho za kufa mtu. Mtu kaenda kisafari kidogo akirudi anakabidhiwa bahasha ina dola elfu 5 tena huyu ndo mtu wa chini.

b. Wamejiwekea sheria kwamba Serekali hainunui gari iliotumika yaani gari zao ni mpya tu Prado, Vx za kuanzia milioni 100 kwenda juu. Hizi gari gharama yake ya kuzitunza ni balaaa. halafu sasa ni full Ac everytime. unaikuta gari ya Serekali imepark switch on vioo tinted inanguruma masaa mawili huku Ac iko wazi.

c. Kuandaa sherehe na matamasha kila kukicha ambazo zinateketeza mabilioni.

Haya ni mfano tu wa mambo yanayoteketeza kodi zetu ukiachilia mbali ufisadi na ubadhirifu wa kutisha wa mali za Umma.

RIPOTI YA CAG YA MWAKA JANA IMEBAINI KATI YA BILIONI 10 ZILOTENGWA KWA MAREKEBISHO YA BARABARA , NI BILIONI MOJA TU NDO ILOTUMIKA , TISA HAZIJULIKANI ZIKO WAPI!!!!! KIDUMU CHAMA TAWALA
 
Ndivyo hali ilivyo Zanzibar, watu walianza kuvimilia vumilia sasa kila mzanzibar analia na vitu vya chakula kupanda bei tena kwa speedi ya kutisha sana.

1. Mkate wa Boflo ambao ndio mkate kila mzanzibar anakula sasa ni Tshs 250/- badala ya 200/=

2. Mchele ambao ndio chakula kikuu kwa maisha ya Wazanzibari Rais Mwinyi alivyoingia madarakani ilikuwa 1kg ni Tshs 1600 wa bei ya chini wanaita mapembe mchele mbovu sana huu sasa umepanda hadi ni Tshs 2000/= per kilo

3. Mchele wa mbeya ambao ni standard kule bara hauzidi Tshs 2000/- per kilogram, Lakini ukiuliza mchelewa mbeya zanzibar utakuta bei zinaanzia 2200/- per kg ambao huu ni chenga tupu, unafuata mchele mwengine wa kawaida 2400/- per kg., unafuata mwengine hadi 2800/- per kg ni tofauti sana maisha haya na awamu iliyopita ya Dr. Ali Mohamed Shein.

4. Sukari ilikuwa Tshs 2000/- per kg sasa wanauza 2400/-

5. Mafuta ya kupikia nusu lita ilikuwa 1000/- sasa ni Tshs 2000/=

6. Sahani ya chips plain ikiuzwa 1500/- sasa wamelazimika kupandisha hadi 2000, ambapo chips mayai ikiuzwa 2500/- sasa ni Tshs 3000/=

Huu ni mfano wa bidhaa kwa vyakula fulani fulani lakini takriban hali ni hiyo hiyo kwa vyakula vilivyobakia kama maharage, kunde nk.

Lakini kama haitoshi adha ya maji imerudi ambapo sasa unaweza kukaa mwezi mieizi miwili ama wiki 3 kwa kiwango cha chini maji hayatoki kwenye mabomba watu inabidi wayafuate maji maeneo ya mbali sana tofauti na awamu ilyopita ya Dr. Mohammed Ali Mohamed Shein ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kuondoa kero ya maji visiwa vya Zanzibar.

Lakini kama haitoshi mahospitali dawa hamna inabidi ununua hadi bomba ya sindano baadae urudi kwa daktari akuchome sindano. nadhan haileti picha nzuri sana kwa Mhe, Rais wetu mpendwa hali imekuwa ni tete sana Zanzibar katika maisha ya watu

Nimeona niilete hapa hii kwenu wadau na labda Mhe. anaweza kulijua hili na kujitathmini kwa muda ambao sasa ameingia madarakani

Wazanzibar walikuwa na matumaini sana baada ya kuunganisha tofauti zilizokuwepo na kumpa mioyo yao Dr. Mwinyi lakini sasa hali imeanza kuwa tete kutokana na maisha ya watu.

Wazanziri wamekuwa wakepewa maneno laini laini lakini sidhani kama hii hali itawapeleka mbele zaidi.

Kwenu wadau katika hili.
Hapo kwenye Chipsi huwa nalima Viazi. Mfuko wa Mbolea umepanda kutoka 65000 mpaka 110000. Gunia la Viazi kwa sasa Dsm ni 80000 kutoka 45000 mwezi August
 
Mkuu hawa watu wanakula pesa vibaya mno kisheria na kinyume na sheria

Kisheria ni hivi
a. wanajilipa marupurupu manono pamoja na posho za kufa mtu. Mtu kaenda kisafari kidogo akirudi anakabidhiwa bahasha ina dola elfu 5 tena huyu ndo mtu wa chini.

b. Wamejiwekea sheria kwamba Serekali hainunui gari iliotumika yaani gari zao ni mpya tu Prado, Vx za kuanzia milioni 100 kwenda juu. Hizi gari gharama yake ya kuzitunza ni balaaa. halafu sasa ni full Ac everytime. unaikuta gari ya Serekali imepark switch on vioo tinted inanguruma masaa mawili huku Ac iko wazi.

c. Kuandaa sherehe na matamasha kila kukicha ambazo zinateketeza mabilioni.

Haya ni mfano tu wa mambo yanayoteketeza kodi zetu ukiachilia mbali ufisadi na ubadhirifu wa kutisha wa mali za Umma.

RIPOTI YA CAG YA MWAKA JANA IMEBAINI KATI YA BILIONI 10 ZILOTENGWA KWA MAREKEBISHO YA BARABARA , NI BILIONI MOJA TU NDO ILOTUMIKA , TISA HAZIJULIKANI ZIKO WAPI!!!!! KIDUMU CHAMA TAWALA
Duh!
 
Vita dhidi ya rushwa.
Hamna kitu saivi mawaziri wake wanapiga mzigo kama kawaida, hela inatafunwa kuliko chochote rushwa na ajira za kujuana zimerud pale pale
 
Unayosema ni kweli kabisa, mfumko wa bei ni mkubwa sana, karibu kila kitu nikienda dukani vimeongezeka bei,
Rais Mwinyi alianza kumiliki na kuongoza vizuri, lkn inaonekana ulikuwa moto wa vifuu,
Mfano vijiji vya (Shamba) Matemwe na Pwani mchangani alipoingia madarakani maji ya Zawa yakawa yanatoka mara 3-4 kwa wiki, baada ya miezi 6 hali ikarudi km zamani, maji yanatoka mara 1 kwa wiki au wiki inapita bila maji kutoka.
Amefeli
 
hii shehia ya uswahilini kwetu huduma ya maji ya ZAWA inapatikana kila baada ya siku 3 au 4, na walivyo wahuni wanaweza kutufungulia maji majira ya saa 7 usiku, hapo tena utachagua usingizi au maji.

kwa sasa tumekuwa tukitegemea zaidi huduma ya maji tuliounga kwa michango ya wanakijiji kuliko maji ya serikali.
serikali za manigga hazijawahi kuwa na huduma zenye uhakika.
siku mbili kabla ya sherehe za mapinduzi walitoa huduma ya maji mchana kutwa

ngoja tusubirie huu mradi mpya wa maji walioanza kuchimbia mabomba, pengine tunaweza kupata unafuu.
Poleni sana. Suluhisho sasa ni kuchimba kisima chako. Ukisubiri maji ya zawa utaoza
 
Back
Top Bottom