Mfumuko wa bei Zanzibar sasa imekuwa gumzo. Ni wakati sasa Rais Dkt. Mwinyi kujitafakari

Unayosema ni kweli kabisa, mfumko wa bei ni mkubwa sana, karibu kila kitu nikienda dukani vimeongezeka bei,
Rais Mwinyi alianza kumiliki na kuongoza vizuri, lkn inaonekana ulikuwa moto wa vifuu,
Mfano vijiji vya (Shamba) Matemwe na Pwani mchangani alipoingia madarakani maji ya Zawa yakawa yanatoka mara 3-4 kwa wiki, baada ya miezi 6 hali ikarudi km zamani, maji yanatoka mara 1 kwa wiki au wiki inapita bila maji kutoka.
Mie kila siku hushangaa ni vipi tunafeli kwenye suala la maji miaka yote hii. Yaani tupo kisiwani halafu tu nakosa maji kweli. Kitu muhimu kama maji, kweli!!!?
 
Ndivyo hali ilivyo Zanzibar, watu walianza kuvimilia vumilia sasa kila mzanzibar analia na vitu vya chakula kupanda bei tena kwa speedi ya kutisha sana.

1. Mkate wa Boflo ambao ndio mkate kila mzanzibar anakula sasa ni Tshs 250/- badala ya 200/=

2. Mchele ambao ndio chakula kikuu kwa maisha ya Wazanzibari Rais Mwinyi alivyoingia madarakani ilikuwa 1kg ni Tshs 1600 wa bei ya chini wanaita mapembe mchele mbovu sana huu sasa umepanda hadi ni Tshs 2000/= per kilo

3. Mchele wa mbeya ambao ni standard kule bara hauzidi Tshs 2000/- per kilogram, Lakini ukiuliza mchelewa mbeya zanzibar utakuta bei zinaanzia 2200/- per kg ambao huu ni chenga tupu, unafuata mchele mwengine wa kawaida 2400/- per kg., unafuata mwengine hadi 2800/- per kg ni tofauti sana maisha haya na awamu iliyopita ya Dr. Ali Mohamed Shein.

4. Sukari ilikuwa Tshs 2000/- per kg sasa wanauza 2400/-

5. Mafuta ya kupikia nusu lita ilikuwa 1000/- sasa ni Tshs 2000/=

6. Sahani ya chips plain ikiuzwa 1500/- sasa wamelazimika kupandisha hadi 2000, ambapo chips mayai ikiuzwa 2500/- sasa ni Tshs 3000/=

Huu ni mfano wa bidhaa kwa vyakula fulani fulani lakini takriban hali ni hiyo hiyo kwa vyakula vilivyobakia kama maharage, kunde nk.

Lakini kama haitoshi adha ya maji imerudi ambapo sasa unaweza kukaa mwezi mieizi miwili ama wiki 3 kwa kiwango cha chini maji hayatoki kwenye mabomba watu inabidi wayafuate maji maeneo ya mbali sana tofauti na awamu ilyopita ya Dr. Mohammed Ali Mohamed Shein ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kuondoa kero ya maji visiwa vya Zanzibar.

Lakini kama haitoshi mahospitali dawa hamna inabidi ununua hadi bomba ya sindano baadae urudi kwa daktari akuchome sindano. nadhan haileti picha nzuri sana kwa Mhe, Rais wetu mpendwa hali imekuwa ni tete sana Zanzibar katika maisha ya watu

Nimeona niilete hapa hii kwenu wadau na labda Mhe. anaweza kulijua hili na kujitathmini kwa muda ambao sasa ameingia madarakani

Wazanzibar walikuwa na matumaini sana baada ya kuunganisha tofauti zilizokuwepo na kumpa mioyo yao Dr. Mwinyi lakini sasa hali imeanza kuwa tete kutokana na maisha ya watu.

Wazanziri wamekuwa wakepewa maneno laini laini lakini sidhani kama hii hali itawapeleka mbele zaidi.

Kwenu wadau katika hili.
Tatizo ni wavivu, hakuna uzalishaji , wanawategemea wabara ndio wafanye kazi zao
 
Hao wabara wamejazana Zanzibar wamekuja kutafuta maisha kwao huko bara imeshibdikana, wanyamwez kibao na familia zao wanamiminika
 
Siku nikienda Zenji nitakaonja na urojo
Yaani mpk ule na urojo au supu au harage ndio uongeze nguvu. Wenyewe na chai tu baada ya lisaa una njaa tena.

Sasa piga Mahesabu family ya watu saba labda mpk Kumi utanunua mingapi!!?
20211106_204740.jpg
 
Ndivyo hali ilivyo Zanzibar, watu walianza kuvimilia vumilia sasa kila mzanzibar analia na vitu vya chakula kupanda bei tena kwa speedi ya kutisha sana.

1. Mkate wa Boflo ambao ndio mkate kila mzanzibar anakula sasa ni Tshs 250/- badala ya 200/=

2. Mchele ambao ndio chakula kikuu kwa maisha ya Wazanzibari Rais Mwinyi alivyoingia madarakani ilikuwa 1kg ni Tshs 1600 wa bei ya chini wanaita mapembe mchele mbovu sana huu sasa umepanda hadi ni Tshs 2000/= per kilo

3. Mchele wa mbeya ambao ni standard kule bara hauzidi Tshs 2000/- per kilogram, Lakini ukiuliza mchelewa mbeya zanzibar utakuta bei zinaanzia 2200/- per kg ambao huu ni chenga tupu, unafuata mchele mwengine wa kawaida 2400/- per kg., unafuata mwengine hadi 2800/- per kg ni tofauti sana maisha haya na awamu iliyopita ya Dr. Ali Mohamed Shein.

4. Sukari ilikuwa Tshs 2000/- per kg sasa wanauza 2400/-

5. Mafuta ya kupikia nusu lita ilikuwa 1000/- sasa ni Tshs 2000/=

6. Sahani ya chips plain ikiuzwa 1500/- sasa wamelazimika kupandisha hadi 2000, ambapo chips mayai ikiuzwa 2500/- sasa ni Tshs 3000/=

Huu ni mfano wa bidhaa kwa vyakula fulani fulani lakini takriban hali ni hiyo hiyo kwa vyakula vilivyobakia kama maharage, kunde nk.

Lakini kama haitoshi adha ya maji imerudi ambapo sasa unaweza kukaa mwezi mieizi miwili ama wiki 3 kwa kiwango cha chini maji hayatoki kwenye mabomba watu inabidi wayafuate maji maeneo ya mbali sana tofauti na awamu ilyopita ya Dr. Mohammed Ali Mohamed Shein ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kuondoa kero ya maji visiwa vya Zanzibar.

Lakini kama haitoshi mahospitali dawa hamna inabidi ununua hadi bomba ya sindano baadae urudi kwa daktari akuchome sindano. nadhan haileti picha nzuri sana kwa Mhe, Rais wetu mpendwa hali imekuwa ni tete sana Zanzibar katika maisha ya watu

Nimeona niilete hapa hii kwenu wadau na labda Mhe. anaweza kulijua hili na kujitathmini kwa muda ambao sasa ameingia madarakani

Wazanzibar walikuwa na matumaini sana baada ya kuunganisha tofauti zilizokuwepo na kumpa mioyo yao Dr. Mwinyi lakini sasa hali imeanza kuwa tete kutokana na maisha ya watu.

Wazanziri wamekuwa wakepewa maneno laini laini lakini sidhani kama hii hali itawapeleka mbele zaidi.

Kwenu wadau katika hili.
Huku Bars pia Hali ni tete,ila kumejaa wanafiki wanajifanya mabo safi kama hawaoni vile
 
mwandish wa habar hii ni mgen sana kwa maisha ya zanzibar kwa miaka yote chakula zanzibar ni ghali sana aswa kwa mchele viaz unga uwez kuona ulojo ukiwa bei juu vyaula vyote ambavyo vinaletwa kutoka morogoro mbeya shinyanga unategemea bei iwe chini wakat dar mchele nzur ni 2000 nk

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
Inawezekana wewe hujui chochote kuhusu maisha ya z'bar alichomisema muandishi kipo sawa sawa bidhaa kwa kipindi hichi zimepanda sana mfano saruji waziri wa biashara baada kuweka mambo sawa yeye ndio kaipandisha kabisa kwa kuagiza iuzwe kwa 18 elfu baada ya 15 elfu kwa mfuko mmoja
 
Hamna kitu saivi mawaziri wake wanapiga mzigo kama kawaida, hela inatafunwa kuliko chochote rushwa na ajira za kujuana zimerud pale pale
Ok. Weka watu watano tu unaowajua waneajiriwa bila vigezo. Kuhusu Mawaziri kupiga mzigo una maanisha?...🙏🙏🙏
 
wanapiga hela ndugu vibaya sana hakuna maendeleo
 
Inawezekana wewe hujui chochote kuhusu maisha ya z'bar alichomisema muandishi kipo sawa sawa bidhaa kwa kipindi hichi zimepanda sana mfano saruji waziri wa biashara baada kuweka mambo sawa yeye ndio kaipandisha kabisa kwa kuagiza iuzwe kwa 18 elfu baada ya 15 elfu kwa mfuko mmoja
Mbatata saivi kg 1800
 
Mbona hali hiyo ya kupaa kwa bei za bidhaa muhimu imeanzia huku bara.--- kimsingi ni nchi nzima.

1----Visiwani---Rais Hussein Mwinyi, mzanzibari.
2----Jamhuri ya Muungano----Rais Samia Suluhu, mzanzibari. Wazanzibar mnashida gani katika eneo hili??!!🤣
Hussein Mwinyi ni kijana wa Mkuranga Si mzanzibari ,ameletwa kuendeleza uvamizi Na kuuza visiwa
 
Back
Top Bottom