Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Ukiona mawaziri husika hawatumbuliwi basi ujue kuwa hakuna hujuma zozote.

Isipokuwa Kuna matatizo ambayo mawaziri wa wizara na Mh. RAIS wanayajua na hivyo hakuna mtu anayeweza kutatua tatizo lililo nje ya human resources( Mfano: ukame).
 
Nchi toka 1961 bado viongozi w serikali wanatoa tamko MVUA hamna.... wamekaa nao wanasubiri mvua.. swali la ziada ni mbona haya makali kuna kipindi hayakuwapo?? Licha ya hali ya mvua kuwa 'duni'?
 
Wanaihujimu vipi? Wao ndio wameleta Ukame?
 
Nashangaa mtu anaesema anahujumiwa wakati taasisi zote zipo chini ya rais.

How insane.
 
Tuchepushe maji ya ziwa victoria yaende kwenye mabwawa ya umeme watu wapate umeme muda wote na mto Ruvu watu wapate maji muda wote!
 
Huu ukame na kupungua kwa kina cha maji ungekua umeanza mwaka huu wangeleweka kidogo japo bado wangelaumiwa kwa kuwa na mipango isiyoangalia dharura
Suala hili ni la kidunia,, kikubwa ni kuwa na chanzo mbadala cha nishati, mfano gesi ambayo tunayo ya kutosha, trilions zilizoenda nyerere hydroelectric power project, zingeenda kwenye mradi wa gesi , tatizo la nishati lingepungua sana
 
Huu ukame na kupungua kwa kina cha maji ungekua umeanza mwaka huu wangeleweka kidogo japo bado wangelaumiwa kwa kuwa na mipango isiyoangalia dharura
Mipango ipo na ndio maana Rais Samia anajenga mabwawa na kidunda nk..

Mwendazake ndio wa kulaumiwa hakuna kitu alifanya kwenye sekta ya Maji.
 
Mipango ipo na ndio maana Rais Samia anajenga mabwawa na kidunda nk..

Mwendazake ndio wa kulaumiwa hakuna kitu alifanya kwenye sekta ya Maji.
Mwendazake ndio kakausha maji mto ruvu?

Semeni ukweli kuongoza nchi kama Tanzania kila anayepewa cheo anataka kuwa mpigaji bila kiongozi wa juu kuwa madhubuti msahau maendeleo.

Watanzania tumezoea kusukumwa ndio mambo yaende bila hivyo business as usual.
 
Nakumbuka ya huko ughaibuni...mama mtu kashika usukani kwa siku 45! Akajipima akaona hatoshi na hivyo akachukua hatua ya kiungwana, akajiwajibisha na kuachia huo usukani.

Hapa kwetu ni kung'ang'ania tu, hajiuzulu mtu hapa. Kuna nyakati hata inabidi Mungu kuingilia kati. Lakini hapa akina mama D ndio huingilia kati...utawasikia mara oh, anahujumiwa! Ebo!
 
Sisi tunaotengeneza ice cream na kuzigandisha mambo hayaendi [emoji1]

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…