Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Leo ukiwauliza wapenzi wa Lissu wakupe hoja ambazo zitamfanya Lissu kumshinda JPM sidhani kama atakupa mwenyewe Lissu mpk leo hakuna solution aliyosema kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi zaidi ya kupiga kelele na kutoa lawama tu.
Hajo zipo jukwaani kampeni ikianza unataka hoja mda huu mje kusema Lisu kaanza kampeni kabla ya mda? Subiria hoja kwenye kampeni utasikia mengi yaliyofichwa pindi mtukufu kazuia mikutano ya siasa kinyume cha Sheria na katiba kwa mda wa miaka mitano.
 
Kichwani una mawenge ya lissu, kwanini kuniwekea maneno kinywani mwangu?
Mkuu kwani aliyesema tatizo la ajira nila dunia nzima ni nani? Au umeshasahau ulichoandika?
 
Kura zimeibiwa excuse inakuja soon....
Wahitimu vyuo vikuu na sekta zinginezo hawana ajira, na wachache wanaajiliwa kwa upendeleo na hira.

Wafanyakazi hawakupandishwa mishahara wala kupewa nyongeza ya mwaka iliyopo kisheria kwa miaka5.Wametukanwa na kudhalilishwa hadharani.

Wakulima wamepolwa mazao yao, bei ya mazao imeshuka na wakulima kutishiwa kupigwa wao na Shangazi zao.

Wafanya biashara wamepokwa Mali zao, biashara zinasua sua na wafanya biashara wengine wameswekwa rumande mpka sasa na hakuna hukumu iliyotolewa kama kweli ni waharifu miaka5 mtu yupo mahabusu hakuna ushahidi lakini amefungwa kibabe.

Raia wameuwa, kupotezwa na kuteswa kikatili.

Ni mtanzania wa aina gani ambaye hana Akili atachagua Utopolo huu wa CCM.

Safari hii tunamchagua Mtanzania mwenzetu anaye jali utu wetu, tamaduni zetu, haki zetu na Uhuru wetu.

Hatuwezi kumchagua mtu anaye jali madaraja au reli kuliko utu wetu na Uhuru wetu.

Makaburu wa Afrika kusini walijenga barabara, madaraja ya juu, reli tena bora kuliko hivi anavyo jenga Magufuli.Lakini Tanzania tulikuwa mstari wa mbele kuwasaidia Afrika Kusini kupigania haki yao ya Uhuru.

Tuliamini kuwa Uhuru wa mtu unazidi thamani ya vitu. Hata wakoloni hapa Tanganyika walijenga reli, shule, barabara na mengine mengi mazuri. Lakini tuliwaondoa kwa kuwa hawakutupa uhuru wetu. Hatuwezi kurudishwa utumwani tena mara ya pili.

Maendeleo hayana vyamaa.
 
Kawadanganye mazuzu wenzako huko lumumba
Tusidanyane na wala msijifariji!.Kiuhalisia ni ngumu sana kukataa jitihada za rais Magufuli ni mtu aliyeifanyia mambo makubwa sana Tanzania na anahitaji muda zaidi ili taifa letu liendelee kupiga hatua kubwa zaidi.
Ukiangalia kiuwalisia Lissu pia ni mtu mwenye uweledi kutokana na elimu yake ya sheria lakini ni mapema mno kwasasa kwa yeye kuingia madarakani ingempendeza zaidi angegombea 2025.Ila kwa Sasa ni anatafuta sympathy tu, kura atakazo pata ni chache sana huo ndo ukwel mchungu. Yaan mtu kakaa Belgium huko miak 3 alafu simply eti anagombea Urais kisa alipigwa risasi kwamba ataonekan shujaa na kupata kura za huruma!. Never ! Urais sio kama kuokota dodo chini ya muembe.
 
Ni ajabu sana kwamba unaweza kumtaja Mwenyenzi Mungu na kuwaita MABEBERU (kwa herufi kubwa) watu ambao wameumbwa kwa sura na mfano wa huyo Mwenyenzi Mungu!!

Watu hao unaowaita MABEBERU wanachangia asilimia kubwa ya budget yetu ya kuendesha serikali na miradi ya maendeleo, na siku hizi wakitua KIA, mawaziri wanatupa takwimu!!😂 lakini kuweza kumtaja Mungu na kuita wanadamu wenzako MABEBERU, Wewe ni genious!!😂

Mbaya zaidi maneno haya ya kibaguzi yanatamkwa na Rais wa nchi yetu mara kwa mara na amekuwa akiyarudia.
Waafrika tukienda Ulaya wakituita Nyani tunachukizwa na huu ubaguzi. Huku kwetu bado tunaendeleza huu ubaguzi. (Tafsiri ya neno Beberu ni Mbuzi Dume, iweje leo tunawaita hivyo Binadamu wenzetu) Tuna kiongozi wa hovyo kwakweli.
 
Walizoeshwa vya kunyonga, sasa wanaambiwa wachinje wanaanza ngonjera
Tafuta kazi ya kufanya mkuu , ccm mwisho wake oct 28 , ni masikitiko sana ! hasa kwa nyie mliokuwa mnalopiwa hadi kodi za nyumba .
 
Kwani Tanzania kuna corona?
Ajira hakuna, korona ndio imeongeza tatizo kabisa hilohalina ubishi zaidi ya hapo ni propaganda za kuomba kura , hilo halina ubishi, #hamna jipya chini ya jua .
 
Mkuu kwani aliyesema tatizo la ajira nila dunia nzima ni nani? Au umeshasahau ulichoandika?
Ajira ni tatizo la kidunia , vinginevyo wazee wa kupiga dili wawadanganye kwa kuiuza nchi kwa mabeberu , Tid anawatafuta.
 
Sawa mkuu. Mimi binafsi nawapenda sana cdm lakini mujitahidi sana kuwa wazalendo kwa mama Tanzania. Kuisema vibaya Tanzania nje ya mipaka sio jambo poa. Lakini jitahidini kuheshimu mamlaka za kiserikali.utovu wa adabu kwa mhe rais, hii kitu sio nzuri.

Cdm hawahitaji upendo wako. Hakuna mwanacdm anaisema vibaya nchi bali mwenendo mbaya wa serikali, na hili litafanyika popote pale duniani. Jifunze tofauti ya serikali na nchi. Serikali inaheshimiwa, lakini haimaanishi serikali na Mungu hivyo haiwezi kukosolewa, kupingwa nk. Inaonekana kwako rais ni Mungu ndio maana unajipa haki ya kuzuia yeye kukosolewa. Hii ni kwasababu una maslahi binafsi na madaraka yake. Kazi ya cdm ni kukosoa serikali kwakuwa wao ni wapinzani, hiyo kazi ya kusifia na kusujudia wasisitizeni NCCR, CUF, TLP nk ndio wawafanyie.
 
Kiukweli nyomi lilikuwa kubwa hadi watu wakakosa pa kukanyaga na picha na video zimepigwa ila haziwezi kuwekwa hapa maana zote zimeliwa na virus.
 
Wahitimu vyuo vikuu na sekta zinginezo hawana ajira, na wachache wanaajiliwa kwa upendeleo na hira.

Wafanyakazi hawakupandishwa mishahara wala kupewa nyongeza ya mwaka iliyopo kisheria kwa miaka5.Wametukanwa na kudhalilishwa hadharani.

Wakulima wamepolwa mazao yao, bei ya mazao imeshuka na wakulima kutishiwa kupigwa wao na Shangazi zao.

Wafanya biashara wamepokwa Mali zao, biashara zinasua sua na wafanya biashara wengine wameswekwa rumande mpka sasa na hakuna hukumu iliyotolewa kama kweli ni waharifu miaka5 mtu yupo mahabusu hakuna ushahidi lakini amefungwa kibabe.

Raia wameuwa, kupotezwa na kuteswa kikatili.

Ni mtanzania wa aina gani ambaye hana Akili atachagua Utopolo huu wa CCM.

Safari hii tunamchagua Mtanzania mwenzetu anaye jali utu wetu, tamaduni zetu, haki zetu na Uhuru wetu.

Hatuwezi kumchagua mtu anaye jali madaraja au reli kuliko utu wetu na Uhuru wetu.

Makaburu wa Afrika kusini walijenga barabara, madaraja ya juu, reli tena bora kuliko hivi anavyo jenga Magufuli.Lakini Tanzania tulikuwa mstari wa mbele kuwasaidia Afrika Kusini kupigania haki yao ya Uhuru.

Tuliamini kuwa Uhuru wa mtu unazidi thamani ya vitu. Hata wakoloni hapa Tanganyika walijenga reli, shule, barabara na mengine mengi mazuri. Lakini tuliwaondoa kwa kuwa hawakutupa uhuru wetu. Hatuwezi kurudishwa utumwani tena mara ya pili.

Maendeleo hayana vyamaa.
Ndoto za mchana bana!! Lol
 
Back
Top Bottom