FACTSFIRST
Senior Member
- Dec 6, 2019
- 191
- 290
Hapo vip!!
Leo nimeangalia msafara wa Lissu wakati anaenda kuchukua form na wakati anarudi, kwa kweli msafara wake ulikuwa kama msafara wa kugombea uenyekiti wa mtaa...
Watanzania waichoke Chadema kwani lini iliwahi kushika madaraka na;
1. Kadhoofisha uchumi wa nchi kiasi cha kusababisha maumivu kwa wananchi wengi wa kawaida.
2. Kutoongeza mishahara ya wafanyakazi kwa maiaka 5 mfululizo wakati gharama za maisha zikipanda kila mwaka kiasi cha kuwafanya wawe masikini zaidi.
3. Kwa kuongeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kutokana na kuelekeza fedha nyingi za nchi kwenye miradi michache mikubwa isiyozalisha ajira kwa wananchi walio wengi.
4. Kwa kuichonganisha nchi yetu na mataifa marafiki kiasi cha kunyimwa misaada ya maendeleo iliyokuwa inasaidia kujazia akisi bajeti yetu, hasa kipindi hiki ambacho mapato ya serikali yameshuka kutokana na biashara nyingi kufungwa na wafanyabiashara wakubwa baadhi kuondoka nchini?
Wananchi waichoke Chadema kwa kuwadabahishia lipi? Hebu subiri TL aanze kuzunguka mikoani ndipo uje na huu uzi wako.
Kuipima Chadema kwa tukio la Dodoma...tena Dodoma... ile ya watu wachache na wengi wao pale mjini wakiwa ni wafanyakazi wa serikali?
Subiri uone akija Arusha, halafu Dar, Mwanza, Mbeya, Tanga, Kagera, Morogoro,...
Subiri utaongea tena.