Uchaguzi 2020 Mgombea Mwenza wa Lissu ni mzaha wa CHADEMA kwa Watanzania!

Lissu pamoja na Mwalimu ni mzaha kwenye urais. Afadhali ya Mzee Hashim Rungwe!
 
Chadema hawajawahi kuwa serious na Mambo ya watanzania
Wamemteua mwalimu Kama Bora liende tu kwa kuwa wanajua hawatopita
Mwalimu anatuhuma za kuuza viti maalum kwa milioni 20 na bao mbili mbili,hizi tuhuma ziliwasilishwa kamati kuu na Peter Msigwa na Sugu
 
Mwalimu ana degree,
Masters bado hajamaliza Research.
 
Ha ha haa... aisee hii kitu sijawahi kuwaza kabisa. Kwa kweli hiki ni kituko.
 
Mwalimu alisoma IFM na alikuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi pale acheni kupotosha na kuwasemea uongo watu.Hivi naibu rais aliyepita bwana Daud Albert Bashite Malyangiri a k a DAB ,mwenye mkoa wake ana elimu gani?
 
Vijana wengi humu JF mnaleta mada kama za udaku vile, mnashindwa kuchambua kwa nini unataka kutuonyesha kwanini mgombea mwanza wa cdm hafai!
 
Hawana watu upande wa Zanzibar inabidi wamchukue huyo garasa. Haina jinsi
 

Hata mimi niliwaza sana jana kuona mwaliu akisaini fomu pale tume, nikawaza hivi hawa wako serious na nchi kweli, yaani uwakabidhi nchi watu ambao akiri zao wote hazieleweki?
Ni bora wangetafuta mtu mzima mwenye busara hata awe anamfunga gavana raisi wao.
Chadema hawako tayari kwenye uraisi ila wamejipanga kuvuruga uchaguzi pamoja na nchi.
 
Mkuu ondokana na haya mawazo mgando.

Ukiangalia viongozi waliotuongoza kutoka uhuru hadi sasa walio wengi ni wa uwezo wa kawaida tu.

Nakuhakikishia hata wewe tukikupea unaweza vizuri tu.

Raisi amezungukwa na wasaidizi na washauri tele hao ndo wanapambana kumletea kila vitu mezani, yeye anabaki kuwa mwamuzi wa kipi kifanyike kipi kiachwe na hakuna wa kumhoji kwanini kafanya hiki na sio kile.

Ukiangalia nchi nyingi hata hapa afrika nyingi zinaachana na vibabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…