Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.
Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?...
Kuna tofauti kubwa kuongea lugha flani na kuwa mkabila au mbaguzi! Makaburu waliongea kwa kiingereza lakini walikuwa wabaguzi, unaweza kuongea kiswahili na ukawa mkabila au ukaongea kikwere na ukawa mzalendo vilevile! Nadhani tunapashwa kutofautisha mambo haya,it is the
Content that matters vinginevyo weka alichoongea. Angalia mifano hii.
1. Katika awamu hii nikichaguliwa nitahakikisha barabara zote zinatengenezwa na kupitika wakati wote (Weka kilugha chako).
2. Safari hii Kiongozi lazima atoke kwetu (Acha kiswahili), ipi ina ukabila au ubaguzi kati ya tungo hizo mbili?! Kwani mwalimu Nyerere alikuwa haongei kikwao au ndiyo nyie dot.com ulimsikia tu (Kung'atuka, manza ganyamu....). Mhe.Dr.John Pombe Magufuli ni multi lingual anaweza kuongea takribani lugha zote za Tanzania ,nadhani wewe ni mkabila ndiyo maana unona tatizto akiongea kisukuma tu, akiongea kijaruo, kihaya, kibondei, kiha, kimakonde siyo tatizo.
Unashauri je tufute lugha zetu za asili tubakishe kiswahili na kiingereza?! Ukweli ni kwamba kuna vitu ni ngumu sana kutafsiri na kupata maana halisi ndiyo maana una maneno kama "equilibrium", momentum, soni, hamsa, Allah, Jehova nk. Acha ukoloni mambo leo!