Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?...
Kuna tofauti kubwa kuongea lugha flani na kuwa mkabila au mbaguzi! Makaburu waliongea kwa kiingereza lakini walikuwa wabaguzi, unaweza kuongea kiswahili na ukawa mkabila au ukaongea kikwere na ukawa mzalendo vilevile! Nadhani tunapashwa kutofautisha mambo haya,it is the Content that matters vinginevyo weka alichoongea. Angalia mifano hii.

1. Katika awamu hii nikichaguliwa nitahakikisha barabara zote zinatengenezwa na kupitika wakati wote (Weka kilugha chako).

2. Safari hii Kiongozi lazima atoke kwetu (Acha kiswahili), ipi ina ukabila au ubaguzi kati ya tungo hizo mbili?! Kwani mwalimu Nyerere alikuwa haongei kikwao au ndiyo nyie dot.com ulimsikia tu (Kung'atuka, manza ganyamu....). Mhe.Dr.John Pombe Magufuli ni multi lingual anaweza kuongea takribani lugha zote za Tanzania ,nadhani wewe ni mkabila ndiyo maana unona tatizto akiongea kisukuma tu, akiongea kijaruo, kihaya, kibondei, kiha, kimakonde siyo tatizo.

Unashauri je tufute lugha zetu za asili tubakishe kiswahili na kiingereza?! Ukweli ni kwamba kuna vitu ni ngumu sana kutafsiri na kupata maana halisi ndiyo maana una maneno kama "equilibrium", momentum, soni, hamsa, Allah, Jehova nk. Acha ukoloni mambo leo!
 
Daaaah we mtoa mada pengine una matatizo binafsi nahuyo mgombea wa ccm.au wewe ni mchaga????
 
Mgombea wa CCM John Magufuli kwa nini hataki kutekeleza agizo la NEC kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili ndio pekee kipindi chote cha kampeni?

Magufuli akiwa Kanda ya Ziwa amekuwa anatumia lugha ya Kisukuma bila woga wala kificho na sio tume wala yeyote ambaye amekemea uvunjifu huo wa kanuni?
 
Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.
Anajifananisha na nani? Shenzi kabisa. Nimechukizwa sana na mfanano huo wa kipuuzi. Halafu watz tunapenda sana kujifananisha fananisha na watu wengine sijui kwa nini. Na wakati mwingine tunajitukuza tu wakati hata hizo sifa hatuna. Kudadadeki.
 
Yeye anafikiri mwanza wanaishi wasukuma peke yao? Wengi hapo kwenye mkutano hawamwelewi, Tanzania ina makabila zaidi ya 120 na wanaishi mikoa mbalimbali bila kujali kabila gani.
Hivi ni kwa nini tunaanza kuujadili usukuma hapa ? Hivi tunakula chakula au usukuma ? Hivi tunaoga maji au usukuma ? Saa nyingine kuna upuuzi sana unaendelea na ni vigumu sana kuufumbia macho. Shame to you tribalists of Tanzania
 
Lazima ufahamu na kujua kwamba kisukuma ni lugha ya tatu kuongewa na watu wengi hapa Tanzania, baada ya Kiswahili, kiingereza na kikifuatia kisukuma. Upo hapo ?
 
huwa na enjoy sana nikisikia mgombea anasalimia kilugha cha pale kwao!! binafs niseme kweli huwa sisikii raha nikiona mtu anaomgea kiswahili tupuu kisa? na ndio mana mnagombea majimbon. mwaga salam ya kinyumban pia. kuna misemo ukiwa eneo husika ukiisema kwa kilugha cha pale inaeleeweka sawasawa mzee . Nashauri mtu akisimama eneo apige kilugha hata ikiwezekana nusu saa nzima.kama ulikulia mjini shauri yako
 
Anaongea na wasukuma wenzake wewe unachowashwa ni nn?
Oya TBC Kila wakati inatoa miongozo ya NEC kuhusu Sheria za kampeni kuwa kampeni zote zitatumika Kwa lugha ya Kiswahili na marufuku Kwa mgombea yoyote kupiga kampeni kwa lugha isiyokuwa Kiswahili na kama wananchi wa eneo husika hawafamu vizuri Kiswahili basi mgombea ataongea Kiswahili na mkalimani atatafsiri. Baada ya kujibu hoja unaleta mipasho.
 
CHADEMA kinajihusisha na ubaguzi wa kikabila na kikanda.
Mgombea wa ccm alipokuwa Magu amehutubia kwa kisukuma mwanzo mwisho. Ninakushauri kaeni naye na mumwambie asiiharibu nchi yetu kwa kupanda mbegu ya ukabila.
 
Back
Top Bottom