Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Uzoefu unaaonyesha kuwa usiri wa mikataba ni moja ya chanzo cha nchi yetu kuingiza katika mikataba ya kifisadi ambayo mwisho wa siku hainufaishi wananchi, bali hunufaishi watu binafsi wakiwemo wanaoitwa mabeberu.
Kwa mfano,nikikumbuka mapambio ya uchumi wa gesi enzi za JK na kinachoendelea leo hii,sioni kama kuna jambo kubwa linalolingana na kelele za wakati ule kuhusu hiyo gesi,ila kama kuna anaeweza kutueleza mafanikio ya kiuchumi yanayotokana na hiyo gesi,basi atueleze na wengine tutafurahi kusikia kutoka kwake.
Sasa wakati uchumi wa gesi wengine hatuoni mpaka sasa,leo hii tumeletewa miradi mingine mikubwa tu ambayo nayo dalili zinaonyesha imegubikwa na usiri wa mikataba.
Sasa tujiulize,kwakuwa mikataba hii ni ya siri kwa maana ya kutoplelekwa Bungeni kama sheria inavyotaka,kwanini tusiwe na hofu kuwa miradi hii nayo huenda ni ya kifisadi?
Je, si kweli wapinzani ndio walisimama kidete Bungeni(mwaka 20125 kama sikosei) wakati wa Bunge la Mama Mkinda wakitaka uwazi wa mikataba ya gesi?
Je, leo hii tunapomsikia mwanasiasa wa upinzani kama Lissu na ambae pia ni mgombea uraisi kupitia CHADEMA anahoji usiri wa mikataba ya awamu hii,kwanini tusIkumbuke yaliyopita na tukawa na hofu na mashaka?
Tukumbuke sheria hii ni ya mwaka 2017 na wameitunga wao wenyewe tena kwa mbwembwe kweli.
Once bitten,twice shy.
Muda utasema.
Shule imeisha sasa niko huru kwa mijadala.