Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu afanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha ITV dakika 45

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu afanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha ITV dakika 45

Uzoefu unaaonyesha kuwa usiri wa mikataba ni moja ya chanzo cha nchi yetu kuingiza katika mikataba ya kifisadi ambayo mwisho wa siku hainufaishi wananchi, bali hunufaishi watu binafsi wakiwemo wanaoitwa mabeberu.

Kwa mfano,nikikumbuka mapambio ya uchumi wa gesi enzi za JK na kinachoendelea leo hii,sioni kama kuna jambo kubwa linalolingana na kelele za wakati ule kuhusu hiyo gesi,ila kama kuna anaeweza kutueleza mafanikio ya kiuchumi yanayotokana na hiyo gesi,basi atueleze na wengine tutafurahi kusikia kutoka kwake.

Sasa wakati uchumi wa gesi wengine hatuoni mpaka sasa,leo hii tumeletewa miradi mingine mikubwa tu ambayo nayo dalili zinaonyesha imegubikwa na usiri wa mikataba.

Sasa tujiulize,kwakuwa mikataba hii ni ya siri kwa maana ya kutoplelekwa Bungeni kama sheria inavyotaka,kwanini tusiwe na hofu kuwa miradi hii nayo huenda ni ya kifisadi?

Je, si kweli wapinzani ndio walisimama kidete Bungeni(mwaka 20125 kama sikosei) wakati wa Bunge la Mama Mkinda wakitaka uwazi wa mikataba ya gesi?

Je, leo hii tunapomsikia mwanasiasa wa upinzani kama Lissu na ambae pia ni mgombea uraisi kupitia CHADEMA anahoji usiri wa mikataba ya awamu hii,kwanini tusIkumbuke yaliyopita na tukawa na hofu na mashaka?

Tukumbuke sheria hii ni ya mwaka 2017 na wameitunga wao wenyewe tena kwa mbwembwe kweli.

Once bitten,twice shy.

Muda utasema.

Shule imeisha sasa niko huru kwa mijadala.
 
Turn and watch now.


Makundi mengi tu yameshaona Lissu ni Rais ajaye. Hakuna namna ya kumkwepa Lissu.

Lissu hakwepeki kwa sasa.

Siro ameshakubali yaishe, Mahakama walishakubali yaishe, bado wale wa vipepeo na NEC nayo inasuasua lakini iko mbioni.

Lissu ni kama Maji usipoyaoga utayanywa tu.
 
Kumsikiliza Lissu ili iweje sasa. Bora Magufuli anaweza akatamka neema kwa wafanyakazi, wamachinga, boda boda na mama ntilie.
Neema yeye ni Mungu. Hivi mbona mnapenda sana kuabudu masanamu?? Siku tutakapokuwa tunamzika kama Mkapa ndio mtajua kuwa kumbe alikuwa ni mwanadamu tu.

Tanzania ameikuta na ataiacha!
 
Yani unapima kiwango cha uharibifu wa mazingira tz kwa kumsikiliza mzungu kule marekani?

Zunguka ndugu ujionee!

Kingine nmeshakwambia hilo bwawa likikamilika litatoa umeme wa bei nafuu kisha mnaotumia mkaa mtaacha na kuanza kutumia umeme, na hapo mamilioni ya miti inayokatwa kwa ajili ya mkaa itapona na mzingira yataendelea kustawi.
Not quite true. Hydropower ni gharama.
Kuni na mkaa vitaendelea kutumika. Gesi ndio suluhisho bora kwa nishati nafuu.
 
Ha
Turn and watch now.


HaYa nimahojiano? Au nikampeni kupitia vyombo vya habari? Maana huyu mama mtangazaji hamuhoji tundu lisu badara yke anachokoza mada tu!
Alitakiwa aulize umeme wa maji, jua, gesi, upepo . Niupi wenye gharama nafuu??
 
Kwa watu kama nyie nipe cost ya kutengeneza offshore rig ili utoe Gas, nipe cost ya kutengeneza LNG plant upate Gas, nipe cost ya kutengeneza pipe ya kutoa Gas baharini hadi kwenye LNG plant na kutoka hapo kufika kiwandani.

Halafu linanginisha hizo cost na cost za hydro power uone hiyo investment ya kutoa Gas tu baharini utajenga hydro power ngapi.

Ni mtu anaejiropokea tu hajui finance, hajui uchumi na kuna kikundi tu cha wapuuzi wenzie wanamsikiliza si ajabu hajui Gas inayotoka baharini imechanganyika na maji inabidi uitoe kwanza kwenye maji ndio usambaze na kama unasafirisha uirudishe tena in liquid form.

Ni mtu anaeropoka ujinga tu
Mbona wewe ndiyo mjinga kuliko wote? Unajiandikia upumbavu mtupu kisha kwa akili zako za popo unajiona umeandika point? Acha ufala wewe kojoa ukalale acha wanaume waongee
 
Nimefatilia mahojiano ya Lissu na Farhia Middle katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV leo usiku,bila shaka ni moja ya kipindi kilichotazamwa na watu wengi nchini na nje ya nchi.

Taarifa zilianza kuzagaa jana katika mitandao ya kijamii hususani Facebook juu ya uwepo wake Itv leo.Nimefatilia sana na kaongea mambo mengi sana juu ya uchaguzi mkuu na kueleza mikakati yao kuelekea huko.

Nimeona Lissu anayo nguvu kubwa ya kuvishawishi vyombo vya habari kuanza kurusha habari zake.Ameongea mambo ya msingi kwa mstakabari wa taifa letu.

Ningeramani hata mh Magufuli ajitokeze ili aibadi ilani yake japo kwa ufupi ili baadae wananchi waachie nafasi ya kuona nani anafaa kwa maendeleo yao ya leo na kesho
Ajitokeze ili afarik
 
Walau aongei mambo ya kipuuzi kama Lissu hajui hata maana ya budgeting limiting factor yeye kila kitu atafanya na kuna mijitu ina amini; hizo hela atatoa wapi. Hata condition za kupewa mikopo na donors pia afahamu anaropoka tu.

Tundu Lissu is sick
Wewe mwenyewe hapo ulipo huna Ubongo kichwani umejaa kamasi debe mbili, tokea lini mpumbavu kama wewe akaweza kuyajua mazuri ya mtu mwelevu? Upumbavu ukikutoka ndipo uje kuandika vya maana lakini sasa bakia na upumbavu wako huko huko ulipo
 
Turn and watch now.

Nimesikiliza mahojiano ya Tundu Antipas Lissu na ITV kuhusu ahadi zake hewa (haelezi jinsi gani atawezedha km kila MTz awe na bima ya afya na mambo kadhaa). Anaishi kwenye ndoto lakini na matumaini kuwa hadaa zake zitafanikisha malengo yake.

Kwenye kampeni zake anatumia muda na nguvu nyingi kuhamasisha vurugu na si kushawishi wapiga kura kwa Sera. Lugha anayotumia kukejeli viongozi wenzake ni dhahiri akishika madaraka ya juu nchini hatakuwa "dikteta uchwara" bali dikteta kamili.

Msiyoyajua kuhusu Lissu, ambayo ni kitendawili cha shambulio dhidi yake.
 
Back
Top Bottom