Acha kupotosha.
Hakuna Sheria inalazimisha mikataba kuidhinishwa na Bunge. Ndiyo maana hata umeshindwa kuitaja.
Ibara ya 63(3) (e) ya Katiba ya JMT 1977, inatamka kwamba Bunge litaidhinisha mikataba kati ya Tanzania na nchi nyingine iwapo mikataba hiyo ina masharti kwamba Bunge ni lazima liridhie.
Na kisheria, mikataba inayotajwa hapo ni 'treaties' between Tanzania and other states' na siyo 'contacts with individuals or companies' yaani mikataba baina ya Tanzania na makampuni au watu binafsi haihusiki hapa.
Na hata Kama ingehusika, hakuna mikataba ambayo inalazimika kuidhinishwa na Bunge.
Kwa hiyo, ili mkataba uidhinishwe na Bunge, ni lazima uwe ni mkataba kati ya Tanzania na nchi nyingine, na pili, mkataba huo utaidhinishwa na Bunge iwapo mkataba huo utaweka masharti kwamba unahitaji idhini ya Bunge la JM wa Tanzania.