Uchaguzi 2020 Mgombea wa Urais wa Tanzania, Tundu Lissu afungiwa na NEC kufanya Kampeni siku 7

Uchaguzi 2020 Mgombea wa Urais wa Tanzania, Tundu Lissu afungiwa na NEC kufanya Kampeni siku 7

Same as Tz ni zaidi ya Meko na tume yake
Kinukisheni sasa! NEC wamemjibu Lisu kwa vitendo na kuonesha umbumbumbu wake wa kutojua sheria. Haya nanyi kinukisheni ili ile mikwara yenu tuone kwa vitendo
 
Tundu Lisu alipoandikiwa barua na kupelekwa katibu mkuu alisema yeye ndio inatakiwa afilishiwe, nyie mkashangilia kama kawaida yenu,

Sasa umeona wanaojua sheria walivyomjibu kwa vitendo?

Sheria unaijua? Sheria iko kwenye kitabu cha NEC...umekisoma wewe? Kama hujakisoma kaa kimya
 
Walikulalamikia we peke yako, mbona awakusema hadharani yepi awakubaliani nayo.

Lissu anadi sera zake za kuruhusu wafugaji kuingia mbugani, sijui kuongeza mishahara, kufuta kodi na porojo zingine. Sidhani kama kuna mtu angekuwa na shida nae tatizo ni huku kujifanya yeye ndio ‘alpha and omega’ ndani ya Tanzania.

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Hayo malalamiko yalikuwepo na kwa kuwa vyombo vya habari vimedhibitiwa ndio maana hukusikia malalamiko yao. Moja ya kanuni zilizolalamikiwa sana ilikuwa ni eneo lisemalo kuwa wakala wa chama cha siasa anaweza kupewa fomu ya matokeo iwapo itakuwepo. Ila ilibidi wasaini kwani ilikuwa usiposaini kukubaliana na huo uhuni, chama chako automatically hakitashiriki uchaguzi.
 
Mkuu Lisu anafikiri yeye ni mkubwa kuliko tz, akisapotiwa na wale mabeberu wake kina Amsterdam. Sasa wenzie wamemwambia kwa vitendo kwamba yeye si chochote hapa tz.

Tz ni zaidi ya Lisu na Amsterdam
Hapana mkuu, tume wamefanya kosa kama lililofanywa na Polisi. Hivi wanaogopa nini kumpelekea Lisu mwenyewe hizo barua zinazomhusu?

CCM angalieni hawa watu wanawahujumu.
 
Mkuu Lisu anafikiri yeye ni mkubwa kuliko tz, akisapotiwa na wale mabeberu wake kina Amsterdam. Sasa wenzie wamemwambia kwa vitendo kwamba yeye si chochote hapa tz.

Tz ni zaidi ya Lisu na Amsterdam

Hiyo buku 7 yako bado haija expire? Hujui unachoongea wewe.
 
Mkuu Lisu anafikiri yeye ni mkubwa kuliko tz, akisapotiwa na wale mabeberu wake kina Amsterdam. Sasa wenzie wamemwambia kwa vitendo kwamba yeye si chochote hapa tz.

Tz ni zaidi ya Lisu na Amsterdam
Mbona Meko anafanya nchi kama yake na mmefyata mkia?? Hafuati sheria anajiamulia tu?? Acha double standard ww
 
Sheria unaijua? Sheria iko kwenye kitabu cha NEC...umekisoma wewe? Kama hujakisoma kaa kimya
Hebu iweke hapa!

Lisu kila akitema boko mnashangilia kama mazuzu kumbe hakuna analojua!

Unaona sasa anaanza kulialia wakati yeye ndio alijifanya anajua sana sheria
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi.

============

Leo tarehe 02 Oktoba 2020 kamati ya maadili ya Kitaifa imesikiliza malalamiko dhidi ya Mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Bwana Tundu Lissu.

Malalamiko yaliwasilishwa na Chama cha NRA na Chama cha Mapinduzi. Chama cha NRA walilalamikia kitendo cha mgombea wa kiti cha Rais kupitia CHADEMA kutoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika. Ambapo akiwa mkoani Mara, alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. John Pombe Magufuli ameitisha kikao cha wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi. Pia imeelezwa kuwa alitoa maneno ya kichochezi na ya kudhalilisha kinyume na Maadili ya Uchaguzi akiwa mkoani Geita.

Barua ya kumtaka kujibu tuhuma hizo iliwasilishwa kwa Katibu mkuu wa CHADEMA kwa mujibu wa taratibu. Katibu Mkuu wa CHADEMA alijibu kuwa, malalamiko hayakihusu chama hivyo, mgombea na chama ni vitu viwili tofauti. Pamoja na kwamba Katibu mkuu wa CHADEMA alijibu barua ya malalamiko kuwa malalamiko apelekewe Tundu Lissu mwenyewe, kamati ya maadili imeridhika kuwa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji na Maadili iliwasilishwa kwa mlalamikiwa kwa mujibu wa taratibu kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 39 ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo bwana Tundu Lissu alidhaminiwa na CHADEMA kugombea kiti cha Rais. Hivyo, barua ya malalamiko kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu ni sahihi kabisa.

Once nec makes the ruling no appeal...this is full.of ...
 
Hapana mkuu, tume wamefanya kosa kama lililofanywa na Polisi. Hivi wanaogopa nini kumpelekea Lisu mwenyewe hizo barua zinazomhusu?

CCM angalieni hawa watu wanawahujumu.
Barua imepelekwa kwa katibu mkuu wa chama kinachomdhamini Lisu.

Kosa la nec lipo wapi?
 
Kama atafata sheria hakuna atakae msumbua lakini kaisha ona hali ilivyo mbaya akaamua kuhara majukwaanii.
 
Hiivi hawa watu wa tume familia zo zipo hapa hapa? Hiki wanacho kitafuta kikitokea tutaugulia wote hapahapa? Mbona wanazingua hawaaa?
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar.9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini. Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar.10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.! #Mwamba #AkiliKubwa #NiYeYe
 
Kusaini maana yake walikubaliana na hizo kanuni. Tatizo ninaloliona ni hii ya kupeleka barua kwa Katibu wa chama wakati anayetakiwa kujibu malalamiko yupo, na anajulikana yuko wapi. Polisi nao wamefanya kosa kama hilo.

Kuna watu wanastahili kuwajibishwa.

Sharti ilikuwa usiposaini hayo maadili automatically chama chako hakitashiriki uchaguzi. Na walifanya makusudi kuweka sheria na kanuni zenye nia ovu, ili wapinzani wa kweli Wagome kuzisaini ili ccm ishinde bila kushindana.
 
Hiivi hawa watu wa tume familia zo zipo hapa hapa? Hiki wanacho kitafuta kikitokea tutaugulia wote hapahapa? Mbona wanazingua hawaaa?
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar.9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini. Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar.10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.! #Mwamba #AkiliKubwa #NiYeYe
 
Na asipojirekebisha anafutwa kabisa kwenye uchaguzi,Lissu asijiropokee hovyo akahisi labda serikali haipo au inamuogopa wala asijifanganye.
Morgan Tshivangirai alikuwa kama Lissu lakini mwisho wa siku alipigwa spana na kaiacha Zimbabwe hiyo inasonga chini ya Zanupf.
Pepo mchafu aliyekuvamia akutoke haraka ili akili yako ikurudie
 
Back
Top Bottom