Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

TRA kamatieni hapo hapo ,hakuna mfanyabishara analipa Kodi Kwa hiari wote Huwa wanakwepa Kodi na risiti hawatoi
 
Report ya CAG inaonyesha viongozi wamejipakulia minyama yaani trillion 8.4 fedha za walipa kodi mmeona haitoshi mmeamua kuwaongezea utitiri wa kodi zisizoeleweka wafanyabiashara na watz kwa ujumla haikubaliki kodi za watz mnahonga mahawara zenu MA VAT XR cc February..,Madelu
 
Mkuu usirudie kufananisha nguruwe na vitu vya ajabu hayo maviongozi yenu ni manyumbu
 
Sio kila bidhaa inayouzwa inapitia bandarini, nyingine zinapitia mipakani ambapo Tanzania inazungukwa na nchi nyingi. Nyingine zinazalishwa ndani ya nchi
Huko nako zinakovuka kuna mamlaka ya forodha.
 
Mtumishi yeyote wa Umma analipa Kodi kubwa kuliko nyie wakwepa Kodi..

Serikali ingeondoa Kodi Kwa Watumishi Ili ibakie Kwa Wafanyabiashara, mtumishi anatoka Huduma Kodi ya nini kwake?
Mfanyabiashara ndiye anafanya wewe mtumishi ulipwe mshahara .
 
Hata huko mipakani nani angekwepa kulipa Kodi kama Kodi za hapa Tanzania zingekua rafiki kwa walipa Kodi? Mfano shati iliyoingizwa Uganda toka China utakuta Kampala Uganda bei ya leja leja inauzwa sawa na Tzs 3500. Lakini Shati hiyo hiyo imengizwa Tanzania toka China Kariakoo inauzwa bei ya jumla sawa na Tzs 14500. Ili Shati hilo liuzwe kwa bei ya leja leja sawa Tzs 15000. Kwa hapo ni nani anaye chochea biashara ya magendo mipakani? . Mfano mwingine kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia, kwa vile Kodi ya vitenge Tanzania ni kubwa sana, vitenge vilivyoingia Zambia kutoka China kupitia Bandari ya Dar, bei ya Zambia ni nusu ya bei ya Tanzania hivyo wafanyabiashara wanajaribu kuingiza vitenge Tanzania kutoka Zambia. Na kwa sababu Kodi ya Tanzania ya kishenzi ikitozwa hicho kitenge bei yake inaendelea kuzuia mzunguko wa biashara, mfanyabiashara atatafuta njia ya kukwepa Kodi.
 
Wana bahati wangefanya huo mgomo kipindi cha mwenda zake, sasa hivi tungekua tuna hesabu maiti za viongozi wa hilo soko.
Bila shaka wale wafanyabiashara za halali hawakuwa na shida na mwendazake
 
Kwani si walisema sahizi kulipa kodi ni kwa kirafiki kabisa sio kipindi kile kukimbizana, imekuwaje tena? Au huwa ni maneno yakupumbaza watu wasifikirie haki zao?
 
Na wewe unazijua sheria za wananchi?
 
Wewe unabiashara au ndo vile tumbo kuna wakati linasemea ulimi?
 
Mfumo wa Kodi wa nchi yetu ulibuniwa enzi za Mwalimu, wakati nchi ikiwa na azma ya kujenga uchumi wa kijamaa. Ujasiriamali ulitambulika kama ubepari ambao ulikuwa moja ya vitu vya kupigwa vita. Mfumo wa Kodi ulibuniwa pamoja na mambo mengine pia kupambana na ubepari, na ndio maana masharti ya mtu binafsi kuingia katika biashara yoyote ile yalifanywa kuwa magumu na viwango vya Kodi vikawekwa vya kukatisha tamaa. Bidhaa kama magari, fridge hata radio ziliitwa luxury goods na kubambikwa kodi hizi tunazoziona sasa.
Kwa kuwa tumeachana na dhamira ya kujenga uchumi wa kijamaa, serikali inapaswa kuufumua mfumo wa Kodi ili uendane na azma ya sasa, ya kujenga uchumi wa soko huria. Bila kufanya hivyo yanayoendelea Kariakoo pengine yatakuwa mwanzo tu wa lawama na machafuko kutokana na kodi kuwa kikwazo kwa maendeleo ya kaya na wananchi kwa jumla.
 
Ukiagiza mizgo ujue Tax charges ni almost 100% ya invoice. Angalia jinsi serikali isivyo fair.
 

Chadema na Act ni Branch za CCM
 

8. Ada za leseni manispaa
9. City levy 0.3%
10. Withholding Tax kwnye Russia mikataba ya pango kila mwaka 10%.
 
Wagome tu mpaka wanye TRA wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria unapokiuka hizo sheria ukabanwa mbavu wakilaumu bi wewe si TRA
 
Hakika nawashangaa sana watu wanaoweka tumaini kwa ukawa wakati wenyewe wanashibisha matumbo yao kwa kifupi hakuna tofauti ya upinzani na ccm labda tutegemee waibuke wanaharakati wengini tofauti na akina zito na mbowe ambao wakinyimwa asali wana midomo kama chiriku.
Chadema na Act ni Branch za CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…