Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Wafanyabiahara pekee ndo tunajua hii kero, hasa hawa vijana wa TRA, wanaingia tu hata mwaka hawana unaona wana ndinga za kil30, sa unajiuliza mbna mshahara wao hauwafikishi huko,
Wanataftia wafanyabiashara makosa ya jilimbikiza na kutaka tuwape hella, usipowapa wanakupiga mfine wa kiserekali ambao ni mil4 au 3
Hapo ni kukulazmisha uwape mil1 wakuache, ishanitokea hii, kosa wanalioungaunga kama matraffic tu, weziwezi sana hawa japaa, TRA wasipolegeza sheria zao au kupunguza kodi haya yataendelea sana,
Sheria za TRA hazitumiki kuendeleza biashara au nji, bali kifungo cha mfanya biashara, mpinzani wako akiwa anaelewana na TRA vzr ndo utakoma kuishi Tanzania
 
Kwani si walisema sahizi kulipa kodi ni kwa kirafiki kabisa sio kipindi kile kukimbizana, imekuwaje tena? Au huwa ni maneno yakupumbaza watu wasifikirie haki zao?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hawa chawa wa team wema hawafi kazi sana mkuu
 
Ukiagiza mizgo ujue Tax charges ni almost 100% ya invoice. Angalia jinsi serikali isivyo fair.
Mzee mmoja mfanyabiashara alinisimuliaa kuwa, Kodi ya customs ni kubwa na inataka kulingana na bei ya kununulia mzigo. Hapo wanachofanya ni kuunder value bei ya mzigo. Mfano Badala ya 100m unaenda customs anamhonga hela kama 2m jamaa anaandika 30m halafu unalipa kodi ndogo. Sasa shida inakuja baada ya mzigo kutoka bandarini 🤣🤣
Nyaraka zinakuwa hazijitoshelezi, hapo tra wakikaza itabidi wapewe rushwa tu.
Kiufupi shida ni kodi kubwa sana bandarini hivyo watu wanaundervalue mzigo. Huko mbeleni hakuna nyaraka, na kutoa risiti inataka vat 18%. Hapo faida ni ndogo na ukichanganya na gharama za kuendeshea biashara na hujuma na fitina za biashara lazima mtu uone chenga.


NB: pakija mfumo ambao ni automatic na centralized wa kodi kati ya bandari na tra. Watumishi wa bandari na TRA watakufa njaa 🤣🤣. Mnadhani mtu kaajiriwa mwaka mmoja tayari ana nyumba mbili, gari mbili kali na mchepuko wenye Tako kubwa, unadhani hela anatoa wapi? Ni rushwa hizi zinawapa hela.
Na tra wanatumika kwenye vita za kibiashara, na tra hawakosi kosa hata siku moja .

DeepPond uje uelezee kwa kina hizi kodi Watery
 
Kama Mjadala wa bungeni ulikuwa wa Kweli kwamba Container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 hapa Tanzania linatozwa Kodi ya Tzs 280milioni, Kenya Container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 linatozwa Kodi sawa na Tzs 35 milioni, na Zambia container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 linatozwa Kodi sawa na Tzs 30 milioni. Kodi za hapa Tanzania ni za kishenzi! Na zinaharibu uwezo wa Watu kununua bidhaa na hivyo kuvuruga mzunguko wa biashara na kuua mtaji ya watu.

Lakini pia nimeona wasafirishaji wa Malory wakisajiri Malory kwa plate number za Zambia na Congo. Kuna Tetes kuwa hela ya kununua na kusajali Lory moja hapa Tanzania ni hela ya kununua na kusajali Malory mawili kule Zambia na change kubakia. Nchi hii inatoza Kodi za kukomoana sana.

Nchi ina madini ina mbuga za wanyama, bandari bado tunahangaika na kodi za maskini. Huko serikalini rushwa zimejaa ndomana taifa halipigi hatua kodi ilibidi iwe last option.
 
Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali? mnaficha kitu gani? wanataka wazifahamu ili wawe wanazikagua, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.

Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.

NB.
Hao jamaa wanasema mfanyabiashara mwenzao yeyote atakayefungua duka ni halali yao, hivi wanazijua sheria za nchi?
Kuorodhesha biashara zako alafu TRA na police wakufanyie Uhanithi na ushenzi kama ule waliomfanyia yule mfanyabiashara wa kigoma mpaka leo analia na mke wake amekua mwendawazimu?? Kufanya biashara Tanzania kunahitaji uvumilivu sana na roho katili la sivyo hufanikiwi
 
Sijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra
Mzigo huohuo ukifika dukani unakutana tena na tra

Sasa najiulizaga yule tra wa bandarini ni tofauti na huyu wa dukani????
Na km wote ni TRA, hizi kodi za mara mbilimbili zinalenga nini????
Na hapo bado huja kutana na trafk,bira kisahau wale wenzetu wa fire lakini soko linaungua hwapo na hera usha toa🤣🤣

Jaribu jiulize y now siasa nimchongo kuliko elimu? Serikali yetu inaharibu sana mkuu
 
Hata huko mipakani nani angekwepa kulipa Kodi kama Kodi za hapa Tanzania zingekua rafiki kwa walipa Kodi? Mfano shati iliyoingizwa Uganda toka China utakuta Kampala Uganda bei ya leja leja inauzwa sawa na Tzs 3500. Lakini Shati hiyo hiyo imengizwa Tanzania toka China Kariakoo inauzwa bei ya jumla sawa na Tzs 14500. Ili Shati hilo liuzwe kwa bei ya leja leja sawa Tzs 15000. Kwa hapo ni nani anaye chochea biashara ya magendo mipakani? . Mfano mwingine kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia, kwa vile Kodi ya vitenge Tanzania ni kubwa sana, vitenge vilivyoingia Zambia kutoka China kupitia Bandari ya Dar, bei ya Zambia ni nusu ya bei ya Tanzania hivyo wafanyabiashara wanajaribu kuingiza vitenge Tanzania kutoka Zambia. Na kwa sababu Kodi ya Tanzania ya kishenzi ikitozwa hicho kitenge bei yake inaendelea kuzuia mzunguko wa biashara, mfanyabiashara atatafuta njia ya kukwepa Kodi.
Sasa unaona hoja hapo ni kodi kuwa kubwa wala sio kodi kukusanywa ndani kama huyo mwenzio alivyosema, maana alitaka kodi ikusanywe bandarini na border pekee. Jambo ambalo hutokaa ulipata maishani
 
Hii inatumika kama justification ya kuwasumbua wafanyabiashara K/Koo na sehemu zingine za biashara ktk nchi hii. But sababu kubwa ni kutaka rushwa tu, period!!!!!!!!!!!!
Muwe mnajielimisha kabla ya kuanza kulalamika na mjue mnalalamikia nini. Tatizo lenu kodi ni kubwa, sio kodi kukatwa ndani. Na kama kuna rushwa nalo ni tatizo jingine la kuzungumzia.

Nakuuliza hivi, nikiwa na hoteli kubwa 5 star, nikawa nanunua mahitaji ya hotel yote ndani ya nchi ni lini nitalipa kodi kama serikali inatoza kodi border na bandarini pekee? Au nyinyi import na export taxes kwenu ndio kodi pekee mnazojua.

VAT, property tax, sales tax, capital gain, witholding tax na nyingine zitatozwa wapi kama mnataka watoze bandarini na border pekee.
 
Jamaa yangu wa kariakoo ananitonya wanayopitia...nimemwambia tulia nchi inakwenda kufunguliwa...unapigwa mwingi.

1.mzigo unapoingia bandalini Kodi kibao
2.kodi ya mapato
3.leseni
4.service levi
5.fire extinguisher
6.usafi wa taka kajenjere na usafi wa jengo
7.kodi ya frem
8.choo
9.ulinzi frem
10.umeme
11.wafanyakazi
12.ulinzi store
13.kodi ya pango la store
14.kusajili ghala/store
15.kodi ya egesho la gari
16. kibari cha TBS
17 .bill ya maji na watu wa osha
 
Hivi kweli hatuwezi kuja na mfumo mmoja tu TRA pale bandarini kuchukuwa kodi mara moja ili mzigo ukitoka basi watu wasisumbuane? mbona kwenye mafuta wameweza mzigo kwenye meli unakatwa kila kitu basi unaingia sokoni. Kuna nini hii kila siku kukimbizana wakati Tech imekuwa sana kuna njia za kuchukuwa mapato kwa njia ya kisasa tu badala ya haya mambo ya double taxation watu hakuna kuaminiana kwanini lakini? kodi kulipa ni haki basi tuweke mfumo utakaonekana ni wa haki.
Unataka hao vishoka wakale wapi
 
Back
Top Bottom