Kwanini unasema kulipa kodi ni kuviziana, unaviziwa nini? Kama unalipa kodi sawasawa wanakuvizia kitu gani. Unataka wasije kukagua kwako unaficha nini?
Kwahiyo na wauza madawa muhimu wasiwe wanakaguliwa kwa sababu wanaviziwa. Wazalishaji viwandani wasiwe wanakaguliwa ubora kisa washapewa leseni hivyo wasiviziwe. Mahospitali binafsi yasiwe yanafanyiwa ukaguzi, watu wauziwe madawa yasiyo na ubora na madaktari wasio na vigezo kisa hospitali zisiviziwe.
Sheria ya kodi inasema kodi ikusanywe kila mnyororo wa thamani unapoongezeka. Na wewe unanunua kitu kwa 800, unakiuza kwa 1500 tiyari kuna thamani imeongezeka wanakuja kuchukua % kadhaa. Wakikusanya kodi kupitia mpakani na bandarini pekee Hyatt Regency, The Kilimanjaro italipaje kodi? Maana hainunui nyanya na kabeji nje, haipitishi nyama bandarini wala mpakani?
Nchi zenye mifumo mizuri ya kodi huwa zinavizia vizuri sana na ole wako ukutwe umekwepa kodi, jera nje nje.