Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Ni mifumo ya kiunyonyaji tu,, Hiyo ni double taxations. Mfano mwingine ni huu Mimi nikienda dukani kariakoo kuchukua mzigo na Kisha kupewa risiti yangu huwa Kuna Kodi nailipia..lkn mzigo huohuo nikileta dukani kwangu kuuza nakutana na TRA Tena ...kwhy ni mwendo wa kukamuana tu
Umenumua aliyekuuzia katengeneza faida kwa hiyo Kuna Kodi upande wake ambayo ataihamishia kwako kwa kuongeza Bei Fulani

Wewe unapoenda kuuza unaongeza bei unapata faida kwa hiyo Kuna Kodi kwenye faida yako, hii Kodi kiujanja utaihamishia kwa mnunuzi wako.

Sasa ulitakaje hapo? Aliyekuuzia awali katozwa Kodi kwenye faida yake
Wewe umetozwa Kodi kwenye faida Yako.

UBAYA NI PALE KIWANGO CHA KODI KINAPOKUWA KIKUBWA KULIKO. UHALISIA WA KIBIASHARA
 
Ndugu mwandishi wale wa kofia ngumu wameshaanza kurusha ule moshi unaotoa machozi?
 
Sijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra
Mzigo huohuo ukifika dukani unakutana tena na tra

Sasa najiulizaga yule tra wa bandarini ni tofauti na huyu wa dukani????
Na km wote ni TRA, hizi kodi za mara mbilimbili zinalenga nini????
Waweke kato moja ambalo litatembea mpaka kwa mlaji. Hii hali ya kutaka kodi kila muamala unapofanyika ni maumivu kwa mlaji wa mwisho.
Kuna sehemu vocha ya 500 ni 550 hadi 600.
 
Habari wakuu nipo mtaa wa mchikichi huku kariakoo maduka hayajafunguliwa hadi muda huu kuna nini kwani?

Ngoja niangalie na mitaa mingine.

img-20230514-wa0007-jpg.2622352
Muandika tangazo sijui alikuwa anakimbizwa 😂😂😂😂
 
Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa

Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana

Maduka yamefungwa ingawa baadhi ya wamachinga wanaouza matunda wanaendelea

Sijajua sababu ya msingi zaidi ya ile ya TRA kututaka tuorodheshe store zetu tunazohifadhia mali

Hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kwa jambo hilo ,Jambo lilihitaji mjadala mpana

Hakuna fujo ingawa polisi ni wengi wanatembea tembea bila uelekeo
View attachment 2622352
Hii mechi kati ya WEZI VS MAJAMBAZI ...bet your score..
 
Hebu twambieni kuna shida gani mkiorodhesha store mnazohifadhi bidhaa zenu? Shida iko wapi? Kwani ni kinyume na sheria? Kuna double taxation? Kivipi ni double taxation? Makadirio ni makubwa? Kivipi makadirio ni makubwa?
1. Itakua sio mfanyabiashara nchi hii
2. Hujawahi KUFANYA biashara nchi hii

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Serikali imezoea mabavu badala ya kuwaelimisha wahusika.

Haya sasa mukwara na maneno ya OLE WENU imekuwaje sasa?

Kodi ndiyo inayoendesha nchi. Kuikusanya kana kwamba ni vita na unyang'anyi ni kujipalia makaa
Hamna haja ya mikwara.....waachwe waendelee kufunga na ifanyike doria maduka yao yawe salama ili isitokee hujuma.

Mwishowe ukweli lazma usemwe mataita, wazito wote wa kkoo wanafanya biashara kutokea store, hawana fremu
 
Sawa kabisa, nawaunga mkono waliogoma kwa 100%

TRA kumejaa ufisadi na uonevu kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.

Nashauri Kariakoo iwe free trade zone, yenye flat rate ya ushuru na unaolipwa mara moja tu, ili kama nchi tunufaike na soko la nchi zinazotuzunguka.
 
Leo Kuna mgomo kwa wafanya biashara soko kuu kkoo kutokana na kila wiki uzinduzi wa kodi mpya

Baadhi ya kodi unazotakiwa kulipa

1: TRA.
2: FIRE.
3: JIJI.
4: USAFI.
5: Kodi ya store.
6: Makato 10% kweny commission (watu wa mihamala)
7: Kodi yakupeleka lori kkoo kubeba au kushusha mizigo

Makadilio ya kodi yamekua makubwa mno kiasi kwamba mtu akiangalia biashara yake na kodi haviendani. Kupungua kwa wateja wa nchi jirani kama Kongo,Zambia,Zimbabwe kutokana na kero ya TRA

Kwa wanaofnya biashara ya kusafirisha mizigo Jioni lzm TRA waje wafanye tasmini na Rushwa yao wanataka 3M kutokana na ukubwa wa mzigo
Alipoondoa migambo na ushuru kusema walipie 20, 000 kwa mwaka mlimuona chizi🤣
Sasa endeleeni kuteseka na huyu aliyefungua nchi. Na kuruhusu wapiga dili kila kona
 
Mimi sijaongelea bandarini tu nimesema TRA kwani unaweza kupita mpakani, bandarini au airport bila uwepo wa TRA? wako kila entry ya nchi waweke mfumo wa kisasa kukusanya kodi sio mambo ya kuviziana madukani mambo ya kishamba sana.
Bidhaa nyingi za dar es salaam zinategemea bandari kwa 90%
 
Hamna haja ya mikwara.....waachwe waendelee kufunga na ifanyike doria maduka yao yawe salama ili isitokee hujuma.

Mwishowe ukweli lazma usemwe mataita, wazito wote wa kkoo wanafanya biashara kutokea store, hawana fremu
Kwa nini hizi hoja mnaleta sasa badala ya kukaa nao?

Ukwrpaji kodi
Ukandamizaji kupitia kodi
Unyanyasaji wafanyabiashara....
Yote haya ni matokeo ya CCM kushikiliwa na majizi na kujazana serikalini.

CCM imefeli pakubwa
 
Umenumua aliyekuuzia katengeneza faida kwa hiyo Kuna Kodi upande wake ambayo ataihamishia kwako kwa kuongeza Bei Fulani

Wewe unapoenda kuuza unaongeza bei unapata faida kwa hiyo Kuna Kodi kwenye faida yako, hii Kodi kiujanja utaihamishia kwa mnunuzi wako.

Sasa ulitakaje hapo? Aliyekuuzia awali katozwa Kodi kwenye faida yake
Wewe umetozwa Kodi kwenye faida Yako.

UBAYA NI PALE KIWANGO CHA KODI KINAPOKUWA KIKUBWA KULIKO. UHALISIA WA KIBIASHARA
Mzigo mmoja kukata Kodi Mara mbili ni double taxations tu ndio maana mfanyabiashara mchuuzi ni ngumu kutoboa lkn pia ndio maana wafanyabiashara wakubwa wanakwepa Kodi.
 
Hebu twambieni kuna shida gani mkiorodhesha store mnazohifadhi bidhaa zenu? Shida iko wapi? Kwani ni kinyume na sheria? Kuna double taxation? Kivipi ni double taxation? Makadirio ni makubwa? Kivipi makadirio ni makubwa?
Kariakoo maduka yote ya vitu vya aina unayouza dukani kwako yndiyo stoo yako, hakuna duka utakwenda ukahitaji kitu ukaambiwa hakuna, unaambiwa subiri uletewe kutoka stoo, kinafatwa duka lingine unaletewa.

Simpo. Wenye mastoo ni wachache sana.
 
Habari wakuu nipo mtaa wa mchikichi huku kariakoo maduka hayajafunguliwa hadi muda huu kuna nini kwani?

Ngoja niangalie na mitaa mingine.

img-20230514-wa0007-jpg.2622352
Hawa wahini washughulikiwe.Yaani wanaingiza bidhaa za kutosha harafu wanazificha stoo ili kukwepa Kodi..

Serikali futia leseni Hawa watu na washtakiwe Kwa uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom