Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ebu project hiyo flat rate iwe bei gani kwa mfano???Sawa kabisa, nawaunga mkono waliogoma kwa 100%
TRA kumejaa ufisadi na uonevu kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.
Nashauri Kariakoo iwe free trade zone, yenye flat rate ya ushuru na unaolipwa mara moja tu, ili kama nchi tunufaike na soko la nchi zinazotuzunguka.
Huyo atakua afisa ubashiri hajui kadhia za kuwa na biashara nchi hii.1. Itakua sio mfanyabiashara nchi hii
2. Hujawahi KUFANYA biashara nchi hii
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Haukatwi mzigo mara mbili!Mzigo mmoja kukata Kodi Mara mbili ni double taxations tu ndio maana mfanyabiashara mchuuzi ni ngumu kutoboa lkn pia ndio maana wafanyabiashara wakubwa wanakwepa Kodi.
Najuwa hilo nilijibu tu kwa hoja ya mtu kusema kuna mipaka lakini shida kubwa hapa watu wa TRA wanajuwa kuwa kukiwa na mfumo usioingilika utaziba mianya ya rushwa watakufa njaa wanataka tubaki na hii analog mtu aweze tu kuamua kuna nini ndani ya container na gharama waamue nadhani kuna wakala wa kufanya clearance hawa wanatakiwa kuonesha 100% kuna nini na gharama zake ni zipi na viwango vya kodi viko kisheria ukiweka number kodi ni hii sasa kuwe na hali kuweka kiwango kuambatane na doc ku support gharama japo najuwa kuna ujanja mwingi mzigo wa mil 1 wanaweza kuweka laki moja hapa ndio tunatakiwa tutafute tech kuziba hii mianya kama shida kodi ni kubwa hilo na la kisera na serikali ina wajibu kuangalia. Mbona magari hakuna shida hizi, unaleta gari unaingiza model inakupa kodi hii wala huwezi kuchezea ndio maana ukija huku mitaani kwa wauza magari bei zinafanana sana.Bidhaa nyingi za dar es salaam zinategemea bandari kwa 90%
Hivi kweli hatuwezi kuja na mfumo mmoja tu TRA pale bandarini kuchukuwa kodi mara moja ili mzigo ukitoka basi watu wasisumbuane? mbona kwenye mafuta wameweza mzigo kwenye meli unakatwa kila kitu basi unaingia sokoni. Kuna nini hii kila siku kukimbizana wakati Tech imekuwa sana kuna njia za kuchukuwa mapato kwa njia ya kisasa tu badala ya haya mambo ya double taxation watu hakuna kuaminiana kwanini lakini? kodi kulipa ni haki basi tuweke mfumo utakaonekana ni wa haki.
Flat rate ya 10% itasaidia kuwa na mzunguko mkubwa sana wa pesa.Ebu project hiyo flat rate iwe bei gani kwa mfano???
Kodi inalipwa kwenye faida.....wanatengeneza faida zisizolingana unataka utoe flat rate?
Kkoo Kuna watu wanatoa makadirio mil 100 kwa mwaka? Je hiyo rate ndio itumike?
Yule ni tofauti...! Nazani yawezekana majukumu pia nitofautiSijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra
Mzigo huohuo ukifika dukani unakutana tena na tra
Sasa najiulizaga yule tra wa bandarini ni tofauti na huyu wa dukani????
Na km wote ni TRA, hizi kodi za mara mbilimbili zinalenga nini????
Wakiweka mfumo wa kodi haki na uwazi hao wezi wa TRA wanaolazimisha rushwa wakatajirikie wapi?Hivi kweli hatuwezi kuja na mfumo mmoja tu TRA pale bandarini kuchukuwa kodi mara moja ili mzigo ukitoka basi watu wasisumbuane? mbona kwenye mafuta wameweza mzigo kwenye meli unakatwa kila kitu basi unaingia sokoni. Kuna nini hii kila siku kukimbizana wakati Tech imekuwa sana kuna njia za kuchukuwa mapato kwa njia ya kisasa tu badala ya haya mambo ya double taxation watu hakuna kuaminiana kwanini lakini? kodi kulipa ni haki basi tuweke mfumo utakaonekana ni wa haki.
Hizo pesa wanazokusanya kwa nguvu hivyo mbona matumizi yake huwa ni ya kifisadi sana? Yani mtu apewe jukumu adokoe hela mchana kweupe na asiguswe. Kutii mamlaka katika mazingira haya ni ngumu mnoKuna mtu humu jf aliwahi kusema kuna wafanyabiashara wanaopitisha mizigo kutoka stoo na kuwauzia wamachinga bila kupitia dukani kwahiyo serikali imeona kuna pesa inapotea hapo.
Umakini wakufuatilia wangeweka kwenye pesa ambazo zinaliwa na mafisadi tungefika mbali kama nchi.Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, wanataka wazifahamu ili wakazikague, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.
Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Yani ww una matatizo..Tatizo limetokea May 2023, kitu cha kwanza unachofikiria ingetokea awamu ile wangeshatekwa.. kwani kipindi kile walikuwa wanadai kodi ya stoo? BadilikaHakuna mantiki yoyote ya kupiga Kodi dukani tena unapiga Kodi stoo kwenye bidhaa zile zile. Huo ni wizi siyo kodi
Ingekuwa awamu ya 5 waandaaji wa mgomo wangetekwa jana kabla ya mgomo kuanza leo..
Ulishawahi sikia kesi nyingi za Kontena za mitumba alafu ndani kuna Range Rover?Najuwa hilo nilijibu tu kwa hoja ya mtu kusema kuna mipaka lakini shida kubwa hapa watu wa TRA wanajuwa kuwa kukiwa na mfumo usioingilika utaziba mianya ya rushwa watakufa njaa wanataka tubaki na hii analog mtu aweze tu kuamua kuna nini ndani ya container na gharama waamue nadhani kuna wakala wa kufanya clearance hawa wanatakiwa kuonesha 100% kuna nini na gharama zake ni zipi na viwango vya kodi viko kisheria ukiweka number kodi ni hii sasa kuwe na hali kuweka kiwango kuambatane na doc ku support gharama japo najuwa kuna ujanja mwingi mzigo wa mil 1 wanaweza kuweka laki moja hapa ndio tunatakiwa tutafute tech kuziba hii mianya kama shida kodi ni kubwa hilo na la kisera na serikali ina wajibu kuangalia. Mbona magari hakuna shida hizi, unaleta gari unaingiza model inakupa kodi hii wala huwezi kuchezea ndio maana ukija huku mitaani kwa wauza magari bei zinafanana sana.
Mimi mwenyewe nisingekubali kulipa kodi ili nikamuongezee kitambi yule waziri..kodi zote zinaishia kwenye matumbo ya watu na bado tunakopa kufidia mashimoWalamba asali utawajua tu.
Je wewe ungeweza kulipia bidhaa ikiwa stoo na bidhaa hiyohiyo ulipie tena ikiwa dukani?Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, mnaficha kitu gani, wanataka wazifahamu ili wakazikague, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.
Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Unakemeaga matrillioni ya fedha yanayopotea serikalini hivihivi??Kodi lazima mlipe mnatabia ya kuficha Mali kwenye stoo harafu mnapeleka kiduchu dukani Ili mkadiriwe Kodi..
Mkigoma tunawafutia leseni na wote waliogoma hayo maduka tunayafunga marufuku kufungua.
Very simple hii mbona.Tanzania ni kubwa hapo Kariakoo ni sehemu.ndogo sana mapato yake kwa.mwka hayafiki hata Bil.500
Wao si wameshalipia kodi walipoingiza hizo bidhaa. Wauze tu.Kuna mtu humu jf aliwahi kusema kuna wafanyabiashara wanaopitisha mizigo kutoka stoo na kuwauzia wamachinga bila kupitia dukani kwahiyo serikali imeona kuna pesa inapotea hapo.