Biashara kkoo imegeuka hivi, machinga na stores!Sasa hivi hadi store nayo wanataka waitandike kodi!
Watu hawachukui fremu Bali stores, utauza huko huko store, no efd Kwan awali mzigo uliingia kimaghumashi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Biashara kkoo imegeuka hivi, machinga na stores!Sasa hivi hadi store nayo wanataka waitandike kodi!
Wamejiorganize vizuri ila wanachokiwakilisha kinaleta picha ya kutaka kukwepa kodi.wameshindwa kutumia watu wenye akili kubwa kuwasilisha hoja zao.Wana hoja dhaifu sana hata serikali kuzikataa ni kazi rahisi
Hoja ya kuviziana nimekubali uko sahihi. Hoja nyingine mbili haziko applicable.Umejichanganya kweli ngoja nijibu hoja zako, kama una TRA imara mzigo hautoki ila uwe umelipiwa kila kitu mbona mafuta wameweza? wanachukuwa mpaka VAT huko huko nenda kituo chochote cha mafuta utapata risiti lakini hukuti makato sababu wameshachukuwa. Mungizaji mali anatakiwa kulipa kila kitu mpaka VAT halafu akifanya mauzo yeye ana deal na TRA anaweza ku claim tax refund akiwa na vielelezo kilichoingia ingia kinalingana na alichouza. Hivi hujawahi kwenda nje ukanunua hata simu tu hapo Dubai unalipa VAT ila kama sio mkazi ukifika airport una claim VAT na ukionesha risiti unalipwa sababu mfumo umewekwa wa haki. Unaongelea nyanya hivi toka lini TRA wakakusanya kodi za nyanya hizo ni kodi zinalipwa sokoni na manispaa ndio wanakusanya kodi hizo. ukija mfano mdogo mafuta yakitoka bandarini yanakuwa yameshalipiwa kila kitu lakini mafuta hayo yanapita mikononi kwa wengi kabla kumfikia mlaji ila hukuti kodi tena inaongezeka kuna wale wanachukuwa mzigo jumla wanaweka kwenye tank zao na wao wanauza kwa wenye vituo na bei hizi zinatofautiana sehemu na sehemu lakini makato same na yameshakatwa. Kuvizia ni ujinga ndio sababu container linatoka bandarini halafu linaanza kufukuzwa mitaani kama TRA hawaaminiki kule bandarini badilisha mfumo kuondoa mianya ya udanganyifu ukiondoa urasimu unapunguza mianya ya rushwa. Kariakoo nzima hawawezi kuwa waizi ukiona kijiji kinalalamika ujue kuna shida.
Hao fanya wanatoza elfu 5 tu nayo ni kodi?Leo Kuna mgomo kwa wafanya biashara soko kuu kkoo kutokana na kila wiki uzinduzi wa kodi mpya
Baadhi ya kodi unazotakiwa kulipa
1: TRA.
2: FIRE.
3: JIJI.
4: USAFI.
5: Kodi ya store.
6: Makato 10% kweny commission (watu wa mihamala)
7: Kodi yakupeleka lori kkoo kubeba au kushusha mizigo
Makadilio ya kodi yamekua makubwa mno kiasi kwamba mtu akiangalia biashara yake na kodi haviendani. Kupungua kwa wateja wa nchi jirani kama Kongo,Zambia,Zimbabwe kutokana na kero ya TRA
Kwa wanaofnya biashara ya kusafirisha mizigo Jioni lzm TRA waje wafanye tasmini na Rushwa yao wanataka 3M kutokana na ukubwa wa mzigo
Hili tatizo linaanzia kwa viongozi wetu.Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?
Huu ni ukweli na ndicho serikali inacholenga kuzuiaKuna mtu humu jf aliwahi kusema kuna wafanyabiashara wanaopitisha mizigo kutoka stoo na kuwauzia wamachinga bila kupitia dukani kwahiyo serikali imeona kuna pesa inapotea hapo.
Wakigoma hata wili tu watakuwa wanaumeHamna ubavu wa kugoma nyie,mkale wapi?lipeni Kodi acheni janja janja,hakuna mjasiriamali kariakoo mwenye kuweza kufunga goli lake walau wiki moja,hakunaaa🙏
Huko ni kutaftana ubaya. TRA mwisho dukan tu. Kufatana store hairuhusiwiKuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, wanataka wazifahamu ili wakazikague, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.
Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Ulikuwa bungeni unafanya nini!?Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa
Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana
Maduka yamefungwa ingawa baadhi ya wamachinga wanaouza matunda wanaendelea
Sijajua sababu ya msingi zaidi ya ile ya TRA kututaka tuorodheshe store zetu tunazohifadhia mali
Hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kwa jambo hilo ,Jambo lilihitaji mjadala mpana
Hakuna fujo ingawa polisi ni wengi wanatembea tembea bila uelekeo
View attachment 2622352
Yeye mwenyewe sasa hivi yuko wapi?Wana bahati wangefanya huo mgomo kipindi cha mwenda zake, sasa hivi tungekua tuna hesabu maiti za viongozi wa hilo soko.
Hivi huyu daktari yupo nchi hii? Na bado ni mtumishi wa serikali?Kama Ulimboka alivyotekwa?
Serikali imezoea mabavu badala ya kuwaelimisha wahusika.Huu ni ukweli na ndicho serikali inacholenga kuzuia
Tumkumbuke nani? Acheni ujinga wenu!! Kariakoo ilikufa wakati wa DIKTETAMtanikumbuka
Wewe bwana najuwa kila kitu sasa ngoja nikupe darasa kidogo, hawa Kariakoo wafanya biashara umewasikia wanalalamikia kodi za Manispaa au kodi ndogo ndogo za ndani? kodi za mapato ni issue nyingine ni makadirio tu na huwa kama unaona kodi kubwa unaongea nao mnafikia njia sahihi japo shida kubwa ya wafanya biashara kukwepa kutoa risiti hili mimi nalipinga sana ni lazima tuwe na tamaduni za kutoa risiti inasaidia kuja kulipa mapato unakuwa na backup sahihi hii ni shida nyingine, malalamiko ni huko kukimbizana mitaani na wenye mizigo container limetoka basi kama limetoka bila kulipiwa basi wafanyakazi wa TRA au bandarini kuna shida hawaaminiki weka mfumo mtu hawezi kutoa kitu bila kulipiwa. Kodi za nje huku zina changamoto lakini tulipo sio pabaya sana tulikotoka. Kuwa na kodi moja kwa kila kitu kama kwenye mafuta wanakata kwa pamoja halafu wanawagawana huko.Hayo makato yana taratibu zake za kukatwa. Sio kwenye risiti. Kama wewe sio mfanyabiashara huwezi kujua.