Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Umejichanganya kweli ngoja nijibu hoja zako, kama una TRA imara mzigo hautoki ila uwe umelipiwa kila kitu mbona mafuta wameweza? wanachukuwa mpaka VAT huko huko nenda kituo chochote cha mafuta utapata risiti lakini hukuti makato sababu wameshachukuwa. Mungizaji mali anatakiwa kulipa kila kitu mpaka VAT halafu akifanya mauzo yeye ana deal na TRA anaweza ku claim tax refund akiwa na vielelezo kilichoingia ingia kinalingana na alichouza. Hivi hujawahi kwenda nje ukanunua hata simu tu hapo Dubai unalipa VAT ila kama sio mkazi ukifika airport una claim VAT na ukionesha risiti unalipwa sababu mfumo umewekwa wa haki. Unaongelea nyanya hivi toka lini TRA wakakusanya kodi za nyanya hizo ni kodi zinalipwa sokoni na manispaa ndio wanakusanya kodi hizo. ukija mfano mdogo mafuta yakitoka bandarini yanakuwa yameshalipiwa kila kitu lakini mafuta hayo yanapita mikononi kwa wengi kabla kumfikia mlaji ila hukuti kodi tena inaongezeka kuna wale wanachukuwa mzigo jumla wanaweka kwenye tank zao na wao wanauza kwa wenye vituo na bei hizi zinatofautiana sehemu na sehemu lakini makato same na yameshakatwa. Kuvizia ni ujinga ndio sababu container linatoka bandarini halafu linaanza kufukuzwa mitaani kama TRA hawaaminiki kule bandarini badilisha mfumo kuondoa mianya ya udanganyifu ukiondoa urasimu unapunguza mianya ya rushwa. Kariakoo nzima hawawezi kuwa waizi ukiona kijiji kinalalamika ujue kuna shida.
Hoja ya kuviziana nimekubali uko sahihi. Hoja nyingine mbili haziko applicable.

Kwanza, mafuta ya Tanzania yanapitia sehemu moja, Kigamboni. Yanashushwa sehemu moja hivyo ni rahisi kufuatilia kila kitu na wakati huo kafuatilie mfumo wa uagizaji wa mafuta wa bulky purchase utajua kwanini makato yake ni sawasawa. Mfumo huu huwezi utumia kwa muuza simu, huyu kanunua Oppo from China, huyu kanunua used Google Pixel from Dubai, huyu Apple from US.

Pili, Dubai sio Tanzania na ni exception duniani kufanya biashara. Mfumo wao ni mzuri kukaribisha wageni na uchumi wao umetengenezwa hivyo kuwa business hub na biashara zao zote kama real estate, bandari kubwa duniani, airport kubwa, hospitality, Fly Emirates & Fly Dubai inaungana kufanikisha mfumo huo wa uchumi. Kuna nchi nyingi sana tunaweza iga ila sio Dubai, gharama za kuifanya Dubai iwe vile tukizitaka mtakatwa kodi ya zaidi ya 50% na mtakimbilia kulima mihogo muachane na biashara.
 
Leo Kuna mgomo kwa wafanya biashara soko kuu kkoo kutokana na kila wiki uzinduzi wa kodi mpya

Baadhi ya kodi unazotakiwa kulipa

1: TRA.
2: FIRE.
3: JIJI.
4: USAFI.
5: Kodi ya store.
6: Makato 10% kweny commission (watu wa mihamala)
7: Kodi yakupeleka lori kkoo kubeba au kushusha mizigo

Makadilio ya kodi yamekua makubwa mno kiasi kwamba mtu akiangalia biashara yake na kodi haviendani. Kupungua kwa wateja wa nchi jirani kama Kongo,Zambia,Zimbabwe kutokana na kero ya TRA

Kwa wanaofnya biashara ya kusafirisha mizigo Jioni lzm TRA waje wafanye tasmini na Rushwa yao wanataka 3M kutokana na ukubwa wa mzigo
Hao fanya wanatoza elfu 5 tu nayo ni kodi?
 
Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?
Hili tatizo linaanzia kwa viongozi wetu.

Hakuna orientational ya kiswahili tena unapoomba kazi
 
ACHA WAITAMBUE SAWASAWA.

KWENYE CHAGUZI SINDO WAO HUWA WANAVAA KIJANI NA KUJINADI KUIPENDA SISIEM.


KAMA WANA MAPENZI YA DHATI NA HII NCHI WASIWACHAGUE SISIEM NDO TUTAJUA HAWATANIIII
 
No upumbavu mtupu kutaka mjue mpaka stoo za watu, hii nchi ya hovyo sana yaani mnataka kodi mpaka stoo!!!

Nipo kkoo hakuna mtu aliefungua labda machinga tu
 
Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, wanataka wazifahamu ili wakazikague, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.

Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Huko ni kutaftana ubaya. TRA mwisho dukan tu. Kufatana store hairuhusiwi
 
Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa

Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana

Maduka yamefungwa ingawa baadhi ya wamachinga wanaouza matunda wanaendelea

Sijajua sababu ya msingi zaidi ya ile ya TRA kututaka tuorodheshe store zetu tunazohifadhia mali

Hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kwa jambo hilo ,Jambo lilihitaji mjadala mpana

Hakuna fujo ingawa polisi ni wengi wanatembea tembea bila uelekeo
View attachment 2622352
Ulikuwa bungeni unafanya nini!?
 
Huu ni ukweli na ndicho serikali inacholenga kuzuia
Serikali imezoea mabavu badala ya kuwaelimisha wahusika.

Haya sasa mukwara na maneno ya OLE WENU imekuwaje sasa?

Kodi ndiyo inayoendesha nchi. Kuikusanya kana kwamba ni vita na unyang'anyi ni kujipalia makaa
 
Hayo makato yana taratibu zake za kukatwa. Sio kwenye risiti. Kama wewe sio mfanyabiashara huwezi kujua.
Wewe bwana najuwa kila kitu sasa ngoja nikupe darasa kidogo, hawa Kariakoo wafanya biashara umewasikia wanalalamikia kodi za Manispaa au kodi ndogo ndogo za ndani? kodi za mapato ni issue nyingine ni makadirio tu na huwa kama unaona kodi kubwa unaongea nao mnafikia njia sahihi japo shida kubwa ya wafanya biashara kukwepa kutoa risiti hili mimi nalipinga sana ni lazima tuwe na tamaduni za kutoa risiti inasaidia kuja kulipa mapato unakuwa na backup sahihi hii ni shida nyingine, malalamiko ni huko kukimbizana mitaani na wenye mizigo container limetoka basi kama limetoka bila kulipiwa basi wafanyakazi wa TRA au bandarini kuna shida hawaaminiki weka mfumo mtu hawezi kutoa kitu bila kulipiwa. Kodi za nje huku zina changamoto lakini tulipo sio pabaya sana tulikotoka. Kuwa na kodi moja kwa kila kitu kama kwenye mafuta wanakata kwa pamoja halafu wanawagawana huko.
 
Tukiachana na yote kkoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi. Watu wanafanyia biashara za mamilioni stoo.

kkoo wanaouza kwenye frem ni maskini tu wale wanaouzia kinyemela stoo ni matajiri wa kutupa sijui nani kasanua mchongo huu
 
Back
Top Bottom