Prince Luanda
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 2,255
- 2,825
- Thread starter
-
- #101
Hajui kodi inayo kusanywa hapo kkoo pekeyake, kuna wilaya nzima haifiki makusanyo yake yote ya kodii yanokusanywa kkooHii ni kkoo sio biashara yako ya kitumbua
Kitendo cha kkoo kugoma hta masaa mawili serikali yako ya ccm inapishana na kodi sio chini 1b
Kodi lazima mlipe mnatabia ya kuficha Mali kwenye stoo harafu mnapeleka kiduchu dukani Ili mkadiriwe Kodi..
Umejichanganya kweli ngoja nijibu hoja zako, kama una TRA imara mzigo hautoki ila uwe umelipiwa kila kitu mbona mafuta wameweza? wanachukuwa mpaka VAT huko huko nenda kituo chochote cha mafuta utapata risiti lakini hukuti makato sababu wameshachukuwa. Mungizaji mali anatakiwa kulipa kila kitu mpaka VAT halafu akifanya mauzo yeye ana deal na TRA anaweza ku claim tax refund akiwa na vielelezo kilichoingia ingia kinalingana na alichouza. Hivi hujawahi kwenda nje ukanunua hata simu tu hapo Dubai unalipa VAT ila kama sio mkazi ukifika airport una claim VAT na ukionesha risiti unalipwa sababu mfumo umewekwa wa haki. Unaongelea nyanya hivi toka lini TRA wakakusanya kodi za nyanya hizo ni kodi zinalipwa sokoni na manispaa ndio wanakusanya kodi hizo. ukija mfano mdogo mafuta yakitoka bandarini yanakuwa yameshalipiwa kila kitu lakini mafuta hayo yanapita mikononi kwa wengi kabla kumfikia mlaji ila hukuti kodi tena inaongezeka kuna wale wanachukuwa mzigo jumla wanaweka kwenye tank zao na wao wanauza kwa wenye vituo na bei hizi zinatofautiana sehemu na sehemu lakini makato same na yameshakatwa. Kuvizia ni ujinga ndio sababu container linatoka bandarini halafu linaanza kufukuzwa mitaani kama TRA hawaaminiki kule bandarini badilisha mfumo kuondoa mianya ya udanganyifu ukiondoa urasimu unapunguza mianya ya rushwa. Kariakoo nzima hawawezi kuwa waizi ukiona kijiji kinalalamika ujue kuna shida.Kwanini unasema kulipa kodi ni kuviziana, unaviziwa nini? Kama unalipa kodi sawasawa wanakuvizia kitu gani. Unataka wasije kukagua kwako unaficha nini?
Kwahiyo na wauza madawa muhimu wasiwe wanakaguliwa kwa sababu wanaviziwa. Wazalishaji viwandani wasiwe wanakaguliwa ubora kisa washapewa leseni hivyo wasiviziwe. Mahospitali binafsi yasiwe yanafanyiwa ukaguzi, watu wauziwe madawa yasiyo na ubora na madaktari wasio na vigezo kisa hospitali zisiviziwe.
Sheria ya kodi inasema kodi ikusanywe kila mnyororo wa thamani unapoongezeka. Na wewe unanunua kitu kwa 800, unakiuza kwa 1500 tiyari kuna thamani imeongezeka wanakuja kuchukua % kadhaa. Wakikusanya kodi kupitia mpakani na bandarini pekee Hyatt Regency, The Kilimanjaro italipaje kodi? Maana hainunui nyanya na kabeji nje, haipitishi nyama bandarini wala mpakani?
Nchi zenye mifumo mizuri ya kodi huwa zinavizia vizuri sana na ole wako ukutwe umekwepa kodi, jera nje nje.
Wana hoja dhaifu sana hata serikali kuzikataa ni kazi rahisiNani kakuambia petrol station hazilipi kodi za ndani?
Kwa kuwa mna maduka yenu siyo?Kodi lazima mlipe mnatabia ya kuficha Mali kwenye stoo harafu mnapeleka kiduchu dukani Ili mkadiriwe Kodi..
Mkigoma tunawafutia leseni na wote waliogoma hayo maduka tunayafunga marufuku kufungua.
Very simple hii mbona.Tanzania ni kubwa hapo Kariakoo ni sehemu.ndogo sana mapato yake kwa.mwka hayafiki hata Bil.500
Ni mifumo ya kiunyonyaji tu,, Hiyo ni double taxations. Mfano mwingine ni huu Mimi nikienda dukani kariakoo kuchukua mzigo na Kisha kupewa risiti yangu huwa Kuna Kodi nailipia..lkn mzigo huohuo nikileta dukani kwangu kuuza nakutana na TRA Tena ...kwhy ni mwendo wa kukamuana tuSijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra
Mzigo huohuo ukifika dukani unakutana tena na tra
Sasa najiulizaga yule tra wa bandarini ni tofauti na huyu wa dukani????
Na km wote ni TRA, hizi kodi za mara mbilimbili zinalenga nini????
Unapokuwa unapigania haki au kupambana na majitu madhalimu hautakiwi kuwazia vitisho vyao wakiteka wa kwenu wakamtesa na nyie mnateka wa kwao mnamtesa na kuwapa taarifa wajue kuwa mnalipiza.Muilize Dr. Ulimboka awamu ya nne alifanywa nini alipokuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari.
Weka risiti kama umejaza kituo cha mafuta onesha hayo makato. Kila kitu wanakusanya hukoAcha uongo. Kodi za mafuta ziko nyingi na hazitozwi bandarini tu. Kodi za mapato, ushurunwa halamashauri, PAYE, SDL n.k. vinatozwa nje ya bandari.
zaidi ya hapo kariakoo kuna machimbo kibao, wenyeji wanayaita machimbo jiulize kes nini.Sio kila bidhaa inayouzwa inapitia bandarini, nyingine zinapitia mipakani ambapo Tanzania inazungukwa na nchi nyingi. Nyingine zinazalishwa ndani ya nchi
Hajui kodi inayo kusanywa hapo kkoo pekeyake, kuna wilaya nzima haifiki makusanyo yake yote ya kodii yanokusanywa kkoo
Sent from my Q2 using JamiiForums mobile app
Hayo makato yana taratibu zake za kukatwa. Sio kwenye risiti. Kama wewe sio mfanyabiashara huwezi kujua.Weka risiti kama umejaza kituo cha mafuta onesha hayo makato. Kila kitu wanakusanya huko
Maduka yetu wapi? Endeleeni Kigoma.uone kama hatujafuta leseni na mnaanza upya na funawasaka..Kwa kuwa mna maduka yenu siyo?
Kama kidume kweli jaribu kufanya huo utopolo.
TRA inanuka rushwa halafu mnawanyanyasa walipakodi. Kwani tumesahau tozo ya kipuuzi ilivyotuumiza wananchi?
Try it and you will test your own broth
Shida ni kutafuta mchawi , watanzania ndio tunakwama hapo ndio sababu hatuwezi kutatua matatizo yetu.Ni kweli zina shida, ila hazijatungwa na TRA. Yani matatizo yetu makubwa ni kuongozwa na vilaza na watu wasioelewa, tatizo mara nyingi sio watekelezaji. Wafanyabishara watatumia TRA kukataa matakwa ya serikali ila serikali ndio ina shida wala sio TRA ambao ni mtekelezaji.
Serikali ikitaka kuwakataa na kuwaonyesha wanadai mambo yasiyowezekana itatafuta makosa kwenye madai yao. Waandae muswada mzuri wagome wakiwa na kauli nzito, sasa hivi ukiwatafuta utakuta kila mmoja anaongea la kwake sasa mgomo gani unafanikiwa hivyo
Kwan wamesema hawauzi. Ndugu ungejua huu mgomo una faida mara mbili kwa wafanyabiashara usingesema hapa. Sasa usianze kunichimba nikupe Siri za ndani ndani boss. Am sorry.Hamuwezi kugoma wiki nyie[emoji1787][emoji1787]kesho njaa na marejesho yatawarudisha kufungua hizo frem zenu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tanzania sio nchi ya kijamaa, ni ya kibepari zaidiSheria za ongezeko la kodi kutokana na mnyororo wa thamani , tumekurupuka , hizi ni system za kibepari hazifanyi kazi vizuri kwenye nchi zaa kijamaa .leo hii vat kwa kuepuka ugomvi na mamlaka wafanyabiashara wameziweka kama gharama ya biashara , maana ili ulipwe vat ni lazima ufanye biashara na kiwanda.
Sio wilaya, kuna mikoa haifikii kodi ya Kariakoo,Hajui kodi inayo kusanywa hapo kkoo pekeyake, kuna wilaya nzima haifiki makusanyo yake yote ya kodii yanokusanywa kkoo
Sent from my Q2 using JamiiForums mobile app
Aliye type alikuwa anatetemeka.Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?