Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Jana nilikuwa huko Kariakoo.
Kuna mgawanyiko baina ya Wafanyabishara.
Wapo watakaofungua na wapo watakaofungua.

Nilisikia Machinga wakisema wao sio wafanyabiashara. Wao wana umoja wao hivyo wao watafungua.

Wamachinga ni wale wenye vimeza wanaokaa na kuziba njia
Eti wanakaa na kuzb njia ,😐🙂
 
Kama hulalamiki basi unalia, then acha kulia
Hiyo utaamua wewe kama utaniweka wapi kama kwenye kulalamika au kulia ili mradi upate amani ndani ya nafsi yako,moja kati tatizo tulilo nalo baadhi ya binadamu ni kutopenda mtu mwingine kuwa na mtazamo tofauti na hoja yake au kile anachokiamini yeye,mara zote yeye hujiona kuwa ndiyo yupo sahihi.
Mtazamo huo siyo sahihi.
 
Unakuwa na kichwa kigumu mbona brother!?? Wakati najua muelewa kabisa Mimi sijajibu Kichwa Cha Uzi bali nimejibu comment ya mtu ..unafeli wapi dingii.??!.... Niliyemquote amesema wafanyabiashara wamefunga maduka lakini MACHINGA WAMEFUNGUA MADUKA hajasema MACHINGA WAMEFUNGUA BIASHARA ...amesema MACHINGA WAMEFUNGUA MADUKA ndio mzizi wa swali langu MACHINGA ANAFUNGUA DUKA KUANZIA LINI !?? DUKA GANI HILO LA MACHINGA !?? ..... Usiniwekee maneno mdomoni ambayo sijasema.... Sijaongelea kufungua BIASHARA ...naongelea MACHINGA KUFUNGUA DUKA ...MACHINGA YUPI HUYO ANAYEFUNGUA DUKA...NA WAPI HAPO KARIAKOOO MACHINGA MWENYE DUKA NIJE KUSHANGAA...... ambaye analipia TRA,service levy etc....

Uliyeni- quote ni Mimi mkuu.
Nimesema Wamachinga wao watafungua.
Jana nilikuwa huko Kariakoo.
Kuna mgawanyiko baina ya Wafanyabishara.
Wapo watakaofungua na wapo watakaofungua.

Nilisikia Machinga wakisema wao sio wafanyabiashara. Wao wana umoja wao hivyo wao watafungua.

Wamachinga ni wale wenye vimeza wanaokaa na kuziba njia

Embu soma vizuri.

Kufungua biashara haimaanishi unaduka
 
Nipe mchanganuo wa kodi kwa kuingiza kontena la vitenge kutoka nje pale bandarini kwa kulinganisha na maeneo mengine kama Zanzibar, Kenya, Uganda na Zambia.

Niwekee data siyo maneno ili twende sawa kwenye mdahalo huu.
Mimi sijawahi kufanya biashara ya hivyo vitenge hivyo kujua huo unaoita mchanganuo si rahisi lakini kwa akili za kawaida tu hilo jambo haliwezekani maana hakuna mfanyabiashara atakayekuwa tayari kuleta hiyo biashara nchini mwako lakini tambua nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki wana itifaki za kikodi hivyo hata kama nchi zitatofautiana katika viwango vya utozaji wa kodi lakini haiwezekani kutofautiana katika kiwango hiko.
 
Hadi Sasa ni saa 2:24 asubuhi maduka mengi hayajafunguliwa.


Licha ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuwasisitiza Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi Saa 9 Asubuhi Wafanyabiashara wengi wamefunga Biashara zao katika Mitaa ya Kariakoo, leo Juni 24, 2024

Awali, Chalamila akizungumzia taarifa za mgomo wa Wafanyabiashara wa #Kariakoo alisema "Yawezekana Wafanyabiashara wana Malalamiko ya dhati kabisa lakini Masuala ya mgomo yasichukuliwe kuwa ni jambo la pamoja."

Taarifa ya mgomo ilianza kusambaa kupitia vipeperushi ambavyo havikuwa na jina la Mwandishi, Juni 22, 2024 na sababu zilizotajwa ni kupinga masuala ya Kodi Kandamizi.

========
Pia, soma

Hadi Mo kagoma.
 
Mimi sijawahi kufanya biashara ya hivyo vitenge hivyo kujua huo unaoita mchanganuo si rahisi lakini kwa akili za kawaida tu hilo jambo haliwezekani maana hakuna mfanyabiashara atakayekuwa tayari kuleta hiyo biashara nchini mwako lakini tambua nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki wana itifaki za kikodi hivyo hata kama nchi zitatofautiana katika viwango vya utozaji wa kodi lakini haiwezekani kutofautiana katika kiwango hiko.
Kama haujawahi fanya usiwabishie wanaofanya, kaa uulize upate ukweli wa mambo ulivyo
 
Ukifunga duka lako, ukaweka mgomo kuuza bidhaa zako ni nani anapata hasara?
Ni serikali au ni wewe mwenye duka?
Tanzania ni kubwa sana na maduka ni mengi sana, Kariakoo ni sehemu ndogo sana ya Tanzania.

Sisemi wafanyabiashara wasitoe malalamiko yao, lakini kuna namna bora ya kuwasilisha malalamiko na siyo kufunga duka.
Tanzania ni kubwa sana, kariakoo ni ndogo sana.
Jaribu kufuatilia mambo boss.
 
Mbona hili ni swala dogo sana. Waache wagome watarudi wenyewe tena kwa kuomba msamaha. Siku tatu watarudi wenyewe maana watanzania hatunaga mazoea ya kuweka stock ya chakula ndani cha wiki nzima.

Huwa ni hand to mouth.
 
3048962_IMG_20211217_181857.jpg
Ulisoma shule gani wewe? Unajua impact ya hilo soko kwenye uchumi wa hii nchi?
 
Back
Top Bottom