Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Chura yy ndio tatizo namba moja katika ili taifa.wateule wake wanapiga rushwa nje nje yy KAZI kuwakumbatia tu.
Kisa yy kadalalia bandari yetu ndio maana anasema kula kwa urefu w kamba zako. Watanganyika tujipange sana kuhusu kizimkazi mwenyewe akistaff anaenda kwao znz.



KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kweli machinga wamefungua....mgomo huu hauwahusu.
Nipo K.Koo muda huu..

Machinga wana umoja wao...na kero zao.
Machinga hawana hata EFD...
Machinga hawalipi Service levy...
Machinga hawasumbuliwi na TRA...

Wamefungua na wanafanya biashara kama kawaida.

Walio funga hadi muda huu ni wamiliki wa maduka
Hawa wala hawakuwa na sababu ya kujifanya wajanja. Mitaji yao ni ya siku kwa siku, baada ya siku mbili wataishiwa products na watalazimika kuwatafuta wenye maduka

Na ndio shida ya nchi hii. Eti mfanyabiashara anashindwa kum support mwenzie kwenye wakati mgumu kisa yeye hana efd na mwenzie ana efd. Watanzania tuna safari ndefu sana
 
Madai yao yana-manktiki sana
Kodi wadhibiti huko viwandani na mipakani na bandarini

Vikiingia wahamasishe tu matumizi ya EFD basi wasichokonoe mambo Mengine kama wameshindwa kudhibiti kodi huko viwandan bidhaa zinakozalishwa au kupita hasira zao wasimalizie Kwa wafanyabiashara kariakoo
 
Na hili ndio tatizo la watanzania.

"No matter who you with or where you're at, or where to
"There's always gon' be three little pigs livin' near you"

Joyner Lucas
Mgomo wa maduka awahitaji wamachinga sababu wamachinga hawajui usumbufu wa TRA

Hata mwaka jana mgomo wa wafanyabiashara wamachinga hawakugoma
 
Jana nilikuwa huko Kariakoo.
Kuna mgawanyiko baina ya Wafanyabishara.
Wapo watakaofungua na wapo watakaofungua.

Nilisikia Machinga wakisema wao sio wafanyabiashara. Wao wana umoja wao hivyo wao watafungua.

Wamachinga ni wale wenye vimeza wanaokaa na kuziba njia
Hata mwaka jana mgomo wa wafanyabiashara wamachinga hawakugoma
 
Wafanyabiashara Kariakoo Waanza Mgomo

Hali ya mitaa ya Kariakoo kwa siku ya leo Juni 24,2024, ni ya ukimya baada ya maduka katika eneo hilo muhimu la biashara kufungwa.

Maduka katika mitaa maarufu ya biashara na misongamano kama mtaa wa Congo, Msimbazi, Uhuru yote yalikuwa yamefungwa.

Katika baadhi ya maeneo matangazo yameonekana yenye kichwa, Kufunga Biashara Zetu, "Tangazo kuanzia leo 24/6/2024 tunafunga maduka yetu kwa muda usiojulikana mpaka Bunge litakapo ondoa sheria kandamizi zinazopora mitaji ya wafanyabiashara," ilisoma sehemu ya tangazo hilo.

Vipeperushi juu ya mgomo huu vilianza kusambaa wiki iliyopita, huku viongozi wa wafanyabiashara hao wakionesha kuwa havikutoka kwao.

Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wametoa onyo kwa wafanyabiashara hao.
 
Back
Top Bottom