Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Wafanyabiashara Kariakoo Waanza Mgomo

Hali ya mitaa ya Kariakoo kwa siku ya leo Juni 24,2024, ni ya ukimya baada ya maduka katika eneo hilo muhimu la biashara kufungwa.

Maduka katika mitaa maarufu ya biashara na misongamano kama mtaa wa Congo, Msimbazi, Uhuru yote yalikuwa yamefungwa.

Katika baadhi ya maeneo matangazo yameonekana yenye kichwa, Kufunga Biashara Zetu, "Tangazo kuanzia leo 24/6/2024 tunafunga maduka yetu kwa muda usiojulikana mpaka Bunge litakapo ondoa sheria kandamizi zinazopora mitaji ya wafanyabiashara," ilisoma sehemu ya tangazo hilo.

Vipeperushi juu ya mgomo huu vilianza kusambaa wiki iliyopita, huku viongozi wa wafanyabiashara hao wakionesha kuwa havikutoka kwao.

Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wametoa onyo kwa wafanyabiashara hao.
 
Yamefungwa maduka ..... Nimemjibu aliyesema " wamachinga wamefungua maduka" ...acha ujuaji ...soma comment ya niliyemjibu..... Na wewe nakuuliza mmachinga ana fungua duka!??

Hapo ulipomjibu ndio imenukuu comment yangu ndio maana nikakuuliza.

Kwa hiyo uelewa wako biashara ni kufungua Duka?
 
Hao wafanyabiashara hawana lolote zaidi ya kutaka kukwepa kodi tu,nawashauri warudishe hizo fremu kwa wenyewe badala ya kuangaika na migomo isiyo na tija.
 
Jana nilikuwa huko Kariakoo.
Kuna mgawanyiko baina ya Wafanyabishara.
Wapo watakaofungua na wapo watakaofungua.

Nilisikia Machinga wakisema wao sio wafanyabiashara. Wao wana umoja wao hivyo wao watafungua.

Wamachinga ni wale wenye vimeza wanaokaa na kuziba njia

Sasa hao watafungua nini wakati wanatembeza na kupanga bidhaa barabarani?
 
Ukifunga duka lako, ukaweka mgomo kuuza bidhaa zako ni nani anapata hasara?
Ni serikali au ni wewe mwenye duka?
Tanzania ni kubwa sana na maduka ni mengi sana, Kariakoo ni sehemu ndogo sana ya Tanzania.

Sisemi wafanyabiashara wasitoe malalamiko yao, lakini kuna namna bora ya kuwasilisha malalamiko na siyo kufunga duka.
 
Ukifunga duka lako, ukaweka mgomo kuuza bidhaa zako ni nani anapata hasara?
Ni serikali au ni wewe mwenye duka?
Tanzania ni kubwa sana na maduka ni mengi sana, Kariakoo ni sehemu ndogo sana ya Tanzania.

Sisemi wafanyabiashara wasitoe malalamiko yao, lakini kuna namna bora ya kuwasilisha malalamiko na siyo kufunga duka.
Wew bwege hujawahi kuuza hata miwa kaaaa utulie usaidiwe na wenye utimamu Maan Akili yako Ni tegemezi
 
Hapo ulipomjibu ndio imenukuu comment yangu ndio maana nikakuuliza.

Kwa hiyo uelewa wako biashara ni kufungua Duka?
Unakuwa na kichwa kigumu mbona brother!?? Wakati najua muelewa kabisa Mimi sijajibu Kichwa Cha Uzi bali nimejibu comment ya mtu ..unafeli wapi dingii.??!.... Niliyemquote amesema wafanyabiashara wamefunga maduka lakini MACHINGA WAMEFUNGUA MADUKA hajasema MACHINGA WAMEFUNGUA BIASHARA ...amesema MACHINGA WAMEFUNGUA MADUKA ndio mzizi wa swali langu MACHINGA ANAFUNGUA DUKA KUANZIA LINI !?? DUKA GANI HILO LA MACHINGA !?? ..... Usiniwekee maneno mdomoni ambayo sijasema.... Sijaongelea kufungua BIASHARA ...naongelea MACHINGA KUFUNGUA DUKA ...MACHINGA YUPI HUYO ANAYEFUNGUA DUKA...NA WAPI HAPO KARIAKOOO MACHINGA MWENYE DUKA NIJE KUSHANGAA...... ambaye analipia TRA,service levy etc....
 
Back
Top Bottom