Mhadhiri SAUT adaiwa kuuawa kwa kunyongwa

huenda mama alikuwa na mtoto pekee wa kike huyo aliyeolewa hivyo urithi ungehamia kwa mwanae polisi ichunguze vizuri tukio hili haiwezekani mtu na mumewe kufanya mambo official ya kutafuta polisi kufungua geti as if kuna kitu walihisi hii huenda ni organized crime
 
Si umesikia walikuwa na miadi nae tangu hiyo jumatatu, ikabidi waende kumtafuta tena jumanne, yaani wewe uwe na miadi na mtu wako wa karibu siku nzima asipatikane usiingiwe na wasiwasi yupo wapi?
 
Mwanadamu kwa kawaida cha kwanza ni ulinzi lakini wengi walio na pesa wanaamini pesa ndiyo kila kitu, nataka nitowe wazo langu, katikafamilia wakwanza kupewa heshima msaidizi nyumbani anapika, anachota maji anakutengea chakula nakasumu hapo kumbuka mshahara mdogo.
 
Comment yako imenifanya nirudie kusoma upya uzi nione wapi ilipoandikwa "kijana wa kazi", sijaona...

Au kuna taarifa imebadilishwa kwenye uzi?
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza, Hamida Mussa maarufu 'Mama Mwakitosi' (64) anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mtandio shingoni na mfanyakazi wa ndani ambaye alitokomea kusikojulikana baada ya tukio hilo.

Mfanyakazi wa ndani ila kazi za ndani ni nyingi, ukizingatia ni jinsia mbili tofauti.
 
Hilo suala limenijia akilini pia. Nimeona huyo mwanae na mmewe wafanyiwe uchunguzi kwanza. Kuna vitu kama walivihisi kama kupiga simu na kuamua kwenda asubuhi na kisha kuita polisi halafu baada ya kuvunja inatokea kama ilivyotokea.

Hizo kadi za benki nazo zitamkamatisha mtu aliyefanya mauaji dk sifuri tu.

Huyo mfanyakazi pia ni suspect ingawa kama hajafanya itakuwa rahisi sana kumpata

Kingine ni uwezekano wa mtu kunyongwa na mtu mmoja nayo ina utata. Ina maana huyo mama hakuoiga hata makelele au ndio anakaa jumba liko mbali na majirani?

Ningesomea upelelezi tu maana uwa najiulizaga sana kwenye matukio kama haya

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Huyo mfanya kazi ana nguvu kiasi gani hadi afaniniwe kuuwa peke yake,duu bado nitakuwa mgumu kidogo kuamini.

Sitoshangaa serikali nayo kuchukua baadhi ya viungo kwa uchunguzi zaidi.
Hoja imeungwa mkono ukizingatia kuwa kadi za benki nazo hazionekani
 
mama aliajiri mtoto huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…