Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

Ndiomana nasema msihukumu kabla kujua tatizo lake lipi!! Subirini mshitakiwa akeletwe Mahakamani ndio mjue uyo Lecture kafanyanini??

Kutoka apo mtoe maoni yenu kwa uhuru!!

Lkn kile mnafanya kwasasa ni Chuki na Mapepo ya Uzwazwa✍️
Tatizo!tatizo! hivi hujui walimkamata kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano.Hapa ugaidi umetoka wapi tena?
 
Mambo ya Kisheria nyinyi mnafata mitandaoni wanasema nini ndio Uzwazwa👈

Wanasheria wake wenyewe hawajui kosa lake kufikia sasa
wanavavanya tu✍️
 
Hivi upo Tanzania hii au upo nchi za nje? Huyu lecturer alikamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano ndiyo taarifa walipewa wanasheria wake.Sasa ugaidi ni upi au unadhani kashikwa leo huyu?

Ndiomana nimekujibu Wanasheria wake wenyewe hawajui ukweli wa mashtaka ya uyo Lecture kufikia sasa👈

watajua mbivu na
mbichi iyo Agosti 5 ✍️
 
Dk Melikisedeki Kaijage, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026, sasa amebadilishiwa shitaka na kuwa la ugaidi na hivyo kunyimwa dhamana.

Awali, Jumanne Julai 21, Dk Kaijage alipewa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi Chang’ombe jijini humo tangu Julai 8, 2026, lakini kabla hajaachiliwa, akapewa shitaka hilo.

Soma pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Dk Gerald Shija amesema walibaini mabadiliko hayo wakati wanashughulikia dhamana.

“Mahakama ilitoa uamuzi kwamba atoke ndani, lakini wakati tunashughulikia dhamana, tukaambiwa amehamishiwa Gereza la Isanga,” amesema Dk Shija.

Amesema Dk Kaijage anatarajiwa kuletwa Mahakamani Agosti 5, 2026.

“Sijajua watampeleka mahakama gani, kwa sababu wamefungua kesi Mahakama ya Mwanzo ambayo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi,” amesema.
Na akome analeta ujuaji mbuzi wa kihaya? Sasa atasema "OF COURSE" nyingi huko korokoroni
 
Ndiomana nimekujibu Wanasheria wake wenyewe hawajui ukweli wa mashtaka ya uyo Lecture kufikia sasa👈

watajua mbivu na
mbichi iyo Agosti 5 ✍️
Aliyesema hayo ni jeshi la polisi walivyoambiwa yuko central wakaenda kumuona mteja wao.Kosa sio la wanasheria wake ni huyu muhusika jeshi la polisi taarifa aliyotoa.
 
Back
Top Bottom