Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

Mtumishi wa umma unatakiwa kuishi kwa kufuata maadili ya utumishi wa
umma
Ndio maana Sheria zinasema kama unataka kuingia katika shughuri za siasa unatakiwa kujiudhuru kazi za utumishi wa umma:
Mtumishi wa umma hatakiwi kujishughurisha katika shughuri za siasa au uwanaharakati;
Stay tuned
Sema mtumishi wa umma kama unaingia kwenye siasa basi ziwe siasa za CCM tu ndipo utakuwa salama nje na hapo umeisha
 
Wacheni kuhukumu kabla hamjajua katenda lipi!!

Sababu za kukamatwa zipo👈

Tuna wahadhiri wengi sana ni uyu tu kakamatwa.

Binadamu mwenzio usibebe zamadha yake kwanza jitaidi kujua tatizo nini!!

Mana hakuna Lecture mwengine kakamatwa niyeye tu👈
Wahadhiri wawili wa St. John's Uni nao wamekamatwa.
Hata mmoja kwa nini akamatwe kiuonevu!!??
 
Unampangia nini afundishe lecturer?, ndio maana Leo tuna wahitim wa vyuo vilaza kwasababu hawafundishwi mambo ya msingi... Mtoto toka Drs 1 anafundishwa historia majimaji war mpaka chuo kikuu!!. Ccm wameua elimu yetu .. hazitakaa zitoekee zama za akina SAMWELI SITTA walikuwa wanafunzi Bora sana ever.
 
Mtumishi wa umma unatakiwa kuishi kwa kufuata maadili ya utumishi wa
umma
Ndio maana Sheria zinasema kama unataka kuingia katika shughuri za siasa unatakiwa kujiudhuru kazi za utumishi wa umma:
Mtumishi wa umma hatakiwi kujishughurisha katika shughuri za siasa au uwanaharakati;
Stay tuned
Wale wa SJUIT ni watumishi wa umma!!??

Mwalimu wa Uraia darasa la tano akiwafundisha watoto wake kwamba maandamano ni haki kikatiba ni uhaini/ugaidi!!???
 
Dk Melikisedeki Kaijage, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026, sasa amebadilishiwa shitaka na kuwa la ugaidi na hivyo kunyimwa dhamana.

Awali, Jumanne Julai 21, Dk Kaijage alipewa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi Chang’ombe jijini humo tangu Julai 8, 2026, lakini kabla hajaachiliwa, akapewa shitaka hilo.

Soma pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Dk Gerald Shija amesema walibaini mabadiliko hayo wakati wanashughulikia dhamana.

“Mahakama ilitoa uamuzi kwamba atoke ndani, lakini wakati tunashughulikia dhamana, tukaambiwa amehamishiwa Gereza la Isanga,” amesema Dk Shija.

Amesema Dk Kaijage anatarajiwa kuletwa Mahakamani Agosti 5, 2026.

“Sijajua watampeleka mahakama gani, kwa sababu wamefungua kesi Mahakama ya Mwanzo ambayo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi,” amesema.
Nchi inaelekea sehemu ya hatari sana.Sheria hazitumiki tena bali utashi wa watu ndio unatumika.Haya mambo yalikuwa huko Rwanda,Russia,Venezuela,Nicaragua sasa yamefika kwetu.Lakini ni jambo la hatari mno
 
Wacheni kuhukumu kabla hamjajua katenda lipi!!

Sababu za kukamatwa zipo👈

Tuna wahadhiri wengi sana ni uyu tu kakamatwa.

Binadamu mwenzio usibebe zamadha yake kwanza jitaidi kujua tatizo nini!!

Mana hakuna Lecture mwengine kakamatwa niyeye tu👈
we nae ndo wale wale
 
Tungejua anachokizungumza lecture room na anachokifanya huko mtaani tungekuwa kwenye nafasi nzuri kujudge nani anayekosea.

Facts tulizonazo ni chache mno.
 
Dk Melikisedeki Kaijage, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026, sasa amebadilishiwa shitaka na kuwa la ugaidi na hivyo kunyimwa dhamana.

Awali, Jumanne Julai 21, Dk Kaijage alipewa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi Chang’ombe jijini humo tangu Julai 8, 2026, lakini kabla hajaachiliwa, akapewa shitaka hilo.

Soma pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Dk Gerald Shija amesema walibaini mabadiliko hayo wakati wanashughulikia dhamana.

“Mahakama ilitoa uamuzi kwamba atoke ndani, lakini wakati tunashughulikia dhamana, tukaambiwa amehamishiwa Gereza la Isanga,” amesema Dk Shija.

Amesema Dk Kaijage anatarajiwa kuletwa Mahakamani Agosti 5, 2026.

“Sijajua watampeleka mahakama gani, kwa sababu wamefungua kesi Mahakama ya Mwanzo ambayo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi,” amesema.

Mabadiliko huanzia vyuo vya elimu ya juu, bila wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu kujitokeza kwa wingi kuandamana kupiga watawala dhalimu nchi na maisha ya siku zijazo yamekwisha.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017


View: https://m.youtube.com/watch?v=M_0s8Cgd7pI
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament.

Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country.

Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile.
 
SHUJAA MSOMI ANAYETAKIWA KUUNGWA MKONO NA VYUO VIKUU VYOTE UDSM, SAUT, UDOM N.K KWA MAANDAMANO MAKUBWA DHIDI YA WATAWALA
1784822366198.jpeg

Photo : Dr. Melikisedek K. Kaijage

Tumuelewe Dr. Melikisedek K. Kaijage shujaa wa fikra tunduizi, usomi wake ameona mengi duniani, hususan kule Latin America maandamano dhidi ya udikteta wa watawala ni utamaduni wao, hawawezi kufisha hisia za Utu wa Watu na haki ya kupinga utawala

Mfano Kijana wa chuo kikuu Boric na maandamano ya vijana kule Latino america

Gen Z wametolewa kafara kwa sababu ya uchanga wao kwenye masuala ya kisiasa, Anayewalipa na kuwasakizia wakaingia barabarani anasubiriwa na hukumu ya Mungu.
KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO, WAKATI HUU 2025 / 2026 NI SAHIHI KUINGIA KTK NAFASI ZA MAAMUZI IKIWEMO URAIS


Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi, Vijana ni taifa la leo, watoto ndiyo viongozi wa kesho. Kauli za kilaghai kuwa vijana ni kwa ajili ya taifa la kesho siyo sahihi.

Vijana msihofu msuguano na wazee waliopo mamlakani, kusubiri kupewa ni kukubali kuwa tumejumuishwa na watoto chipukizi. Ni wakati wa vijana kuchagiza kwa mbinyo wa hoja kuwa uongozi wa nchi ni kwa ajili ya vijana.

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement:
59,554Views :2017 14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.

VIJANA NI WAKATI WA KUACHA KUTEGEMEA CHAMA DOLA KONGWE


Picha maktaba : Vijana chawa wa Vyuo vya elimu ya juu Tanzania.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

VIJANA KULE CHILE BARA LA LATINO AMERIKA WAMEWEZA

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME​

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
So, make it make sense for me, please.

Mhadhiri mmoja wa moja ya vyuo vikuu hapa nchini anatumia haki yake ya kikatiba iliyoandikwa na CCM, anawaambia wanafunzi wake waitumie haki yao ya kikatiba kupaza sauti zao juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

Mhadhiri huyo anakamatwa, anaswekwa jela, halafu anafunguliwa mashitaka ya ugaidi.

Papo hapo, kuna fala mmoja ajiitaye shehe Mwaipopo anaitisha hadi mikutano na waandishi wa habari, tena mara kadhaa, na kutoa kila aina ya vitisho vya kigaidi dhidi ya watu Wanaotaka kutumia haki zao za kikatiba.

Hadharani kabisa anadai kwamba ana makundi yake ya watu makatili sana ambao wako tayari kuwaua na kuwaumiza watu wataojitokeza kuandamana.

Lakini cha ajabu mtu huyo wala hakamatwi na polisi.

Hata waziri mwenye dhamana ya kulinda usalama wa wananchi hasemi chochote.

Hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyemkemea huyo shehe.

Make it make sense.

Nchi ya kifala sana hii.
 
Siasa za CCM zimefikia kwenye anguko.

Miaka ya nyuma hakuna watu walikuwa wapinzani kama wahadhiri wa vyuo vikuu na watumishi wa umma maana hili ndilo kundi la wasomi. Na walikuwa wanaendelea na maisha yao bila kubughudhiwa, zaidi sana ikitokea jina lake linatakiwa kufanyiwa vetting ilikuwa lazima likwame “huyu si mwenzetu”

Tangu enzi za Magu (RIP) na Samia sasa ni shurti kuwa shabiki wa serikali, acheni kulazimisha mahaba.

Kama Kikwete (role modo) wa Samia amekosa cha kushauri basi ni wazi kuwa hakuna namna nyingine zaidi ya mabavu.
 
Back
Top Bottom