Na Mwandishi wetu MBEYA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe John Mongella amepokea ujumbe wa umoja wa madereva wa daladala Mkoa wa Arusha ambao wameiomba serikali kuwahusisha wadau wa usafirishaji wakati vibali vya maandamano vinapotolewa kwa vyama vya siasa ili kuepusha usumbufu ambao madereva hao wanahofu kuwa utasababishwa na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo hapo kesho.
Mkuu wa Mkoa ameeleza kupokea mapendekezo yote yaliyowasilishwa na viongozi hao wa chama cha madereva wa daladala na kuahidi kufanyia kazi. Hata hivyo ameeleza kuwa maandamano ya Chadema ni kwa mujibu wa sheria na ni kutokana na azma ya Mhe. Rais kuhakikisha shughuli za kisiasa zinafanyika bila matatizo yoyote.
Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi wote wa Jiji la Arusha na maeneo ya karibu kujitokeza katika shughuli ya kuaga miili ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea Mkoani humo siku ya Jumamosi tarehe 24 Februari 2024 katika eneo la Bypass uelekeo wa Ngaramtoni.
Mkuu wa Mkoa ametoa angalizo kuwa shughuli ya kuaga miili itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia saa tatu kamili asubuhi. Aidha, ameeleza kuwa shughuli ya kuaga kama ilivyoombwa na viongozi wa dini ni utamaduni ambao ni wa kawaida na hivyo usihusishwe na suala la maandamano kwani vyote vitaweza kufanyika bila tatizo lolote.
----
Pamoja na ukweli kwamba Mkuu wa Mkoa wa Arusha anafahamu kuwa kesho tarehe 27 /02 /2024 ni siku kubwa ya Maandamano ya Amani Jijini humo kwa lengo la kupinga Ugumu wa Maisha pamoja na Miswada mibovu ya sheria za uchaguzi , lakini ameamua kuifanya siku hiyo pia kuwa ya kuaga miili ya Marehemu wa Ajali .
Ni dhahiri kwamba RC anapanga ratiba hiyo ili kupambana na kujaribu kuvuruga Maandamano ya Wananchi , lakini atashindwa vibaya sana , kwa haya yanayoendelea sisi wengine tunaanza kuitafakari minong'ono ya wadau ya kudai kwamba " Huenda ajali hiyo ilipangwa kwa lengo la kuvuruga maandamano "
Itakuwa Aibu kubwa sana kwa Nchi ikiwa minong'ono hii ina ukweli wowote na kuna Hati hati ya Wananchi kushinikiza baadhi ya viongozi kujiuzulu .
Ngoja tuone.
Soma: