Mimi kitaaluma kabisa ni muhasibu japo ninayoyafanya sshv ni nje ya hiyo prof, nimesha fanya kazi hiyo japo sikufika mbali nikachochora, najua hekaya za hawa mabwana na nina mifano hai ya madhila yanayo wakuta waasibu, nimesha wahi simulia siku moja mkasa mmoja wa muhasibu fulani kwenye moja ya thread japo siikumbuki ilikua ina husu nini, ila ili pelekea nikakumbuka huo mkasa na kuuchangia! Labda kwa fikra ndogo tu! Tofauti na ishu za ugoni nini kingine kinaweza kikasababisha tukio kama hilo kama sio zuluma ama ukuda makazini!? Kuna mahala tuliajiriwa kama wahasibu wanne hivi tukapewa tutorial ya kazi yao jinsi wanavyofanya, awali nilishituka, kulingana na utaratibu wao ikabidi tufanye kadiri walivyokua wanataka, kumbe tulikua mbuzi wa kafara