Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pasco siasa mchezo mchafu! Jioni utawakuta hivi!
![]()
![]()
Hivi vyeo vya JF, sivielewi. By the way ongera pasco
Bunge halina kazi waondoke tu watusamehe hizo kodi zetu wanazotafuna kila siku kwa kukaa bila kazi, ndio maana Zitto ameamua aende zake kigoma kufanya shughuli za chama! Shame on them! Bunge linaogopa kuisimamia serikali sasa kazi yake ninini hasa?
hakuna kitu alifikiri kujichezesha na tindo ndio kubembeleza urafiki wa kaisari tindo inabomoa miamba migumu hadi inatoa dhahabu na almasi uliza machali watakuambia jinsi ya kupata tanzanite lazima uwe na tindo lisu kali iliyonolewaha ha haaaaa!!!,nimecheka mpaka basi kweli kikulacho kipo nguoni mwako.
Wanabodi,
Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.
Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.
Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.
Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.
Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.
Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.
Pasco.
Niheri mumpe DR silaa urais kuliko Tundulisu awe mbunge.asante muumba nikweli