Mheshiwa Lissu kajitetea vibaya kwenye kipengele cha heshima kubwa aliyonayo kimataifa

Alichokisema kabla ya kukamatwa kilichochea kilichotokea Oct29, hasa kutokana na heshima aliyonayo kitaifa na kimataifa kama alivyokiri mwenyewe kuwa heshima hiyo anayo kubwa.
Heshima aliyonayo nje na ndani ya nchi ni kwasababu ya kutetea haki za binadamu na kupigania demokrasia ya kweli.

Je, hiyo ni sifa mbaya ama nzuri kutetea haki za binadamu na utawala bora?

Kwanini usiseme pia kiburi cha watawala kutosikiliza maoni ya watu mbalimbali, jumuia za kimataifa, kikanda ,asasi za kiraia na taasisi za kidini kwamba uchaguzi uahirishwe hadi pale itakapopatikana katiba yenye usawa kwa vyama vyote, ndicho kilichosababisha machafuko yale?

Ni wananchi wenyewe waliochoshwa na maigizo ya uchaguzi ndiyo walioamua kuonesha hadharani kutopendezwa kwao na kilichokuwa kinaendelea.
 
Mfano kwa mazingira yaliyopo hivi sasa ukalazimisha kwenda kwenye uchaguzi 2030 kwa katiba hii hii na sheria za uchaguzi hizi hizi halafu yakatokea yaliyotokea uchaguzi uliopita bado utamlaumu Lissu?

Jaribuni kuruhusu watu watoe madukuduku yao kwa uwazi bila kuwabughudi uone watakavyofunguka wala hawashikiwi akili na mtu yeyote bali wananchi wengi kwasasa wameshajitambua sana.

Binafsi ni mtu huru sijihusishi na chama chochote lakini huku mitaani tunapoishi watu wamechoshwa na maigizo ya chaguzi zetu wanataka uwanja uwe sawa ushindani uwe fair ili wakishinda chama tawala ama wapinzani basi waridhike.
 
Mleta mada, pole sana, umedhihirisha uwezo mdogo wa akili.

Kwanza kufanya uasi kwa jambo inalojua ni batili, siyo kosa. Na kamwe haliwezi kua ni uhaini. Hata wewe, kutiba unakuelekeza kuasi chochote kilicho kinyume cha katiba, mara unapogunfua. Lisu ameeleza vizuri sana. Katiba yeti inatamka kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, Lisu ameeleza na kutoa vithibitisho mbalimbali kuwa chaguzi zetu siyo huru na za haki. Hivyo wananchi watii katiba, walistahili kufanya uasi dhidi ya mfumo unaodanya uchaguzi usiwe huru na wa haki. Kiuhalisia ni kwamba walipridhia kushiriki uchaguzi wa namna hiyo, huku wakijua, kwa mujibu wa katiba yetu, ni wahalifu. Vithibitisho vya kuwa mifumo ya ucjaguzi wa Tanzania haina uwezo wa kuufanya uchaguzi huru na wa haki, ni pamoja na taarifa za tume mbalimbali kuanzia ile ya Jaji Nyalali, na wengine wengi, na taarifa za taasisi mbalimbali za watazamaji wa kimataifa. Na hayo yote Lisu ameyaeleza na kuyafafanua vizuri sana.

Ni mwendawazimu pekee anayeweza kusema kuwa neno kukinukisha ni uhalifu. Nenda kasome hata kamusi ya Kiswahili ujue maana ya kunuka, kunukisha.
Kwa tafsiri rahisi, kama unafanya hadaa, na unaheshimika na jamii, mtu anayekuja kuanika uovu wako, hapo amekunukisha, kwa sababu anawafanya watu waujue uhalisia wako, kuwa wewe unafanya hadaa, na baada ya hapo hutaheshimika, utanuka.

Mwendawazimu pekee ndiye anaweza hata kufikiria kuwa kusema nitakinukisha, ni kosa la jinai.
 

Kuna vitu vingine hekima inakua ni kunyamaza au kujifunza na kusikiliza wanaoelwa.

Sasa iko hivi, TL alieleza mwenendo wa chaguzi zilizopita na malalamiko kutoka kwa tume kadhaa ikiwepo waangalizi wa kikanda na kimataifa, wote wakinyooshea kidole mapungufu na kutoa mapendekezo ya kutatua kero hizo.

Tahadhari mojawapo ikiwepo kwamba endapo baadhi ya mambo hayatafanyiwa kazi, ipo siku uchaguzi utaleta machafuko.

Sasa TL hakukana hayo maneno ya NRNE akimaanisha uchaguzi ufanyike kwa tume huru na mapendekezo ya tume zilizotangulia yafanyiwe kazi, vinginevyo, matokeo ni yale yale, uchaguzi hauna maana.

Sasa kwa mantiki hiyo, kwanini akatae kwamba hakusema bila mabadiliko, hakuna uchaguzi?
 
'Mahakama hii haiangalii uzito wa ushahidi wala kuaminika kwake' Jaji Ndunguru
 
Uchaguzi kumefanyika yupo ndani, Sasa asiseme ya moyoni na huo ndio ukweli!


Mambo ya kisheria yanaongozwa kisheria
Sio kwa hisia zako tuπŸ‘ˆ

Kisheria inasomeka ivi

Mh Lissu kawasha MOTO πŸ’₯ wa hatari
JAMHURI imemkamata hasije kukimbia mana tayali kawasha MOTO
Wkt Lissu yupo Lupango ule MOTO uliendelea zaidi na zaidi mwisho ukaenda kuuwa na wananchi mali ya Jamhuri

Mh Lissu anashtakiwa kwa kuwa yeye ni chanzo cha ule MOTO βœ…οΈ
 
Tukio limetokea muda mrefu baada ya matamshi yake na mhusika akiwa gerezani.
 
Manake kuna vichwa vengine tumimie hesabu za vijiti ndio tutaelewana🀠🀠
 
Acha ujinga na uccm wako.nyie ndo wajinga mnaotuharibia nchi.
 
Tukio limetokea muda mrefu baada ya matamshi yake na mhusika akiwa gerezani.

Nisawa tu na MOTO ukiwasha mpaka ule MOTO uhakikishe umezimika

Sasa mh Lissu kilichomponzo zaidi ule MOTO wake yeye akiwa chanzo MOTO umeendelea kutoka mwezi wa 4 mpaka mwezi 10 kuendelea mwezi wa 11

Chanzo ni MOTO πŸ’₯
Na ni kilekile chake
yeye πŸ‘ˆ
ndiomana hakukamatwa mwengine yoyote mana niyeye ndio chanzo ✍️
 
Logical non sequitur fallacy.

Not even wrong.

Meaning, less than wrong.

Meandering rubbish.
 

Ukipata muda lekebisha kwa faida ya wasomaji ❗️
Nami nitakujibu
 
Naam. Moto ni wale walioagiza na waliofyatua risasi kuua. Ila chanzo ni huyu bwana...
 
Chawa anaona kafanya analysis ile mbaya yani, haya umejitahidi.

Ulifundishwa multiple choice?πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›
Mheshimiwa alijikweza sana mwenyewe kimataifa bila kujua anajishusha mwenyewe kitaifa. Heshima yake hiyo alipaswa kuchunga sana ulimi wake na matendo yake kwakuwa ni rahisi kuigwa na kutekelezwa na wanajamii ambao wanamheshimu sana. Ni role model kwa vijana kutokana na heshima yake hiyo kubwa, anachokiagiza ni sheria kwa wanaomheshimu.

Maneno yake yalitosha kusababisha vurugu zile.
 
Crap πŸ’© πŸ’© πŸ’©
 

Attachments

  • downloadfile-4.png
    1.4 MB · Views: 8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…