Mheshiwa Lissu kajitetea vibaya kwenye kipengele cha heshima kubwa aliyonayo kimataifa

Kavulana ndiyo umeandika upuuzi gani? Kesi ya Lissu haina tofauti na wale wanaotumia mstari mmoja wa Biblia kuhalalisha uovu wao.
Hoja ya Lissu ni kuwa inakuwaje aliongea masaa zaidi ya 3 lakini wakachukua sentensi moja tu?
 
Aliyasema lini na vurugu zilifanyika lini? Na neno lake linaishi milele kuliko hata Kilimo Cha Kufa Na Kupona la Mwalimu Nyerere?
Tafsiri ya kuzuia uchaguzi ni kwa njia gani na KUKINUKISHA maana yake nini?
Usiokote hisia zako majalalani na kuzisokomeza kuwa ndio tafsiri sahihi
 
Hujui good character ni relevant kwenye criminal cases?

Utetezi wa good character ni muhimu kwa mshitakiwa kwasababu unamsaidia kujisafisha dhidi ya tuhuma mbaya anazokabiliwa nazo.
Naona umeniwahi, nami nilitaka kumuuliza swali hili...kakurupuka tu huyu mleta thread..
 
kavulata naomba uzi wako wowote, au comment yako yoyote uliyowahi kumsema Tundu Lissu kwa wema.
Ukifanya hivyo ndipo utapata uhalali na kibali mbele za Mungu
Soma threads zangu kuhusu Lissu kabla ya No reforms no election na kususia kutia saini kanuni za uchaguzi. Mimi simchukii mtanzania mwenzangu kwakuwa nimeshavuka huko. Hata sasa simchukii ila namchukia mtu yeyote anaetumia jinsia ya Rais Samia kumdharau na kumchukia bila sababu.

Kwa mahaba ya Samia kwa Lissu hakustahili kusumbuliwa na Lissu kama hivi anavyomsumbua na kumbeza.

Hata wewe mheshimiwa utakuwa hutendi haki kama utamfurahia mtu yeyote ambae anadai haki kwa kutuharibia miundombinu yetu inayotudumia ambayo iliyotugharimu sisi wote kuijenga
 
Dah 😅😅😅

Walau ungewauliza wenzako kwanini Lissu alifanya hivyo.
 
Hapo kwenye "anakili".

Amandla...
 

Punguzeni mihemuko, uliwahoji wale wale walioandamana wakakwambia walikuwa wafuasi wa Tundu Lissu?? Polepole si alionya na hamkusikia? Mwl.Nyerere aliwahi kusema,"Taifa linawahitaji vijana jeuri wliotayari kuhasi kwa ajili ya uzalendo kwa Taifa lao" wewe utaendelea kuwa chawa mpaka lini?? Muachieni Tundu Lissu hana kesi.
 
Kumbe unajua yanaenda kisheria, Sasa mdomo wa nini?
 
Hata Samia anayo heshima kubwa kimataifa baada ya kupewa tuzo na nchi za nje, huu si uhaini bali ni sifa.
 
Mliua harafu mnatafuta upenyo? Nchimbi alishapeleka ushahidi wa mauaji yenu na makaburi ya haraiki kashayaonesha yalipo, kwa ushauri nendeni mkafukue tena mpeleke sehemu nyingine msipoteze muda kuomba huruma
 
Si ni bora kwenu huko lumumba.
 
Ulitaka Lissu aseme ana shahada 8 za kupewa kama Samuya wakati darasani alitoka na 0 ndio uridhike?

Vilaza wa mtindo wako ndio aliowataja mnapenda multiple choice questions na sio critical thinking.
 
Uko sahihi kwa hilo, hata hivyo ndio maana ikatenganishwa kati ya kuua kwa kukusudia na kuua bila kukusudia, na adhabu zake ni tofauti kabisa (mbingu na ardhi). Kwanza lazima tuipate orodha kamili ya watu wooote waliouliwa, kisha tuipate orodha ya watu woooote walioua, kisha tuipate orodha ya watu wooote waliouliwa kihalali na kimakosa ili tujue nani alipwe fidia na nani aadhibiwe.
 
Uchaguzi kumefanyika yupo ndani, Sasa asiseme ya moyoni na huo ndio ukweli!
Kusema alikuwa ndani siku ya uchaguzi ni Janja ya nyani kula mahindi mbichi!
Katika kufanya uhalifu kuna watu wa aina tano hivi:
1. Anaepanga uhalifu/mapinduzi - ana mbinu zake za kufanikisha
2. Anaepeleleza na kupelemba/anaefundisha namna utakavyofanyika - ana mbinu zake
3. Anaegharamia - anazo mbinu na njia zake za kufanikisha kugharamia
4. Anaetekeleza - ana mbinu zake
5. Anaefaidika/anaetumia/anepelekewa - na yeye amejipanga/wamepangana kupokea faida.

Watu hawa watano hawafanyi kazi kwa wakati mmoja mara moja. Hoja ya kwamba alikuwa ndani siku ya tukio ni kujifanya mjuaji tu.
 
Tofauti Yako na Lissu.

Lissu ni mkweli, asiye na hofu kusimamia Ukweli.
Wakati wewe ni Mnafiki.

NB: Hata Mungu hapendezwi na Wanafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…