Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Bado aina ya elimu inayotolewa nchi hii haijamkomboa kijana kujenga fikra za kukiajiri
 
Nafikiri kukosa wazazi wa kumshauri vzr na yy kutojichanganya ndg na jamaa wengine ili kupata mawazo mbadala ya kuendesha maisha yake ndio kungetajwa kuwa chanzo cha kujiua kwake ningemuelewa.

Otherwise ni mlevi asiye na staha ugoro + pombe kali lazima achizi na kujiua ndio option rahisi kwake kwani hana washauri au washauri wake nao ni ugoro + cuca, ananas etc.
 
Waweza kumuita hivyo ukipenda, lakini ugumu huu wa maisha alioupata kama yatima (kulingana na maelezo) angeweza kutafuta riziki kwa kuwa jambazi na siku moja akasimamisha gari la mumeo au baba yako na katika purukushani za kumpora akauwawa. Sidhani kama ungemuita mpuuzi kwa dharau hivyo badala ya majina mengine. Tumesema Ukosefu wa ajira ni bomu linalo subiri kulipuka tuu
Nyie ndiyo mnajidanganya na kwadanganya wengine. Ni yeye pekee hana ajira? Na hao malaki kwa malaki walioishia darasa la saba mbona hatuoni wakijiua kwa sababu hawana ajira? Mkiamuwa kupeleka lawama kwa rais kwa kila linalotokea mtashia kukosa hata viraka vya kushonea nguo zenu!
 
Hivi mkuu unaishi Tanzania gani hio ambayo eti unaenda wizarani tu unawaambia nipeni kazi mshahara laki tatu??


Kuingia tu geti la wizara hayo maswali utakayopigwa hapo mlangoni na walinzi hautarudi Tena aisee.
Nadhani haujawahi kwenda wizara yoyote hapa nchini.
Teh teh teh teh!
 
This wat we call due point. Ila computer science PC uliyotoka nayo chuo ni mtaji tosha kitaa, unadesign business cards unatawanya stationeries zote mjin kwamba we ni kishoka. Utapigiwa Simu tu japo sio kila siku and utasurvive .yote tisa mambo ya jiwe haya "the future is not clear"


sio rahisi km unavyofikiria ww eti kusambaza kadi stationery...walosoma computer sc..wanatakiwa mtaji mzuri tu...
 
Mie nashangaaga hata kama hawana watu waku wa advice vizuri huko serikalini,kwa nini wasitumie JF ushauri unaotolewa humu?...Napata picha kila mtu anawaza tumbo lake huko…...haya unayoyaandika trust me wanayajua sana...kuyatekeleza ndio ishu,..sijui nani afanye nini..
My dear sister they dont have time to came hee and read, and learn a thing or 2,but remeber this ccm regime said it dont need anyones advice, and you know very well only FOOLS think they dont need advice,but trust me many in tz go to uni expecting to be hired, and as you know companies are even running away from tz coz of harsh investment climate, so when she, he lacks employement, the results is as you see here,tz needs to re think its education strategy, otherwise we will continue producing people with degrees on papers only and in their heads, happy weekend pls
 
sio rahisi km unavyofikiria ww eti kusambaza kadi stationery...walosoma computer sc..wanatakiwa mtaji mzuri tu...
Mtaji ndo haupo sasa! Inabidi mtu aanze from the scratch. Sema kitu ambacho kinahitaji ujitoe ufaham kidogo kwakuwa changamoto ni nyingi sana. Mpaka mtu anajiua ujue ashafanya a lot of trials akaona enough is enough we never know mkuu nin hasa kilimsibu
 
Mtaji ndo haupo sasa! Inabidi mtu aanze from the scratch. Sema kitu ambacho kinahitaji ujitoe ufaham kidogo kwakuwa changamoto ni nyingi sana. Mpaka mtu anajiua ujue ashafanya a lot of trials akaona enough is enough we never know mkuu nin hasa kilimsibu

Nakuelewa sana mkuu..mie namuelewa sana
 
Hana kazi pesa ya kununulia pombe alikuwa anapata wapi?

Kwann alishindwa kuwashawishi wanaomnunulia pombe wampatie mtaji?

Hawa ndio wapumbavu wanaoshindwa kujiongeza kwa kudhani jina la chuo alichosoma litamsaidia.

Darasa la saba wanatoboa kwa kuchakarika msomi unasubiria ajira ya ofisini kwa kupiga viroba na ugoro kama sio upumbu ninini?
 
Pumzika kwa Amani, ndugu Ali

Ni tukio la kusikitisha sana, kwani kijana huyu alikuwa ni mwenye umri wa kuchapa kazi na ni nguvu kazi ya taifa pia. Na ifahamike kuwa, sisi vijana ni nguvu kazi ya taifa kwa jumla.

Tukumbushane sisi kwa sisi, kuwa elimu za taaluma hazina ulazima sana wa kutupatia ajira za serikalini ama kwenye makampuni binafsi. Ijapokuwa ni wazi kwamba kila mtu angependa iwe hivyo na hasahasa kwa upande wake binafsi.

Lakini kwa kusema ile ukweli wa dhati kabisa ni suala gumu kutekelezeka kwa kila mtu kwa maana ya wahitimu wote kuweza kuajiriwa ama serikali ama kwenye makampuni binafsi.

Tukumbushane kuwa, tupo kwenye karne yenye kauli mbiu kuhusu elimu isemayo: Elimu haina mwisho; ikiwa na maana kuwa tusichoke kujifunza mambo mapya nje ya tuliyojifunza kwanye mavyuo huko ama kolejini, kwa ajili ya kuweza kupata uwezo wa kutumia fursa nyingi zaidi.

Na ningependa kwa binafsi yangu, ile kauli mbiu kuhusu elimu, isemayo: Elimu ni ufunguo wa maisha, kwa kweli kauli mbiu hiyo imekwishapitwa na wakati. Maana inajenga fikra ya maisha ya mtelezo kwa wanafunzi wengi pindi wawapo mashuleni. Tofauti na uhalisia ulivyo baada ya kuhitimu.

Tumtakie kila lenye kheri huko aendako, ndugu yetu Ali. Na kwamba tukio hili la mwenzetu huyu aliwezi kuwa ni la kujivuna nalo katika kutetea hoja za ukosefu wa ajira, na kuendelea kusubiri ajira: Na hasahasa kwa vijana wahitimu wa elimu ya vyuo.
 
Huwa unajisifu kwa akili ambazo huna lakini kuwa na staha ya kawaida tu.. Likes zinaishia jf ila ulichokifanya wala hakitobagua kuwa ID ni fake au real.. Mungu akusamehe lakini

Usinipangie nini cha Kuandika au Kuchangia hapa Jamvini sawa? Bloody Swine!
 
Back
Top Bottom