Miaka 10 Kawe Barabara ni mitaro ya maji, Gwajima okoa jahazi

Miaka 10 Kawe Barabara ni mitaro ya maji, Gwajima okoa jahazi

Hujui kuwa pesa za walipakodi wa Tanzania ikiwemo wana Kawe kwa uwingi (maana kwa Dar es Salaam , matajiri wengi wanakaa jimbo la kawe) ndo zimeenda kujenga uwanja wa ndege wa Chato tena hata bila kufuata taratibu????
Achana na siasa uchwara.
Tunataka Gwajima atakayeleta barabara Kawe.
Kazi hiyo Halima kashindwa vibaya.
Full stop.
 
Kwa miaka 10 aliyokaa Halima Mdee kuwakilisha jimbo la Kawe, maendeleo ya miundombinu ya kijamii ni kama hakuna.
Barabara chache sana za kuunganisha maeneo zimejengwa.

Nimeishi jimbo ka Kawezaidi ya miaka 20 baada ya kuhamia huku toka Temeke, hali ya Kawe inatisha.
Tunahisi Mdee aidha hawezi kazi yake kushawishi serikali kuleta hayo maendeleo muhimu ya miundombinu ya barabara, au tu kwamba hafai.

Kwa muda wote huo sijamwona huku mitaani akipita kusikiliza kero kubwa za wananchi hususan barabara.

Huwa narudi Temeke, Tandika na Kijichi na huwezi kuamini.
Barabara mpya maeneo hayo ni zaidi ya kilometa 100, na zinapita hadi uchochotoni.

Tatizo lipo kwa muwakilishi wetu, Halima Mdee.
Tusichague vyama tuchaguemtu awezaye kuleta maendeleo ya barabara.
Watu wasichague kwa mazoea, chagua Gwajima tupate mabadiliko na maendeleo.
Hata waliomchagua Trump si kwamba wanampenda, wamemchagua kwa maslahi ya maendeleo yao.

Wana Kawe tuwe strategic, chagua Gwajima.
Hivi mwenye wajibu wa kujenga barabara na miundombinu mingine ni mbunge ama serikali! Hivi wana Kawe tunaadhibiwa na kucheleweshewa maendeleo kwa kosa la kumchagua kiongozi wao kwa njia ya kidemokrasia?

Basi sasa na tuone, kwa kuwa viongozi wote wa mitaa na vitongoji waliotokana na uhuni uliotokana na uchafuzi wa 2019 na kupelekea wote watoke CCM, na tuyaone hayo maendeleo na wala visitafutwe visingizio vingine kupitia nafasi ubunge. Nafasi hii ya ubunge CCM tupa kule, bado tuna imani na mbunge aliyemaliza muda wake.
 
Hizo barabara mbovu Gwajima hakuziona kabla? Kwani kuzitengeneza lazima awe Mbunge? Atapata wapi pesa ya kutengenezea?
 
Kwa miaka 10 aliyokaa Halima Mdee kuwakilisha jimbo la Kawe, maendeleo ya miundombinu ya kijamii ni kama hakuna.
Barabara chache sana za kuunganisha maeneo zimejengwa.

Nimeishi jimbo ka Kawezaidi ya miaka 20 baada ya kuhamia huku toka Temeke, hali ya Kawe inatisha.
Tunahisi Mdee aidha hawezi kazi yake kushawishi serikali kuleta hayo maendeleo muhimu ya miundombinu ya barabara, au tu kwamba hafai.

Kwa muda wote huo sijamwona huku mitaani akipita kusikiliza kero kubwa za wananchi hususan barabara.

Huwa narudi Temeke, Tandika na Kijichi na huwezi kuamini.
Barabara mpya maeneo hayo ni zaidi ya kilometa 100, na zinapita hadi uchochotoni.

Tatizo lipo kwa muwakilishi wetu, Halima Mdee.
Tusichague vyama tuchaguemtu awezaye kuleta maendeleo ya barabara.
Watu wasichague kwa mazoea, chagua Gwajima tupate mabadiliko na maendeleo.
Hata waliomchagua Trump si kwamba wanampenda, wamemchagua kwa maslahi ya maendeleo yao.

Wana Kawe tuwe strategic, chagua Gwajima.

Kwani anayejenga mitaro na barabaraa ni halima mdee au serikali...muache ujinga...naona kama jamii forums imevamiwa na vibaka wa ccm...kwanza.amepambana sana kwenye ardhi kwanza wako mpaka huyu mwabepande.....
..
 
Kwanza huyu Gwajima amejenga Kanisa lake au ofisi yake ya kila siki? unategemea mtu kama huyo akujengee wewe chuo Cha uvuvi...huyu ni utindiga kabisa....karibu tutalete Mkonda wa porn wa phase 2gwajima the pornstar humus humu
 
Watu hamko serious, yaani mzinzi gwajima aokoe jahazi kawe? Yeye anachojua in kununua kadi za wapiga kura basi.
 
Kawaambie hivyowana Kawe, Halima ameshindwa kuiamsha Serikali jimboni Kawe.Gwajima nina uhakika ataiamsha Serikali.


Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

MHE. HALIMA J. MDEE:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru.

Kwanza nimshauri tu Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, usiige utamaduni wa mtangulizi wako wa kutuletea vitabu vikubwa ambavyo mtu akisoma between the lines kuna maneno mengi kuliko uhalisia. Ushauri wangu kwako tu, inawezekana huu ni mwaka wa kwanza bado una mihemko ya aliyekutangulia, kuanzia mwaka ujao uje na kitabu ambacho kinaeleza tumepanga nini na tutatekeleza nini kwa huo mwaka, hilo ni la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili watu ambao mnaongea sana, sijui Mheshimiwa Magufuli alivyokuwa Waziri kafanya nini, mwaka jana mwenyewe amekiri hapa, katika miaka kumi ya Ilani ya CCM, 2005 – 2015 ameweza kutekeleza asilimia 31 ya kile mlichotakiwa mkifanye. Sasa hivi nyie mtoto akifanya mtihani akipata 31 chini ya 100, hivi huyo amefeli amefaulu? Kwa hiyo, tuache kujikomba, unafiki, tusaidie Serikali ndilo jukumu letu kama Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nina barabara zangu Jimboni, najua kuna wengine huko wanapata shida na barabara zao zimechokachoka, sisi wa town tuna nafuu kidogo. Lakini nimeahidiwa hapa, miaka mitatu iliyopita na Mheshimiwa Waziri, naomba utoe majibu. Kuna barabara za kupunguza foleni mkoa wa Dar es Salaam; barabara ambazo zinaunganisha Jimbo la Kibamba na Jimbo la Kawe; barabara ya Goba – Tanki Bovu; Goba – Wazo Hill –Tegeta, Gao – Goba – Makongo – Mlimani City.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mkiwa mnanijibu hapa, msiniambie ujenzi umeanza, ninajua hizi ni barabara tatu tofauti zinazounganishwa na kipande kimoja. Sasa nataka leo msiniambie kwa sababu ukiangalia vitabu vya bajeti, na ndio maana nawaambia Waheshimiwa Wabunge,tuwe tunasoma, tukiwa hatusomi Mawaziri hawa wanakuja wanatudanganya. Miaka mitatu mfululizo hizi barabara zimetengewa fedha, kipande cha kuunganisha Jimbo la Kibamba na Kawe, Goba – Mbezi, Goba – Wazo Hill, Goba – Mlimani City, lakini leo ni mwaka wa tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaona kuna hela zimetengwa hapa, zipo, kama ambavyo mwaka wa jana Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa maneno haya haya kama ya kwako zilikuwepo lakini mwaka mmoja baadaye hakuna barabara. Sasa Waziri kesho ukiwa unajibu naomba uniambie kwa uhakika wananchi wa Kawe wasikie, kwa sababu wewe ni mwananchi wangu pia na Mbunge wako nikiwa nazungumza lazima usikilize hizi barabara zinakamilika lini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa juzi, wakati wanajenga hii barabara ya Mwenge – Tegeta – Kibaoni niliishauri Serikali nikaiambia wakati wa mvua kuna kiwango kikubwa cha maji kinachotoka ukanda wa Wazo huku juu Goba na ili barabara iweze kudumu kuna maeneo ambayo lazima mapokeo na matoleo ya maji yawe makubwa Ili tuweze kuelekeza maji baharini. Leo barabara imejengwa, mvua ikinyesha ukiwa pale Afrikana, Goigi ni majanga, hii barabara itakatika miaka mitano haitimii, kuna faida gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi namuomba Mheshimiwa waziri akiwa anajibu, kwa sababu niliandika barua kama Mbunge nikiwaomba; mkasema ooh! huyu mjapani ambaye tumepewa msaada ana masharti tutatumia fedha za ndani kujenga mapokeo ya maji makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo naomba niambiwe maana mvua ikinyesha yakitokea maafa Mheshimiwa Jenista Mhagama huyo, halafu mvua ikikauka na yeye anasepa, barabara iko vilevile. Sasa leo nataka mniambie mna mikakati gani, dhahiri, shahiri, kuweza kuokoa ile barabara ya mabilioni ya shilingi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Rais ambaye watu tunaambiwa tusimtajetaje, tutamtaja tu kama alichemsha, msitutishe. Wakati tunapitisha bajeti ya barabara ya Mwenge – Tegeta ya shilingi bilioni 88 tuliambiwa hii barabara itajengwa vipande viwili, kwa matukio mawili. Moja ni Mwenge kwenda Tegeta ya pili ni Mwenge kwenda Morocco, bilioni 88. Sasa leo kuna uchafu unaendelea pale, kutoka Mwenge kwenda Morocco sijui mnatengeneza kichochoro, sijui mnatengeneza kitu gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninataka nijui zile shilingi bilioni 88 ambazo Mheshimiwa John Pombe Magufuli, katika Bunge hili akiwa Waziri alisema kazi yake ni kujenga hizi barabara mbili, ziko wapi? Nataka majibu. Na ule uchafu mnaojisifia sijui fedha za Uhuru, sijui fedha za nini, ile barabara ilikuwa na pesa; kwa hiyo msitafute ujiko kwa kuwa mmezitafuna zile pesa mnatuletea uchafu. Si hadhi ya Dar es Salaam kujengwa ibarabara zile na kama mnatuambia mnajenga kwa muda, hilo pia ni tatizo linguine, misuse of resources. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafuriko. TANROADS walifanya upembuzi yakinifu sijui mnavyoita ninyi, wakatengeneza na michoro kwa ajili ya mfereji mkubwa kuzuia mafuriko ukanda wa Kunduchi, miaka minne imepita. Mwaka juzi alienda Mheshimiwa Pinda, akaambiwa mchoro huo upo, wakati wananchi wanaelea kwenye bahari ya mafuriko, mkasema itajengwa, itatengewa fedha, hakuna kilichofanyika, naomba nipate majibu kesho.
 
Sasa kama kila kitu anapinga mtapataje maendeleo..ye dereva kakanyaga breki mnategemea kufika?
 
Nikiwaweka kwenye mizani ya ushawishi Gwajima anaweza kushawishi serikali na wadau wengine kutatua changamoto za Kawe.
Sidhani Kama Mdee anaushawishi, zaidi anakera anaopaswa kiwashawishi.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Kwa miaka 10 aliyokaa Halima Mdee kuwakilisha jimbo la Kawe, maendeleo ya miundombinu ya kijamii ni kama hakuna.
Barabara chache sana za kuunganisha maeneo zimejengwa.

Nimeishi jimbo ka Kawezaidi ya miaka 20 baada ya kuhamia huku toka Temeke, hali ya Kawe inatisha.
Tunahisi Mdee aidha hawezi kazi yake kushawishi serikali kuleta hayo maendeleo muhimu ya miundombinu ya barabara, au tu kwamba hafai.

Kwa muda wote huo sijamwona huku mitaani akipita kusikiliza kero kubwa za wananchi hususan barabara.

Huwa narudi Temeke, Tandika na Kijichi na huwezi kuamini.
Barabara mpya maeneo hayo ni zaidi ya kilometa 100, na zinapita hadi uchochotoni.

Tatizo lipo kwa muwakilishi wetu, Halima Mdee.
Tusichague vyama tuchaguemtu awezaye kuleta maendeleo ya barabara.
Watu wasichague kwa mazoea, chagua Gwajima tupate mabadiliko na maendeleo.
Hata waliomchagua Trump si kwamba wanampenda, wamemchagua kwa maslahi ya maendeleo yao.

Wana Kawe tuwe strategic, chagua Gwajima.
Kabla ya kuingia halima mdee kawe mbunge wa kawe alikuwa anatoka chama gan??? Hivi wapinzani wakiingia kwenye majimbo ndiyo maendeleo yanaondoka?? Kwa ufupi huo ni ufinyu wa kufikiri kabisa kwa kudhan mbunge kupitia ccm akiingia jimboni ndo utapata maendeleo. Kazi yetu ni kusikiliza sera na kuchagua mtu sahihi kabisa kwa mustakabali wa wapiga kura. Lakin kwa kawe kumchagua huyu mcheza ngoma ni kujidanganya kabisa. Hili nalisema leo lakin kumbukeni mtakuja humu humu tena kulalamika
 
Hujui kuwa pesa za walipakodi wa Tanzania ikiwemo wana Kawe kwa uwingi (maana kwa Dar es Salaam , matajiri wengi wanakaa jimbo la kawe) ndo zimeenda kujenga uwanja wa ndege wa Chato tena hata bila kufuata taratibu????
na kibaya zaidi yote hayo ya chato hayakuwa kwenye budget
sikuwahi kusikia budget za kuanzisha miradi hiyo ikijadiliwa bungeni alafu leo mnakaa na fikra zenu finyu mnaanza kumuongelea vibaya halima
 
Back
Top Bottom