Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

DP World wako vizuri wale jamaa wanaweza hata kupanua hiyo Port wana uzoefu wa hali ya juu.

Maza alienda Dubai sijui waliongea nini?

Kila International company inayokuja Tanzania inakuwa vizuri na inakuja na standard zake, hata hawa Barrick, TICS ya wale wahongkong nk.

Shida inaanzia kwa watu wetu wanapolazimisha 10% zao na interest zao ambazo ukipiga calculation za kibiashara unakuta sio viable, matokeo yake ni either kugeuka kuwa shetani ufanane nao au uachane na hiyo biashara.

Kumbuka kila mfanyabiashara ni mafia na focusing after super profit, sasa anapoona loop holes za yeye kupata superprofit kwa kuwapa tu wajinga 10% lazima afanye namna ili apige hela.

Mtanzania yuko tayari hata kuwafanya Watanzania wenzie maelfu watumwa ili yeye tu apate hela aishi vizuri huku maelfu wakiteseka, ndio basi yuko tayari hata kupokea rushwa ya 500K ili atoe documents muhimu inayoweza hata kufilisi nchi.

Kila biashara kubwa au project kubwa kubwa Tanzania na Africa lazima kuna mikono ya weusi hata ikiwezekana hiyo project ifail ili wao wapate hela.

Biashara ya Bandari pekee kama inaweza kusimamiwa vizuri inaweza kabisa kuleta big impact kwenye uchumi wa Tanzania na watanzania.
 
Ahsante mkuu 'imhotep', kwa hizo taarifa ulizoniwekea kama ushahidi wa umahiri wa kampuni hiyo, ambao hata TICTS ukitafuta habari zao na wao watakuwa na wasifu wa namna hiyo.
Hivi unajua TCTS ni kitawi cha kampuni gani duniani?
 
Na ndiyo sababu kuna umuhimu wa kuwaiga wachina katika kupambana na hawa wapumbavu wachache wanaotuuza utumwani tena.
Hawa siyo watu wa kuwaonea huruma shaba zikiwaingia mwilini mwao.
 
Ahsante mkuu 'imhotep', kwa hizo taarifa ulizoniwekea kama ushahidi wa umahiri wa kampuni hiyo, ambao hata TICTS ukitafuta habari zao na wao watakuwa na wasifu wa namna hiyo.
Hivi unajua TCTS ni kitawi cha kampuni gani duniani?
Hawa wanahudumia Bandari nyingi Duniani kote sio njaa njaa kama TCTS
 
Lakini kuna jambo mhuhimu ninaloomba waTanzania tukumbushane kwa kwa kuutumia huu mfano wa mkataba na TICTS.
Kampuni hiyo imekuwepo hapa kwa miaka 20 na kwa muda wote huo sisi waTanzania hatukuweza kujifunza lolote kutoka kwao, kwamba tutajijiengea uwezo wa kuiendesha hiyo sehemu ya bandari baada ya hawa wageni kuondoka.

Hapana, sijasema serikali iingie kwenye huo uendeshaji, (najua kuna watu husema serikali haiwezi chochote), lakini je, hata kuwaandaa na kuwapa uwezo waTanzania nje ya serikali haiwezekani?

Kuna utaalam gani wa zaidi sana ambao watu wetu hawawezi kamwe kuumudu kuendesha shughuli kama hiyo?

Ninaelewa ni kiasi gani tunavyojidharau, kwamba hatuwezi chochote, jambo ambalo sikubaliani nalo kabisa. Kinachotushinda ni viongozi wetu kutosimamia vizuri shughuli zetu na kuwatia moyo wananchi wake ili waweze kuleta mageuzi makubwa katika nchi yao.
Hatuna viongozi wanaoamini kwamba tunaweza, matatizo yetu yanaanzia hapo.

Mkuu shida ipo kwa walamba asali
 
Ninakuomba uelewe kwamba TICTS ni kitawi tu kilichopo hapa Tanzania ambacho ni sehemu ya kampuni kubwa duniani.

Hata hao Dubai wakija hapa, wanaweza kuunda tu kitawi chao hapa kwetu kuendesha shughuli zao.
Tufanye mabadiliko labda DpWord watakuja na ufanisi zaidi.
 
Kwa jinsi CCM ya zamani inavyorudi na Karamagi mwenyewe kaukwaa uenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, yawezekana imeondoka TICTS lakini amebaki Karamagi.
Jinsi walivyovungavunga mambo tokea mkataba uishe na kuendeleza majadiliano, inanibidi nikubaliane na wewe, kwamba kuna jambo linasukwa, na litakapokuwa tayari tutaelezwa.
Hawa watu sasa hivi hawana woga wowote tena wa kufanya chochote wanachotaka.
 
Lakini kuna jambo mhuhimu ninaloomba waTanzania tukumbushane kwa kwa kuutumia huu mfano wa mkataba na TICTS.
Kampuni hiyo imekuwepo hapa kwa miaka 20 na kwa muda wote huo sisi waTanzania hatukuweza kujifunza lolote kutoka kwao, kwamba tutajijiengea uwezo wa kuiendesha hiyo sehemu ya bandari baada ya hawa wageni kuondoka.

Hapana, sijasema serikali iingie kwenye huo uendeshaji, (najua kuna watu husema serikali haiwezi chochote), lakini je, hata kuwaandaa na kuwapa uwezo waTanzania nje ya serikali haiwezekani?

Kuna utaalam gani wa zaidi sana ambao watu wetu hawawezi kamwe kuumudu kuendesha shughuli kama hiyo?

Ninaelewa ni kiasi gani tunavyojidharau, kwamba hatuwezi chochote, jambo ambalo sikubaliani nalo kabisa. Kinachotushinda ni viongozi wetu kutosimamia vizuri shughuli zetu na kuwatia moyo wananchi wake ili waweze kuleta mageuzi makubwa katika nchi yao.
Hatuna viongozi wanaoamini kwamba tunaweza, matatizo yetu yanaanzia hapo.
Utaalamu wetu tutakaouweza zaidi tukipewa hiyo bandari ni nyodo na kuibia watu vitu vyao kwa sana.
 
TPA waendeshe wenyewe
Hata mimi nakubaliana na wewe TPA waendeshe wenyewe,maana kuruhusu watu binafsi hawafai kabisa japo mzee wa Lupaso alitamani kila kitu ni kubinafsisha kulikuwa na NASCO,TACOSHILI na mengine mengi
 
Tufanye mabadiliko labda DpWord watakuja na ufanisi zaidi.

Sawa, mkuu 'imhotep', ninajua huko ndiko tunakoelekea; lakini kuhusu "ufanisi zaidi"; kwa maslahi ya nani?

Hao watakaa hapa miaka yao mingine 20 au zaidi, na bado Tanzania itakuwa haina uwezo wowote wa kuendesha bandari zake.
Huoni hayo kuwa maajabu makubwa sana?
 
Kuondoa ubabaishaji mmoja na kuweka ubabaishaji mwingine ndiyo zetu wabongo. Hata aje nani kama sisi wenyewe hatubadilika kutoka kwenye ubabaishaji basi hakuna chochote cha maana. Hakuna hata kitu kimoja tunafanya kwa ufanisi!
Hawa wanahudumia Bandari nyingi Duniani kote sio njaa njaa kama TCTS
 
Kuondoa ubabaishaji mmoja na kuweka ubabaishaji mwingine ndiyo zetu wabongo. Hata aje nani kama sisi wenyewe hatubadilika kutoka kwenye ubabaishaji basi hakuna chochote cha maana. Hakuna hata kitu kimoja tunafanya kwa ufanisi!
Usinung'unike sana kuwa na subra.
 
Utaalamu wetu tutakaouweza zaidi tukipewa hiyo bandari ni nyodo na kuibia watu vitu vyao kwa sana.
Lakini kweli ni lazima iwe hivi, mkuu wangu 'Algore'?
Hatuwezi kamwe nasi tukafanya jambo jema kwetu sisi wenyewe, kwa sababu zipi hasa?
 
Back
Top Bottom