Lakini kuna jambo mhuhimu ninaloomba waTanzania tukumbushane kwa kwa kuutumia huu mfano wa mkataba na TICTS.
Kampuni hiyo imekuwepo hapa kwa miaka 20 na kwa muda wote huo sisi waTanzania hatukuweza kujifunza lolote kutoka kwao, kwamba tutajijiengea uwezo wa kuiendesha hiyo sehemu ya bandari baada ya hawa wageni kuondoka.
Hapana, sijasema serikali iingie kwenye huo uendeshaji, (najua kuna watu husema serikali haiwezi chochote), lakini je, hata kuwaandaa na kuwapa uwezo waTanzania nje ya serikali haiwezekani?
Kuna utaalam gani wa zaidi sana ambao watu wetu hawawezi kamwe kuumudu kuendesha shughuli kama hiyo?
Ninaelewa ni kiasi gani tunavyojidharau, kwamba hatuwezi chochote, jambo ambalo sikubaliani nalo kabisa. Kinachotushinda ni viongozi wetu kutosimamia vizuri shughuli zetu na kuwatia moyo wananchi wake ili waweze kuleta mageuzi makubwa katika nchi yao.
Hatuna viongozi wanaoamini kwamba tunaweza, matatizo yetu yanaanzia hapo.