Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa makahaba wastaafu

Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa makahaba wastaafu

Bado haujaelewa, jambo lolote ambalo linamnufaisha mtu kwa namna moja ama nyingine, huyo mtu hawezi kuliona hilo jambo kama tatizo.

Unachokitaka wewe hakiwezekani, hiyo ni ndoto, yani mwanamke ambaye analipiwa kodi ya nyumba ,analishwa na kuvishwa unataka aone kufanyiwa hivyo vitendo ni tatizo? How?

Kama wanaume hatuwezi kuwa wamoja kwenye hili, hakuna mantiki ya kuwalaumu hao wanawake kile wakifanyacho ikiwa sisi wenyewe ndiyo tuna support hayo wanayo yafanya.
Wewe ndio hauelewi halafu hautaki kukubali kwamba hauelewi. Hakuna ambapo kalaumiwa mwanamke. Hata heading tu inajieleza. "Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa malaya wastaafu". Hivi hapo huo ujumbe umemlenga mwanaume au mwanamke. Kimsingi kinachoandikwa kinamlenga mwanaume, mwanamke anaguswa tu kama mmoja ya wahusika kwenye movie.. Mfano nikisema "vijana zingatieni bikira mnapooa". Ujumbe unawahusu vijana wa kiume sio wanawake ambao hawana bikira.
 
Bado kuna kitu kidogo sana haukielewi au unakielewa lakini unajizima data.

Hiyo relationship monetization inafanikiwa kwa sababu ya wanawake wanaotaka kuuza, au kwa sababu ya wanaume wanaotaka kununua?

Kwanini unatumia nguvu kubwa sana kuwashutumu wanawake badala ya kuwasema wanaume ambao ndiyo wenye capital ya kuendesha hiyo biashara?
Tunarudi kule kule kwenye kutaka ku-dictate mimi niende na mpangilio au mtililiko upi. Mambo ni mengi na mimi siwezi kucover kila angle. Kama mimi nimeona shida ni wanawake kujirahisha. Andika wewe thread useme shida ni wanaume kuonga. Sio lazima kila angle iguswe na natafuta ajira
 
Wewe ndio hauelewi halafu hautaki kukubali kwamba hauelewi. Hakuna ambapo kalaumiwa mwanamke. Hata heading tu inajieleza. "Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa malaya wastaafu". Hivi hapo huo ujumbe umemlenga mwanaume au mwanamke. Kimsingi kinachoandikwa kinamlenga mwanaume, mwanamke anaguswa tu kama mmoja ya wahusika kwenye movie.. Mfano nikisema "vijana zingatieni bikira mnapooa". Ujumbe unawahusu vijana wa kiume sio wanawake ambao hawana bikira.
Kama lengo lako ni kuwashauri wanaume, kwa nini unatumia lugha ya kudhalilisha badala ya kujenga?

Unafikiri kwa kutumia lugha ya dharau ndiyo njia pekee ya kuwafanya wanaume wakusikilize?
 
Tunarudi kule kule kwenye kutaka ku-dictate mimi niende na mpangilio au mtililiko upi. Mambo ni mengi na mimi siwezi kucover kila angle. Kama mimi nimeona shida ni wanawake kujirahisha. Andika wewe thread useme shida ni wanaume kuonga. Sio lazima kila angle iguswe na natafuta ajira
Huwa unaandika uzi ili kila atakayesoma akubaliane na wewe moja kwa moja kile unachokiwasilisha?
 
Nice men will get used. Ruthless men get respected
It takes zero effort to be ruthless, anyone can be mean.

It takes real strength and confidence to be kind in a world that often rewards selfishness, if you think kindness is a weakness, it's likely because you haven't mastered the art of being kind while still having strong boundaries.
 
Namaanisha kwenye miingiliano yangu na watu(mke akiwepo) huwa na-assume kuna siku anaweza kuzingua. Kwahiyo huwa siweki matarajio makubwa kwenye hisia za mtu. Katika maisha yangu nimejenga mfumo wa kwamba mimi mwenye ndio ninakua center ya maisha yangu. Kwahiyo mtu yoyote(mwanamke, rafiki, ndugu n.k) akija kwenye maisha yangu na kuondoka hakuna nguzo ambayo itaanguka
Umekuja sehemu niliyotaka ufike ili tuelewane kuhusu exception rule unayopendekeza isitumike maishani.

Tofauti ya mwanamke uliye naye na mwanamke mwingine ni ipi kama wote watakuacha wakifatwa na mwenye pesa?
 
Kama lengo lako ni kuwashauri wanaume, kwa nini unatumia lugha ya kudhalilisha badala ya kujenga?

Unafikiri kwa kutumia lugha ya dharau ndiyo njia pekee ya kuwafanya wanaume wakusikilize?
Wanaume tuna namna yetu ya kupeana mizuka kwenye maongezi. Kama unataka kupewa ushauri kwa lugha tamu tamu fanya maongezi na bi mkubwa au kiongozi wako wa dini. Lakini men to men lugha za bullying utakutana nazo sana tu.
 
Huwa unaandika uzi ili kila atakayesoma akubaliane na wewe moja kwa moja kile unachokiwasilisha?
Sikatai kupingwa lakini ninachostaajabu ni wewe kutaka niandikeje. Nimeongelea scenerio mbili nilizokutana nazo. Ilitosha tu kusema tatizo ni ubovu wa malezi, kushuka maadili n.k au kupinga tu kwa kusema wadada hawana hizo tabia.

Lakini kutaka mimi niipanue mada kuwaongelea na hao wanaoonga hapo ndipo unataka mimi niandike vile unataka wewe. Ndio maana nikakuambia kama mimi sijaigusa hiyo angle unayotaka twende basi iandikie thread wewe.
 
Wanaume tuna namna yetu ya kupeana mizuka kwenye maongezi. Kama unataka kupewa ushauri kwa lugha tamu tamu fanya maongezi na bi mkubwa au kiongozi wako wa dini. Lakini men to men lugha za bullying utakutana nazo sana tu.
Kwamba huu uzi umesomwa na utasomwa na wanaume tu?

Umepost hapa jukwaani ukiwa unajua fika kuwa si wanaume tu watakaosoma hata wanawake, mabinti zetu, na jamii nzima itasoma but still ukatumia lugha ya kudhalilisha.

Kama hoja yako inahitaji lugha za bullying ili ieleweke, maana yake huna hoja za msingi za kuwashawishi watu wenye akili timamu, unategemea nguvu ya matusi na dharau tu.
 
Sikatai kupingwa lakini ninachostaajabu ni wewe kutaka niandikeje. Nimeongelea scenerio mbili nilizokutana nazo. Ilitosha tu kusema tatizo ni ubovu wa malezi, kushuka maadili n.k au kupinga tu kwa kusema wadada hawana hizo tabia.

Lakini kutaka mimi niipanue mada kuwaongelea na hao wanaoonga hapo ndipo unataka mimi niandike vile unataka wewe. Ndio maana nikakuambia kama mimi sijaigusa hiyo angle unayotaka twende basi iandikie thread wewe.
Lilikuwa suala la kuzikubali tu hizo hoja , nimekupinga kwa sababu tatizo la watu wachache wewe unataka kulihalalisha lionekane ni la jinsia nzima, ndiyo maana nikakomaa na hiyo hoja ya kuwaongelea wanaume kama ndiyo mzizi wa tatizo kuzidi kukua.
 
Umekuja sehemu niliyotaka ufike ili tuelewane kuhusu exception rule unayopendekeza isitumike maishani.

Tofauti ya mwanamke uliye naye na mwanamke mwingine ni ipi kama wote watakuacha wakifatwa na mwenye pesa?
Mustakabali wa mahusiano ni fumbo lakini huo sio uhalali wa mimi kufanya gamble kwa mwanamke ambae tayari nishaziona red flags. Siwezi nikapuuzia redflags kwa kigezo cha exception. It's ok the future is not ours to see, but when it come to vetting i will jugde women harshly and ruthlessly based on their past
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wambie wanaume wenzio
wasioe kabisa
Ili kukata mzizi wa ftina

Hua mnakuja na nyuzi hizi kama darasa ila kwa upande mwingine mnapenda mnoo kudhalilisha wanawake

Hampendi kutumia ule msemo Baadhi ila wanawake wote ni malaya hakuna msafi aisee🙌🙌🙌🙌🙌

Kwenye jamii yoyote ile iwe zamani au sasa umalaya ukahaba ulikuepo

Na umalaya ni wapande mbili wanaume kwa wanawake
Kama baadhi ya wanaume wasingekua malaya umalaya usingekuepo na pia kama baadhi ya wanawake kua malaya ukahaba ungewezekana vipi?

Hii ni tabia chafu mbovu inategemea pande zote za shilingi ajabu mnachagua upande mmoja na kuubebesha mzigo wa lawama

Nb: Siungi mkono hizo tabia za ukahaba
Wewe mtoto akili yako inakuwa kwa kasi sanaa tugemee mrithi wa Jadda so soon..
Hii nni dhana nzuri kupinga hoja ila bado mzani unaegemea kwenu tuu.. Ngoja nikitulia nisome bandiko
 
Kwamba huu uzi umesomwa na utasomwa na wanaume tu?

Umepost hapa jukwaani ukiwa unajua fika kuwa si wanaume tu watakaosoma hata wanawake, mabinti zetu, na jamii nzima itasoma but still ukatumia lugha ya kudhalilisha.

Kama hoja yako inahitaji lugha za bullying ili ieleweke, maana yake huna hoja za msingi za kuwashawishi watu wenye akili timamu, unategemea nguvu ya matusi na dharau tu.
Nikisema walengwa ni wanaume haimaanishi kwamba thread itasomwa na wanaume tu. Hao wanawake wanaweza kusoma lakini ujumbe hahwahusu wao directly. Kuhusu matusi unaweza ukaonyesha wapi limeandikwa tusi kwenye heading au thread
 
Back
Top Bottom