Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Tulipokuwa tunasema Magu ni genius na mzalendo watu walikuwa hawaelewi. Wakaruhusu kudanganywa na propaganda za upinzani na wanaharakati wanaotekeleza ajenda za wazungu.

Sasa wengine ndiyo wataelewa!
 
Kuna mkulima anayeenda kuuza mazao huko nje,
Bei ya shambani bado iko chini Ila inapandishwa na wafanyabiashara
Bei ndiyo inavyopanda. Wakulima waliohifadhi watauza bei nzuri. Mwakani watu watavutiwa kulima na wakulima watataka bei nzuri kama ya mwaka huu. Ili kumfaidisha mkulima linatakiwa kuwa suala endelevu. Ile mwaka huu unafungua mpaka, mwakani unafunga ndiyo iliyokuwa inamnyonya mkulima.
 
Asante msemaji wa mama Samia.
 
Mpumbavu mkubwa wewe, wakulima wetu ndiyo wakati wao wa kupata fedha na kuboresha maisha yao. Wewe badalanya kwenda kulima mahindi unakuja kuandika pumba JF.

Nenda na wewe ukalime halafu uone uchungu wa kuambiwa usiuze mahindi nje ya nchi.
Boya kabisa, wakulima gani wanapata pesa.......pesa mnapata nyinyi matapeli mnaojiita wafanyabiashara baada ya kuwaibia wakulima kupitia lumbesa, kangomba na kubana mizani, shwaini!
 
Huyu dereva nchi imemshinda kabisa.watu wameanza kula mara moja tu kwa siku kutokana na vitu kupanda bei kiholela.Hadi tufike 2025 tutakuwa kila mwananchi amejikondea na kuonesha mbavu zake zote mwili mzima
Kumbe huyu dereva ndiyo analima mahindi,maharage, mchele, choroko na ngano eh?!
Huyu dereva ndiye kapandisha bei ya vyakula kenya, uganda zambia, burundi, rwanda...
Fanyeni kazi kwa maarifa na akili ili mle milo mitatu. Msitegeme dereva atawaletea milo mitatu
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Leo nimenunua sembe 1kg@1800/= huku DSM.
Acha nikalime mihogo nimeshuhudia wakulima wenzangu wakiuza gari (Canter) ya muhugo 2,700,00/= mwaka huu toka 600,000/= ya mwaka jana. Mtu kapiga milioni 18.9 za mihogo mwaka huu, mimi nilidharau muhogo sikulima.
Nilikuwa sijui sababu ya kupanda thamani mihogo kumbe watu wanashindia mlo mmoja wa mihogo huku DSM.
 
Hali ni tete hususan kwa wanyonge wanaotafuta kwa kubangaiza.......tunaenda kushuhudia udumavu kwa watoto ambao haujawahi kutokea kutokana na lishe duni, acha tuendelee kuagiza viiieite na ndege nyingine tano bila kusahau Yutongu.​
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Mahindi lazima yapelekwe nje ili mkulima apate faida. Kama ni rahisi kalime na wewe. Yaani unataka unafuuwa maisha kwa gharama za mkulima?! Unashangaza sana!!!
 
Mahindi lazima yapelekwe nje ili mkulima apate faida. Kama ni rahisi kalime na wewe. Yaani unataka unafuuwa maisha kwa gharama za mkulima?! Unashangaza sana!!!
Hakuna mkulima anayepata faida, mnaopata faida ni nyinyi madalali na matapeli mnaompa mkulima bei ndogo na bado mnabana mizani, kujaza lumbesa na kununua mazao shambani aka. kangomba, hovyo kabisa....
 
Ni kweli mkuu, lakini zama za JPM na zama za mama hazifanani!
Wakati wa JPM janga kubwa lililotikisa uchumi wetu ni Corona, na hapo tulipewa misaada kukabili mtikisiko wa kiuchumi japo kwanza sisi hatukusimamisha shughuli nyingi za uzalishaji, hata wananchi hawakwenda lockdown!
Lakin kipindi cha mama kumetokea mambo makubwa mawili, Uhaba mkubwa wa Mvua na vita ya Ukraine!
Hivi vyote kwa pamoja vimechangia mfumuko mkubwa wa bei za nafaka!
Hapa uhaba wa mvua umeleta shortage kwenye mazao mengi ya chakula, hivyo bei lazima ipande! wakati vita ya Ukraine imeleta mgogoro kwenye mafuta, Hapa gharama za uendeshaji wa shughuli nyingi zinazotegemea mafuta ikiwemo usafirishaji wa mazao lazima zipande! Hivyo serikali ifanye jitihada kupunguza usafirishaji wa mazao ya nafaka nje ya nchi kunaweza saidia kuepuka bei kupaa zaidi!
 
Mpumbavu mkubwa wewe, wakulima wetu ndiyo wakati wao wa kupata fedha na kuboresha maisha yao. Wewe badalanya kwenda kulima mahindi unakuja kuandika pumba JF.

Nenda na wewe ukalime halafu uone uchungu wa kuambiwa usiuze mahindi nje ya nchi.
Wewe mburula unajulikana kwa pointless
 
Black shit
 
Kama kulima rahisi nawe kalime bwashee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…