Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Mpumbavu mkubwa wewe, wakulima wetu ndiyo wakati wao wa kupata fedha na kuboresha maisha yao. Wewe badalanya kwenda kulima mahindi unakuja kuandika pumba JF.

Nenda na wewe ukalime halafu uone uchungu wa kuambiwa usiuze mahindi nje ya nchi.
Hiki kitu watu wengi hufata mkumbo, lkn hawajui mtu umelima kwa gharama zako yaan kila kitu umetumia ela lkn ukitaka kuuza unapangiwa wa kumuuzia na bei, hovyo sana
 
Kwa nchi hii wakulima ni vigumu kufaidika, hata bei ikipanda wanaofaidika ni wafanya biashara tu, mkulima yeye akivuna tu, anauza wala hana haja ya kisubilia eti bei zipande.na tatizo la mwaka huu licha ya sababu nyingine lakini mavuno hayakuwa mazuri kabisa.
Mkulima anaelima kibiashara hauzi haraka kama yule anaelima auze apate mlo na hao ni wachache na kilimo chao ni duni wanaolima kibiashara wengi wamenufaika sana
 
Enzi za mwendazake unga wa mahindi kuna wakati ulifitika kilo sh.2000/ na watu walipo nung,unika Kayafa akawaambia wakulima waongeze Bei Zaidi HAKUNA anayewasaidia shambani....
Eti leo chawa wameshasahau mpyuuuu
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna mkulima anayeenda kuuza mazao huko nje,
Bei ya shambani bado iko chini Ila inapandishwa na wafanyabiashara
Wapo mkuu na kuna mkulima maarufu wa mchele mbeya juzi tu kapata tenda ya kuuza maelfu ya tani za mchele kila mwezi kwenda Kenya au nae huyo sio mtanzania?
 
Mkulima anaelima kibiashara hauzi haraka kama yule anaelima auze apate mlo na hao ni wachache na kilimo chao ni duni wanaolima kibiashara wengi wamenufaika sana
Mkuu asilimia karibu 70, ya wakulima wetu ni kilimo cha kujikimu!!yeye alime apate chakula kinachobakia ni kuuza, akidhi mahitaji yake kwa muda huo.Sasa chakula kinapopanda bei yeye anakuwa hana mazao tena, kwani wenye pesa washanunua na kuyaweka store.Wengine hata pesa ya kuandaa mashamba tena kwa sasa hawana.
 
Wapo mkuu na kuna mkulima maarufu wa mchele mbeya juzi tu kapata tenda ya kuuza maelfu ya tani za mchele kila mwezi kwenda Kenya au nae huyo sio mtanzania?
Acha stori za tenda


Nenda Taveta ujionee mwenyewe
 
Wanachi wataumia sana
Hawana mtetezi
👇

Nipashe ilitembelea maeneo mbalimbali ya Dar es Salam na kubaini kupanda bei za bidhaa zinazotumiwa na kwa mlo wa kila siku ambazo ni mchele, maharagwe, unga wa ngano, unga wa sembe, dona na choroko.

Mchele kilo moja umepanda kutoka Sh. 1,800 au 2,000 hadi Sh. 2,700 daraja la kwanza na super kutoka Sh. 2,500 hadi 3,500, unga wa sembe na dona umetoka Sh. 1,200 hadi Sh. 1,600 na unga wa ngano Sh. 1,300 hadi 2,000 kwa kilo huku choroko ikipanda kutoka Sh. 1,500 hadi Sh. 2,500. Bei ya mfuko wa kilo tano za unga imepanda kutoka Sh. 6,000 hadi 8,000.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wamesema kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hizo, wamelazimika kula milo miwili kwa siku badala ya mitatu.

Mkazi wa Tabata, James Macha, alisema analazimika kutokunywa chai ya asubuhi kutokana na kupanda kwa bei za vitafunwa ikiwamo chapati, maandazi na vitumbua, hivyo ili aweze kumudu gharama nyingine za maisha ikiwamo kulipa kodi ya nyumba na kulipa ada ya shule.

Macha, mwenye mke na watoto wawili, alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo, sasa anatumia Sh. 3,000 kwa ajili ya kununua vitafunwa asubuhi kutoka Sh. 1,200 aliyokuwa anatumia awali. Alisema hali hiyo imetokana na vitafunwa hivyo kupunguzwa kipimo, hivyo kumlazimu kununua vingi ili vitosheleze.

Naye Mkazi wa Salasala, Mwajabu Abdul, mwenye watoto watatu anayefanya kazi ya saluni, alisema hali hiyo inawalazimu kutokula chakula cha mchana ili kuepuka gharama kubwa kutokana na kuwa na kipato kidogo.
"Wakati mwingine unajikuta umeamka na Sh. 5,000, hivyo kuigawanya upate miko mitatu si rahisi.

Tunachofanya na wanangu tunachemsha mihogo ya buku (Sh. 1,000) tunakunywa na chai saa tano asubuhi. Tukishashiba tena tunakuja kupika chakula saa 11:00 jioni, tunakula saa moja tunalala, siku zinasogea," alisema.

Mwajabu alisema awali walipata shida kwa sababu walikuwa wameshazoea kula milo mitatu hali iliyosababisha watoto kulegea na kusinzia wakati wa mchana lakini sasa wameshazoea na maisha yanakwenda sawa.

Dereva wa bodaboda eneo la Mwenge, Alex Mushi, alisema alichukua uamuzi wa kutokula chakula cha mchana baada ya kugundua kuwa anatumia pesa nyingi kula kwa mama ntilie.

"Kwa siku nikipata sana katika biashara yangu ni Sh. 25,000. Hapo Sh. 10,000 ni ya mwenye bodaboda, nabaki na Sh.15,000. Asubuhi chai tu Sh. 2,500, mchana ili ushibe lazima ule pande mbili za ugali maana unapimwa kidogo sana jumla Sh. 4,000. Jioni pia utumie Sh. 4,000 jumla Sh. 10,500 bado hujanywa maji. Sioni hata dalili ya kununua kiwanja," alisema.

Kutokana na kupanda huko kwa bidhaa, Mushi alisema kuna haja ya serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za nafaka kwa kuwa ndizo inasababisha gharama za vyakula kupanda huku watu wa hali ya chini wakiathirika zaidi.

Nipashe ilifunga safari mpaka kwa wauzaji wa vyakula ambapo Angela Maganga, muuzaji wa vitumbua Temeke, alisema amepoteza baadhi ya wateja baada ya kupunguza kipimo cha vitumbua ili apate faida kutokana na kupanda gharama za nafaka na mafuta ya kupikia.

Alisema ndani ya mwaka mmoja kilo moja ya mchele wa vitumbua imepanda kutoka Sh.1,400 hadi Sh.2,000 na mafuta lita moja ilikuwa Sh. 3,500 sasa Sh.5,000.

"Ni kweli dada nimepunguza kipimo cha upawa ili na mimi nipate faida nihudumie familia yangu, ndicho kimewakimbiza wateja. Serikali iangalie hizi nafaka mbona zinazopanda kila kukicha na zinaelekea kuua biashara zetu ambazo ndizo tunategemea kusomesha watoto,” alisema.

Naye Maria Kallaghe, mamalishe katika soko la Tandale, alisema kitendo cha wateja katika eneo hilo kutokula chakula cha mchana, kimemrudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu anapata faida nusu ya aliyokuwa anapata mwanzo.

"Mauzo yameshuka kutoka Sh. 50,000 hadi Sh. 30,000. Hapo nikitoa hela ya mtaji najikuta napata Sh. 10,000 faida na inategemea na siku. Ukiamka ukakuta mchele umepanda hapo tena faida inazidi kupungua. Kwa ufupi maisha ni magumu,” alisema.

SERIKALI IKO KAZINI
Agosti 15, mwaka huu, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alipozungumza jijini Dodoma, alisema serikali inaendelea kuchukua hatua ili kuwapunguzia wananchi athari zitokanazo na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu.

Alisema hatua hizo ni pamoja na kuwapunguzia gharama za uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa bidhaa, ili kuleta uhimilivu wa bei kwenye soko lengo likiwa kumlinda mlaji kwa kuhakikisha anapata bidhaa bora kwa bei stahiki na kuzuia upandishwaji holela wa bei za bidhaa.

Pia alisema serikali imeondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wazalishaji wa mbolea kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji, hivyo kuleta unafuu wa bei ya mazao muhimu ya chakula pamoja na kupunguza ushuru kwa maroli yanayosafirisha bidhaa.

Ripoti ya Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi (OECD), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kuhusu Mtazamo wa Kilimo 2022-2031 inaonyesha mazao ya kilimo kote duniani yatakabiliwa na changamoto za kimsingi kwa miaka 10 ijayo na kuzitaka nchi kuchukua hatua endelevu kukabiliana na changamoto hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza changamoto hizo ni kupanda kwa bei za mazao ya kilimo kulikosababishwa na mlipuko wa virusi vya corona, hali mbaya ya hewa katoka nchi muhimu za utoaji wa mazao, kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji na uuzaji usio na uhakika wa mazao ya kilimo kutoka Ukraine na Russia ambazo ni nchi muhimu zaidi za utoaji wa nafaka umeifanya hali ya hivi sasa izidi kuwa mbaya.

Chanzo: Nipashe
APPROXIMATELY soma hapa kuhusu ule mfumo niliokwambia usipoelewa hapa ndio baasi hauwezi kuelewa

Huu ni km mfano tu wa mfumo

Huu ni mfumo wa mfumuko wa bei

Soma vizuri taarifa hii kisha angalia hizo pesa zinavyorukaruka ilikua ngapi ikafika ngapi angalia hilo gap hapo umeliona?

Mfumo si huo hapo umeuona?

Sasa fikiria ujitafutie ukiwa nje ya huo mfumo sio ndani ya huo mfumo
 
Leo nimenunua sembe 1kg@1800= huku DSM.
Acha nikalime mihogo nimeshuhudia wakulima wenzangu wakiuza gari (Canter) ya muhugo 2,700,00/= mwaka huu toka 600,000/= ya mwaka jana. Mtu kapiga milioni 18.9 za mihogo mwaka huu, mimi nilidharau muhogo sikulima.
Nilikuwa sijui sababu ya kupanda thamani mihogo kumbe watu wanashindia mlo mmoja wa mihogo huku DSM.
Safi sana ,Acha nao wajipatie hela linalotokana na jasho la ukweli

Ova
 
APPROXIMATELY soma hapa kuhusu ule mfumo niliokwambia usipoelewa hapa ndio baasi hauwezi kuelewa

Huu ni km mfano tu wa mfumo

Huu ni mfumo wa mfumuko wa bei

Soma vizuri taarifa hii kisha angalia hizo pesa zinavyorukaruka ilikua ngapi ikafika ngapi angalia hilo gap hapo umeliona?

Mfumo si huo hapo umeuona?

Sasa fikiria ujitafutie ukiwa nje ya huo mfumo sio ndani ya huo mfumo
Kama nimekuelewa ni hivi kwa kuwa chakula kimekuwa ghali,ili usitumie ela nyingi kwenye kula inakubidi usinunue chakula chochote town,nina maana kuzama mikoa yenye vyakula vingi kwa mfano kama ukienda mbeya ukachukua kilo Mia za mchele,na kilo 50 za maharage,ukaenda katavi ukachukua gunia la mahindi kilo 100,ukaenda babati ukachukua dumu la mafuta ya alizeti,ukaja ukaviweka store kwa ajili yachakula kazi yako nikununua mboga tu,hapo unapiga bajeti ya hivyo vyakula vikupeleke hata miezi kadhaa
 
Mchele gredi ya mwisho kwa muonekano zile chenga kwa ajili ya unga wa vitumbua au uji wa mgonjwa kilo 1,700/=.
 
Sasa naona kidooogo umeanza kufukiria jinsi ya kujitafutia nje ya mfumo kudos ila bado endelea kujifunza mkuu
Kwakuwa mfumo wa watu wanaoishi bongo ni wakununua chakula cha kula siku hiyo dukanini bora kuchenji hiyo tabia na kujiwekea akiba cha chakula hata ya miezi mitano mbele,maana kununua kitu kodogo kidogo kinaongeza kitu hocho kuwa na thamani kubwa
 
Kwa nchi hii wakulima ni vigumu kufaidika, hata bei ikipanda wanaofaidika ni wafanya biashara tu, mkulima yeye akivuna tu, anauza wala hana haja ya kisubilia eti bei zipande.na tatizo la mwaka huu licha ya sababu nyingine lakini mavuno hayakuwa mazuri kabisa.


Mkuu dunia imebadilika na kama unadhani mazingira yanaruhusu utajirikie kupitia bei za shamba ingia uone moto wake watu wanasafirisha mahindi anafika na mzigo anakula loss
 
Back
Top Bottom