Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Mama Samia anajua anachokifanya.Kwa miaka mi5 sekta ya kilimo ilikufa kwa zaidi ya 50%.Watu kama Sumri walioachana na biashara ya mabasi na kwenda kulima mahindi kipindi cha kilimo kwanza,walifikia hali ya kujuta kuingia huko kwa sababu ya serikali ya awamu ya 5 kuharibu msingi wa masoko.Sasa hivi mama anarudisha hali ya ushindani katika sekta ya kilimo ilikuinua uchumi halisi wa mtanzania ambao unategemea kilimo kwa 70%.Mama Samia akili nyingi.


Baadhi ya wajanja wa mjini walikuwa wanafurahia na kusherehekea sana kufungwa mipaka bei za mazao zinaanguka wao wanakula kwa bei chee
 
Kuna mkulima anayeenda kuuza mazao huko nje,
Bei ya shambani bado iko chini Ila inapandishwa na wafanyabiashara

Bei ya shambani ni shilingi ngapi na sokoni ni shilingi ngapi usafiri nao ni shilingi ngapi ? Haya nendeni shambani si ndio kuna bei nzuri
 
Leo nimenunua sembe 1kg@1800/= huku DSM.
Acha nikalime mihogo nimeshuhudia wakulima wenzangu wakiuza gari (Canter) ya muhugo 2,700,00/= mwaka huu toka 600,000/= ya mwaka jana. Mtu kapiga milioni 18.9 za mihogo mwaka huu, mimi nilidharau muhogo sikulima.
Nilikuwa sijui sababu ya kupanda thamani mihogo kumbe watu wanashindia mlo mmoja wa mihogo huku DSM.

Mlo mmoja wapi watu wanashinda kwenye pombe hela zinachezewa kwenye pombe,bangi,ukahaba na anasa
 
Huyu dereva nchi imemshinda kabisa.watu wameanza kula mara moja tu kwa siku kutokana na vitu kupanda bei kiholela.Hadi tufike 2025 tutakuwa kila mwananchi amejikondea na kuonesha mbavu zake zote mwili mzima


Wasiomudu kwanini wasilime kama wakulima tu wapate hivyo vya shambani katika bei wanazozitaka
 
Hakuna mkulima anayepata faida, mnaopata faida ni nyinyi madalali na matapeli mnaompa mkulima bei ndogo na bado mnabana mizani, kujaza lumbesa na kununua mazao shambani aka. kangomba, hovyo kabisa....

kumbe kuna uwezekano wa kupata kwa bei ndogo kwa mkulima sasa waKanunue kwa bei ndogo kama walivyoweza hao madalali kununua kwa bei ndogo haina haja ya mbeleko ya nguvu za serikali bei ziporomoke
 
Na wewe ni tapeli unayejiita mfanyabiashara wa mazao?

Wakulima ni watu kama wewe hawajatenda kosa lolote mpaka wapewe mzigo wa kukulimia zao upate kwa bei chee bei unazozitaka weee ilhali hujasaidia chochote kwenye kulima kwao
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Gharama za uzalishaji mwaka jana pia zilikuwa juu mno. Acha wauze kwa Bei yoyote.
Mwakani pigeni kelele Bei zishuke sababu angalau mbolea zitanunuliwa kwa 70,000
 
Wanaouza mahindi kwa gharama sio wakulima ni wafanya biashara so kama selikal inasema wakulima wauze bei watakayo uhalisia inakuwa inasema na wafanya biashara wa mazao
 
Wanachi wataumia sana, hawana mtetezi.
👇

Nipashe ilitembelea maeneo mbalimbali ya Dar es Salam na kubaini kupanda bei za bidhaa zinazotumiwa na kwa mlo wa kila siku ambazo ni mchele, maharagwe, unga wa ngano, unga wa sembe, dona na choroko.

Mchele kilo moja umepanda kutoka sh. 1,800 au 2,000 hadi sh. 2,700 daraja la kwanza na super kutoka sh. 2,500 hadi 3,500, unga wa sembe na dona umetoka sh. 1,200 hadi sh. 1,600 na unga wa ngano sh. 1,300 hadi 2,000 kwa kilo huku choroko ikipanda kutoka sh. 1,500 hadi sh. 2,500. Bei ya mfuko wa kilo tano za unga imepanda kutoka sh. 6,000 hadi 8,000.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wamesema kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hizo, wamelazimika kula milo miwili kwa siku badala ya mitatu.

Mkazi wa Tabata, James Macha, alisema analazimika kutokunywa chai ya asubuhi kutokana na kupanda kwa bei za vitafunwa ikiwamo chapati, maandazi na vitumbua, hivyo ili aweze kumudu gharama nyingine za maisha ikiwamo kulipa kodi ya nyumba na kulipa ada ya shule.

Macha, mwenye mke na watoto wawili, alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo, sasa anatumia sh. 3,000 kwa ajili ya kununua vitafunwa asubuhi kutoka sh. 1,200 aliyokuwa anatumia awali. Alisema hali hiyo imetokana na vitafunwa hivyo kupunguzwa kipimo, hivyo kumlazimu kununua vingi ili vitosheleze.

Naye Mkazi wa Salasala, Mwajabu Abdul, mwenye watoto watatu anayefanya kazi ya saluni, alisema hali hiyo inawalazimu kutokula chakula cha mchana ili kuepuka gharama kubwa kutokana na kuwa na kipato kidogo.
"Wakati mwingine unajikuta umeamka na sh. 5,000, hivyo kuigawanya upate miko mitatu si rahisi.

Tunachofanya na wanangu tunachemsha mihogo ya buku (sh. 1,000) tunakunywa na chai saa tano asubuhi. Tukishashiba tena tunakuja kupika chakula saa 11:00 jioni, tunakula saa moja tunalala, siku zinasogea," alisema.

Mwajabu alisema awali walipata shida kwa sababu walikuwa wameshazoea kula milo mitatu hali iliyosababisha watoto kulegea na kusinzia wakati wa mchana lakini sasa wameshazoea na maisha yanakwenda sawa.

Dereva wa bodaboda eneo la Mwenge, Alex Mushi, alisema alichukua uamuzi wa kutokula chakula cha mchana baada ya kugundua kuwa anatumia pesa nyingi kula kwa mama ntilie.

"Kwa siku nikipata sana katika biashara yangu ni Sh. 25,000. Hapo Sh. 10,000 ni ya mwenye bodaboda, nabaki na sh. 15,000. Asubuhi chai tu sh. 2,500, mchana ili ushibe lazima ule pande mbili za ugali maana unapimwa kidogo sana jumla sh. 4,000. Jioni pia utumie sh. 4,000 jumla sh. 10,500 bado hujanywa maji. Sioni hata dalili ya kununua kiwanja," alisema.

Kutokana na kupanda huko kwa bidhaa, Mushi alisema kuna haja ya serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za nafaka kwa kuwa ndizo inasababisha gharama za vyakula kupanda huku watu wa hali ya chini wakiathirika zaidi.

Nipashe ilifunga safari mpaka kwa wauzaji wa vyakula ambapo Angela Maganga, muuzaji wa vitumbua Temeke, alisema amepoteza baadhi ya wateja baada ya kupunguza kipimo cha vitumbua ili apate faida kutokana na kupanda gharama za nafaka na mafuta ya kupikia.

Alisema ndani ya mwaka mmoja kilo moja ya mchele wa vitumbua imepanda kutoka Sh.1,400 hadi Sh.2,000 na mafuta lita moja ilikuwa sh. 3,500 sasa sh.5,000.

"Ni kweli dada nimepunguza kipimo cha upawa ili na mimi nipate faida nihudumie familia yangu, ndicho kimewakimbiza wateja. Serikali iangalie hizi nafaka mbona zinazopanda kila kukicha na zinaelekea kuua biashara zetu ambazo ndizo tunategemea kusomesha watoto,” alisema.

Naye Maria Kallaghe, mamalishe katika soko la Tandale, alisema kitendo cha wateja katika eneo hilo kutokula chakula cha mchana, kimemrudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu anapata faida nusu ya aliyokuwa anapata mwanzo.

"Mauzo yameshuka kutoka sh. 50,000 hadi sh. 30,000. Hapo nikitoa hela ya mtaji najikuta napata sh. 10,000 faida na inategemea na siku. Ukiamka ukakuta mchele umepanda hapo tena faida inazidi kupungua. Kwa ufupi maisha ni magumu,” alisema.

SERIKALI IKO KAZINI
Agosti 15, mwaka huu, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alipozungumza jijini Dodoma, alisema serikali inaendelea kuchukua hatua ili kuwapunguzia wananchi athari zitokanazo na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu.

Alisema hatua hizo ni pamoja na kuwapunguzia gharama za uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa bidhaa, ili kuleta uhimilivu wa bei kwenye soko lengo likiwa kumlinda mlaji kwa kuhakikisha anapata bidhaa bora kwa bei stahiki na kuzuia upandishwaji holela wa bei za bidhaa.

Pia alisema serikali imeondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wazalishaji wa mbolea kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji, hivyo kuleta unafuu wa bei ya mazao muhimu ya chakula pamoja na kupunguza ushuru kwa maroli yanayosafirisha bidhaa.

Ripoti ya Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi (OECD), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kuhusu Mtazamo wa Kilimo 2022-2031 inaonyesha mazao ya kilimo kote duniani yatakabiliwa na changamoto za kimsingi kwa miaka 10 ijayo na kuzitaka nchi kuchukua hatua endelevu kukabiliana na changamoto hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza changamoto hizo ni kupanda kwa bei za mazao ya kilimo kulikosababishwa na mlipuko wa virusi vya corona, hali mbaya ya hewa katoka nchi muhimu za utoaji wa mazao, kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji na uuzaji usio na uhakika wa mazao ya kilimo kutoka Ukraine na Russia ambazo ni nchi muhimu zaidi za utoaji wa nafaka umeifanya hali ya hivi sasa izidi kuwa mbaya.

Chanzo: Nipashe
Kwani Magufuri alikuwa anawapelekea wananchi wote chakula??
 
Wanaouza mahindi kwa gharama sio wakulima ni wafanya biashara so kama selikal inasema wakulima wauze bei watakayo uhalisia inakuwa inasema na wafanya biashara wa mazao

Wanaotaka bei rahisi si ndio hapo sasa kumbe wakulima wanauza kwa bei rahisi kwa nini sasa wasiende wanakonunua wafanyabiashara
 
WATANZANIA ROHO YENYE INDA TUMEITOA WAPI KUTAKA WENGINE WATESEKE?

05 September 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Wengine ni hawa hapa wanajiita ni Wadau wa Stendi ya mabasi ya Magufuli jijini Dar es Salaam wenyewe umimi na roho ya inda wanataka wasafiri wateseke ili wao wapate mlo na kwenda mbali kubeba mabango kuichagiza serikali iwatese abiria wa mabasi yaendayo mikoani


MamaNtilie, machinga, wenye mogahawa n.k katika stendi ya kuu ya mabasi ya kwenda mikoa iliyopo jijini Dar es Salaam wataka waziri mkuu, waziri wa TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na mkuu wa mkoa waingilie kati ili kusiwepo vituo vidogo vya kupakia na kuteremsha abiria katika jiji la DSM ambalo ni jiji lenye eneo kubwa (upana) kupita yote Afrika Mashariki hata kama bado mabasi hayo yatapita kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli.

Kubwa wadau hao wafanyabiashara ktk kituo cha mabasi cha Magufuli wanataka abiria wateseke ili biashara zao zineemeke
Source : millard ayo
 
Anza kulima hutalalamikia bei.

Ni kweli waondoke mjini wakafanye shughuli zingine zenye faida au wabaki lakini waanzishe kilimo cha mazao ya chakula . Wakulima wavunja jasho wanajituma sana kwa kujitegemea wenyewe sana sana anayewasaidia wakulima hawa ni mnunuzi mfanyabishara wa nafaka.

Mjini kila mtu anataka kuwa waendesha bodaboda au bajaji n.k kwa kuisikiliza CCM ikigawa mikopo ya pikipiki za bodaboda, bajaji na umachinga hivyo sekta yao kuzidiwa na utitiri wa watoa huduma za usafiri au chinga mitaani.

Wajiulize mbona waendesha teksi / taxi wa miaka mingi mjini walikubali ushindani wa uber, bodaboda na bajaji wakajiongeza kwa kuamua kufanya shughuli zingine au kuboresha huduma zao hivyo kuwa na abiria wa uhakika kwa kutumia simu n.k
 
Ni kweli waondoke mjini wakafanye shughuli zingine zenye faida au wabaki lakini waanzishe kilimo cha mazao.

Mjini kila mtu anataka kuwa waendesha bodaboda au bajaji n.k

Wajiulize mbona waendesha teksi / taxi wa miaka mingi mjini walikubali ushindani wa uber, bodaboda na bajaji wakajiongeza kwa kuamua kufanya shughuli zingine au kuboresha huduma zao hivyo kuwa na abiria wa uhakika kwa kutumia simu n.k

Hakuna muendesha taxi mwenye mshahara mmoja/anayetegemea taxi tu ambaye bado yuko sokoni.
 
Back
Top Bottom