Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,490
- 7,422
Kwa Tz, hakuna mkulima anayeweza kuwa na uwezo wa kufanya hiyo biashara eti maefu ya tani za mchele kwa mwezi?
Hujanielewa, mimi nilikuwa namkatalia jamaa, aliyesema kuwa wakulima msimu huu wamefaidika kutokana na nafaka kuwa juu, nikasema sio kweli, kwani wakulima wetu wengi wakaishavuna wao ni kuuza tu, ila wanao kuja kufaidika ni wafanya biashara ambao wao hununua mazao mengi kipindi cha mavuno na kuyaweka kwenye maghara hadi bei zipande, ndipo wauze, sikatai nao kuna wakati wanapata hasara kutokana na bei, kuwa chini, kwa muda mrefu, hii biashara ya mazao nimeifanya sana hada mpunga ninajua nini nasema.Mfano kipindi cha mavuno una nunua gunia la mpunga kwa tsh.25, 000 ukiuhifadhi baada ya muda hasa kuanzia miezi ya 12-1, hilo gunia unaweza kuliuza kwa 80, 000-100, 000!!
Mpunga wa elfu 25 gunia ilikuwa wapi hiyo nami nijue aisee? Maana huu mwakaa kote bei zimefumuka na zinarandana vibaya sana hii nchi yote hapa sijui bei za Mpanda tu