TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

Mi nasubiri za kuona chanzo cha utajiri wake ni nini? Maana kama Mzee Edwin Mtei aliiba pale BOT etc, huyu lazima kuna chanzo ambacho siyo sahihi
Chanzo ni Kodi zetu kupitia mkono wa Mramba alizokwapua akiwa waziri wa fedha kisha akapewa adhabu ya kwenda kupiga picha akifanya usafi hospital ya mwananyamala,kisha akawa waziri wa ujenzi na usafirishaji akaua reli na Air Tanzania ili Precious ikue,na malori na mabus yapate biashara.
 
Chanzo ni ufisadi kupitia Kodi zetu kupitia mkono wa Mramba alizokwapua akiwa waziri wa fedha kisha akapewa adhabu ya kwenda kupiga picha akifanya usafi hospital ya mwananyamala,kisha akawa waziri wa ujenzi na usafirishaji akaua reli na Air Tanzania ili Precious ikue,na malori na mabus yapate biashara.
 
Alale mahali pema anapostahili.

NOTE: Hakuna tajiri anayeweza kukueleza kiini cha utajiri wake hata siku moja.

Nimeona kagusia kuhusu kuuza kahawa, udereva wa malori n.k ilikuwa hatua nzuri pia
Siyo wote Mkuu. Wengine tuna vyanzo clean kabisa. Kuna Yule MTU wetu alikuwa anataka matajiri wageuke mashetani. Sasa akamtaka jamaa mmoja aweke vyanzo vya utajiri na awasilishe statement za bank zote. Jamaa alipeleka vyanzo vyote na mwenye wivu akabana ngenge. Kisa tu kumbe ni kwa vile tajiri alikuwa mchaga na yeye ilikuwa damu kunguni kwao. Mungu fundi.
 
Ilishamilikiwa na watu wengine kitambo alibaki na share kidogo sana.
Bado Late Shirima ni majority shareholder maana anamiliki 42% plus na nyingine zilizobaki zinamilikiwa na minority waliojigawa ikiwemo Kenya Airways 41%, wafanyakazi 2% Precision na Public 14%. Muwe mnafanya kautafiti kidogo ili ukisema Jambo usionekane ni chuki. Pamoja sana
 
IPP bado ipo
Mkuu waambie kuwa wachaga wengi biashara zao zinaendelea kwa kuwa wanaweka misimgi imara ya succession ( Wana succession plan). Wajifunze kwa Marehemu Mengi. Pamoja na ufala wa Gold Digger aliyetaka aifilisi IPP Holding ili akaishi Dubai na yule Banake lakini IPP ilisimama imara na walioachwa ambao ni watoto na Management imara. Mengi aliwekeza kwa warithi na alikuwa mjaja Sana hakumuweka Jack na Warithi. Hata ule Wosia kama kweli Mengi alihusika kuuandika basi aliandika kiufundi Sana akijua Jack hatatoboa nao. Chezea Mangi wewe.
 
Huyu mwamba hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake?
 
Mtu akishauza hisa za kampuni Kwa watu wengine...hawi tena 'mmiliki"..anabaki kuwa founder...kichwa kingepaswa kusema "muasisi wa Precision air"..
Hana tena majority shares..
Ameuza 49% ya Hisa Kwa KQ
 
Kula 10 Mkuu. Yaani watu tunapambana halafu jinga Moja linawaza tu kuwa ukiwa tajiri ni mwizi. Najitolea mfano Mimi nikiwa kijana mdogo kabisa nilianza kuweka bank fixed account Ile pesa napewa kwenda shule I e sehemu ya pocket money. Na nilikuwa siyo Mtumiaji wa pesa hovyo. Nikirudi likizo June na FDR ina mature naongezea na nyingine narudishia. By the time namalizia form 4 nilikuwa na pesa nzuri. Nikiwa nasubiri kuingia F5 nikajipinda kazi mahali miezi kadhaa nikapata pesa nikaongeza FDR. Niliingia chuo nikiwa na millions kadhaa. Nikaongeza na boom FDR ikawa inakuwa kwa speed ya radi. Kwa sabanu ya uchapakazi mzuri lecturers wakaniona hivyo nikawa napewa research assistant tasks na za pesa nzuri Sana. I made millions nikarejesha kwenye FDR. I graduated well nikapata free scholarship na madola ya ukweli. Hapo sasa ndiyo utajua FDR ilikuwa kwa Kasi ipi. By the time namalizia scholarship na degree kadhas unafikiri nilkuwa na millions ngapi? Baadaye nikaingia biashara za Shareholding na biashara nyinginezo clean. Hivi utaniitaje mwizi ukisoma figure za pesa niliyokuwa nayo? Halafu biashara ni akili kubwa. Kwa umri wangu huu situmikii pesa bali pesa Inatitumikia na nimeachana na biashara za kuibiwa. Nafanya biashara za kupigiwa simu au automatic SMS kuwa biashara ime mature njoo tuongee biashara mpya. Katika biashara kila mmoja anachagua inayolipa na Mimi nilichangua stress free businesses na zinazolipa na ambazo hata nikizeeka bado zitaendelea na watoto wanazijua na sharti waziendeleze maana zitakuwa kwenye Foundation. Na nyingi ni silent businesses maana hutasikia Zogwale akitajwa waziwazi kama wengine. Hivyo inabidi kuheshimu struggle za watu japo pia mijizi IPO.
 
Ni sawa na kusema taarifa ya CAG ya kupotea kwa zaidi ya trilioni 2 ni ya uongo kwa sababu haijadhibitika hela zilizopotea zilichukuliwa na kina nani. Hela ikipotea njia hii kuna njia nyingine inaingia, kutojulikana imeenda wapi haimaanishi haijapotea.

Vilevile kwenye biashara kuna vitu wazi kabisa, kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa bongo ni co-owner wa viwanda viwili vya bidhaa moja muhimu, pamoja na biashara nyingine. Kwenye story yake hakuna sehemu atataja jinsi anavyofanya kazi kwa mgongo wa kiongozi mkubwa serikali ya awamu ya tatu na ndio maana akamiliki usimamizi wa viwanda, sanasana atakwambia alivyokuwa fundi magari sijui gereji ghafla story inaruka unakuja kwenye kumiliki viwanda na hapo katikati kuna nafasi wazi.

Umeona kiongozi mmoja mkubwa awamu ya 6 anaenda zindua hoteli uko kwao eti "anachochea uwekezaji" wa mkulima mmoja aliyejenga hoteli. Kiongozi mwingine awamu ya nne alienda zindua shule binafsi ambayo inafanya vizuri sana kwenye matokeo na mmiliki wa hiyo shule eti alikuwa mvuvi na kaishia darasa la saba, na huyo kiongozi hajawahi zindua sio shule tu ya binafsi nyingine, hata vyuo binafsi hajawahi.

Au nawewe ni wale mliokubali Masanja Mkandamizaji alivyoonyesha mali kisha akasema analima mpunga na ana mashine za kulimia ndio anakopata hela, miaka michache tunamuona mkulima wa mpunga kaanzisha kanisa akatumie muda wake kukusanya waumini, mwaka huu akaanza kurusha vipindi studio kwa kulipwa.

Tunarudi palepale kwa Honoré de Balzac, kama mtu hawezi elezea maelezo ya kueleweka kuhusu mali zake ujue kuna jinai nyuma. Huu sio uchawi wala ujinga, huu ndio msingi wa accountability duniani na ndio msingi wa auditing.
Ila kwetu sisi Shabiby akisema alinunua basi at the age of 19 kwa kuuza karanga akiwa shule watu wanakubali, hakuna anayetaka kujua kule Gairo biashara gani ya siri ilitendeka because it was a well executed crime.
 
Kifo hiki jamani ,,, nakumbuka wayback nikiwa mdogo tunaishi Kijiji Cha nayeme , tukisikia helicopter au ndege ndogo hizi zikipita usawa wa chini , Mimi na wenzangu tulikuwa tunasema ngaleku anapita [emoji28][emoji28], kutokana na historia yake ya kumiliki ndege. Kiukweli biashara ya kahawa hii familia ya ngaleku wameifanya sana. Maana maeneo ya kibaoni hapo walikuwa na ofisi Yao hapo . Kipindi nakua dada yake huyu ngaleku ambaye alikuwa ni mama wa umri kidogo alikuwa anaitwa mama mganga ndio alikuwa anaisimamia hiyo biashara maeneo ya kibaoni.
 
Ukibahatika kusoma riwaya ya the godfather ya Mario puzo , ukurasa wa kwanza kabisa mwandishi anaanza na nukuu inasema kwamba " behind every great fortune there's crime" . Upo sahihi kwa hiki ulichokisema hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…