Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mkuu tumekusikia...Kuna jamaa nadhani na yeye ni ndugu wa huyu mzee maana na yeye ukoo wao ni Shirima.
Miaka ya 2010 baada ya kumaliza chuo akapata kazi kwenye hilo shirika, baada ya muda akaacha kazi akaanza kuporomosha majumba.
Ila nasikia aliiba hela kwenye hiyo kampuni akaacha kazi,
Mpaka sasa hivi mali anazomiliki jamaa haziendani na muda aliokaa kazini kabisa, hata kama analipwa kama mbunge.
Wachaga wezi sana.
Marekebisho yamepokelewa na ansard imerekebishwaOndoa hiyo "na" katika sentensi yako
watu wako busy na kiatu cha Mfungaji bora wakati Muarabu anakamilisha taratibu za kukeketa Bandari zote za Tanganyika200% true
Kizazi hichi cha punyeto + simba na yanga hamna kitu
Haina kwere man. Karibu bro.Nini tena mkuu Mad Max? Halafu nitaku check PM baadaye!.
Mi nasubiri za kuona chanzo cha utajiri wake ni nini? Maana kama Mzee Edwin Mtei aliiba pale BOT etc, huyu lazima kuna chanzo ambacho siyo sahihiBado nasubiri comment za masikini wenzangu za kujipa moyo utaskia "Hata matajiri wanakufa cha muhimu kuishi kwa upendo"
tutafute pesa huo ujinga hautusaidii
Pole babuR.I.P classmate
Nimeumia sana
Kweli tunabaki na vilaza , wapuuzi , wanauza mpaka bandari yetu pendwa .Innalillah wainna ilayh rajiuun
Akili kubwa zinaondoka tunabaki na vilaza
View attachment 2652129
Mmiliki wa Shirika la Ndege Nchini Tanzania la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima, ameaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya AgaKhan, Jijini Dar es Salaam
===========
Mfahamu zaidi Michael Ngaleku Shirima
Michael Ngaleku Shirima CEO wa Shirika la Ndege za Precision Air alianza kufahamika zaidi na watu baada ya ndege za shirika kukumbwa na tafrani za hapa na pale zikihusisha ajali iliyotokea jijini Mwanza ambapo ndege ya shirika hilo ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege Bukoba na kulazimika kugeuka Mwanza ambapo rubani aliona ni vyema kuishusha ndege hiyo kweye maji ya ziwa Victoria.
Michael Shirima ni moja kati ya wapambanaji ambao wamepambana kutoka chini hadi kufikia mafanikio ya juu kwa kuwa alikuweka ujasiri na kutokata tamaa. Michael alizaliwa mwaka 1943 huko Usseri Rombo Mkoani Kilimanjaro, baada ya kumaliza shule na kila kitu aliamua kuingia katika ulimwengu wa wachakarikaji kukimbiza ndoto zake ambazo alizigeuza kuwa mipango na baadaye utekelezaji.
Michael aliajiriwa kwa muda kidogo na hapa anasema “Nilipokuwa naanzisha Shirika la ndege la Precision Air haikuwa kama lilivyo sasa hivi lilianza kidogo, likakuwa. Nimekulia kwenye Taasisi ya usafiri wa anga. Nilipofikisha miaka 18 ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mambo ya ndege (ilikuwa ndege ndogo). Ndipo ilipoingia kwenye damu na ijapokuwa nilibadilisha mawazo mara kwa mara lakini nilirudi kwenye wazo langu. Sikuanzisha Precision Air moja kwa moja lakini nilifanya kazi kwenye Shirika la ndege ya East African Airways kwa miaka 12 Jijini Nairobi. Lilikuwa ni Shirika la Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda”
“Mtaji wa kuanzisha Kampuni ya Precision Air niliutoa kwenye Kahawa. Ni kazi ambayo ilikuwa haifanywi na watu wengi. Na pia nilikuwa dereva wa malori. Nilikuwa napeleka mizigo Mwanza kutoka Moshi. Nilikuwa napeleka mbao kule. Pia nilikuwa nanunua mafuta ya pamba naleta Moshi” Mzee Michael Shirima, Founder wa Precision Air na Mwandishi wa kitabu cha On My Father Wings
“Tuna wafanyakazi 300. Hii kazi ni ngumu Sana, sio watu wengi wanaweza kuifanya. Kuna Mtaalamu aliandika kwamba ukitaka kuwa Milionea (Dola kwa mfano) uwe Bilionea halafu uingie kwenye kazi ya kuendesha Shirika la ndege ndio utakuwa Milionea. Na huingii kwenye kazi hii ili uwe tajiri au utengeneze fedha hapana unaingia kwenye kazi kwa sababu ya kupenda passion. Na Mimi sifanyi kazi kwa maono nafanya kazi iliyopo sasa hivi”
Yule wa lushoto bumbuli lini? Au wa mtama?View attachment 2652129