Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Inasikitisha sana, lakini inatukumbusha ya kuwa maisha ya hapa duniani yana mwisho na wote tutaondoka; tuishi kwa kumpendeza allah
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dr Saa100, Dr Abood, Dr Musukuma, Dr Doto Biteko, Dr Gwajima, Dr Angelina Mabula 🙆♂️Kwenye jina lake halianzi na Dr wala Pro lakin kafanya makubwa
Pumzika kwa amani akili kubwaz
Hawa wote wanachofanya kikubwa ni kutuibia kwa kalamu na wengine kuwa machawa ili waleDr Saa100, Dr Abood, Dr Musukuma, Dr Doto Biteko, Dr Gwajima, Dr Angelina Mabula 🙆♂️
[emoji23][emoji23]wote wa munguInnalillah wainna ilayh rajiuun
Akili kubwa zinaondoka tunabaki na vilaza
Shirima wizi wake nauunga mkono ingawa sipendi wezi, unajua hata Nyerere kuna siku alisifia wezi wa mbolea. Kuna mbolea ilikuwa inatolewa kwa ruzuku wanaopewa wanalima hovyo jamaa mmoja akaiba akalima kwa usahihi akapata mavuno mengi na kukidhi haja ya serikali ya uzalishaji wa chakula.Mi nasubiri za kuona chanzo cha utajiri wake ni nini? Maana kama Mzee Edwin Mtei aliiba pale BOT etc, huyu lazima kuna chanzo ambacho siyo sahihi
Alifariki muda tu, Soma Kitabu chake "On my father's wing"Mkewe yupo hai au alikufa kabla yake?
SEMA watanzania woooote bana vipi wewe!? Karibu nipo kiboriloni Kuna mbege safi!!SAd news, pole kwa WA-ROMBO wote, wana kilimanjaro, familia ya SHIRIMA na mwanae MIKE SHIRIMA MAWALA na familia ya kina OBREY MAWALLA.
Kweli kabisa..Innalillah wainna ilayh rajiuun
Akili kubwa zinaondoka tunabaki na vilaza
Alale mahali pema anapostahili.View attachment 2652129
Mmiliki wa Shirika la Ndege Nchini Tanzania la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima, ameaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya AgaKhan, Jijini Dar es Salaam
===========
Mfahamu zaidi Michael Ngaleku Shirima
Michael Ngaleku Shirima CEO wa Shirika la Ndege za Precision Air alianza kufahamika zaidi na watu baada ya ndege za shirika kukumbwa na tafrani za hapa na pale zikihusisha ajali iliyotokea jijini Mwanza ambapo ndege ya shirika hilo ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege Bukoba na kulazimika kugeuka Mwanza ambapo rubani aliona ni vyema kuishusha ndege hiyo kweye maji ya ziwa Victoria.
Michael Shirima ni moja kati ya wapambanaji ambao wamepambana kutoka chini hadi kufikia mafanikio ya juu kwa kuwa alikuweka ujasiri na kutokata tamaa. Michael alizaliwa mwaka 1943 huko Usseri Rombo Mkoani Kilimanjaro, baada ya kumaliza shule na kila kitu aliamua kuingia katika ulimwengu wa wachakarikaji kukimbiza ndoto zake ambazo alizigeuza kuwa mipango na baadaye utekelezaji.
Michael aliajiriwa kwa muda kidogo na hapa anasema “Nilipokuwa naanzisha Shirika la ndege la Precision Air haikuwa kama lilivyo sasa hivi lilianza kidogo, likakuwa. Nimekulia kwenye Taasisi ya usafiri wa anga. Nilipofikisha miaka 18 ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mambo ya ndege (ilikuwa ndege ndogo). Ndipo ilipoingia kwenye damu na ijapokuwa nilibadilisha mawazo mara kwa mara lakini nilirudi kwenye wazo langu. Sikuanzisha Precision Air moja kwa moja lakini nilifanya kazi kwenye Shirika la ndege ya East African Airways kwa miaka 12 Jijini Nairobi. Lilikuwa ni Shirika la Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda”
“Mtaji wa kuanzisha Kampuni ya Precision Air niliutoa kwenye Kahawa. Ni kazi ambayo ilikuwa haifanywi na watu wengi. Na pia nilikuwa dereva wa malori. Nilikuwa napeleka mizigo Mwanza kutoka Moshi. Nilikuwa napeleka mbao kule. Pia nilikuwa nanunua mafuta ya pamba naleta Moshi” Mzee Michael Shirima, Founder wa Precision Air na Mwandishi wa kitabu cha On My Father Wings
“Tuna wafanyakazi 300. Hii kazi ni ngumu Sana, sio watu wengi wanaweza kuifanya. Kuna Mtaalamu aliandika kwamba ukitaka kuwa Milionea (Dola kwa mfano) uwe Bilionea halafu uingie kwenye kazi ya kuendesha Shirika la ndege ndio utakuwa Milionea. Na huingii kwenye kazi hii ili uwe tajiri au utengeneze fedha hapana unaingia kwenye kazi kwa sababu ya kupenda passion. Na Mimi sifanyi kazi kwa maono nafanya kazi iliyopo sasa hivi”
utabaki kusema wachagga wezi...huku waswahili wakiuza bandariKuna jamaa nadhani na yeye ni ndugu wa huyu mzee maana na yeye ukoo wao ni Shirima.
Miaka ya 2010 baada ya kumaliza chuo akapata kazi kwenye hilo shirika, baada ya muda akaacha kazi akaanza kuporomosha majumba.
Ila nasikia aliiba hela kwenye hiyo kampuni akaacha kazi,
Mpaka sasa hivi mali anazomiliki jamaa haziendani na muda aliokaa kazini kabisa, hata kama analipwa kama mbunge.
Wachaga wezi sana.
Unakosea sana. Mtu kufa akiwa na miaka 80 ni habari? Ameshapita expectancy age na ameshainjoi sana tu maisha.!Rip!pole KWA FAMILIA,matajiri wazawa wanaitwa sana katika zama za muongo mpya!!!
Matajiri wa Bongo hawana MAISHA kabisa AISEH!wanaitwa sana!labda Mungu anawapenda ZAIDI!
Wale wengine MBONA hawaitwi!!?wale wenye asili ya asia MBONA hawaitwi!!?hawana hiyo 80!!?Unakosea sana. Mtu kufa akiwa na miaka 80 ni habari? Ameshapita expectancy age na ameshainjoi sana tu maisha.!
Unadhani inaweza kuwa ni hujuma? Hapana! Unaweza kunitajia hao matajiri wenye asili ya Asia wenye miaka kuanzia 80?Wale wengine MBONA hawaitwi!!?wale wenye asili ya asia MBONA hawaitwi!!?hawana hiyo 80!!?
Kama ni sawa Bas poa!!