Michango ya harusi ni mzigo kuliko Ada ya shule

Michango ya harusi sio mzigo umaskini wako ndio mzigo wewe mleta mada

Pambana na umaskini wako utoke mleta mada .Umaskini ukikutoka hutaona michango ya harusi mzigo lofa mkubwa wewe pamoja na malofa wenzie walio like mada yako na kukuunga mkono

Mo Dewjiau Bakheresa hata apeleke kasi za michango laki moja haimpi shida kuchangia

Ulofa unakusumbua
Masikini mna akili fupi sana.
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Jinsi unavyolalamika ndivyo laana na mikosi itakavyoiandama ndoa ya hao waliokupa kadi. Kosa kubwa wanalofanya wanandoa wa siku hizi kudhani ndoa bora ni tukio na mbwe mbwe za harusi. Kumbe hapo ndipo wanapobeba mikosi,laana za kishirikina na mabalaa mengine. Wengi hurogwa kupitia zawadi za harusi bila kujua.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
tena mzigo mkubwa sana. mi sitaki hata kuisikia.
 
Miaka ya nyuma ndoa zilifungwa kwa bajeti ya mwanaume tu kulisha wahudhuriaji mpaka wapita njia, hizi harusi za ukumbini wanaoingia ni wachache tena kwa kadi za ualiko lakini ni gharama kubwa za michango. Wengine wanafungia ndoa bomani halafu anaipeleka ukumbini kwa kadi ya kuingilia waliotoa michango tu, unakuta single 50000 na double ni 100000, hizi ni pesa nyingi sana ni ufahari usio na maana kwa jambo la kuoa tu
 
Michango ya harusi sio mzigo umaskini wako ndio mzigo wewe mleta mada

Pambana na umaskini wako utoke mleta mada .Umaskini ukikutoka hutaona michango ya harusi mzigo lofa mkubwa wewe pamoja na malofa wenzie walio like mada yako na kukuunga mkono

Mo Dewjiau Bakheresa hata apeleke kasi za michango laki moja haimpi shida kuchangia

Ulofa unakusumbua
Kawapelekee kadi hao akina MO halafu urudi utupe mrejesho wa dhati kabisa.
 
Jinsi unavyolalamika ndivyo laana na mikosi itakavyoiandama ndoa ya hao waliokupa kadi. Kosa kubwa wanalofanya wanandoa wa siku hizi kudhani ndoa bora ni tukio na mbwe mbwe za harusi. Kumbe hapo ndipo wanapobeba mikosi,laana za kishirikina na mabalaa mengine. Wengi hurogwa kupitia zawadi za harusi bila kujua.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Acha imani potofu wewe utachelewesha mafanikio yako.
 
Nikiangalia kadi nilizonazo zinazodai michango Ni Kama kumi. Kiwango Cha chini Ni laki mojà. Hivyo nahitaji milioni Moja mpàka end of May kukidhi michango hiyo.

Sawa ni hitaji la kijamii, lakini ni changamoto! Lazima michango iwepo ila, Swali langu kuu Ni Hili:

Je tunawezaje kufanya harusi zetu bila michango mikubwa au harusi bila michango?
Swali linapaswa kuwa, Je inawezekana kufanya Harusi bila kutembeza kabisa bakuli la Mchango?
Jibu ni Ndiyo, inawezekana.
 
Ukiwa tajiri unachangisha mchango wa nini?
Wanaochangisha michango ndio maskini au wana mawazo ya kimasikini.
Mwombe Mungu akuondolee umaskini
Kifupi Tatizo sio michango una umaskini wa kufa mtu
 
Kifupi ukiona mtu analalamikia michango ya harusi kuwa ohhh imezidii ujue huyo lofa sana. Full stop
Aende kwa Mwamposya akaombewe apate Pesa
We jamaa Fala sana yani unaamini mwamposa akikuombea unapata pesa?
 
Masikini na anayatembeza bakuli la mchango huku akituma meseji za ususmbufu kukumbusha watu kila siku.
Hakuna kitu kibaya kama umaskini uogope kama ukoma vikao vya harusi vya matajiri wala hata hawapangiani viwango

Wanauliza bajeti shilingi ngapi ? anaibuka mmoja tu anaandika cheque ya bajeti yote anasema pelekeni kadi bure kwa ndugu na marafiki waje hakuna mchango ila zawadi kuja nazo ruksa ruksa

Umaskini ndio Tatizo usipochangia kiharusi cha mtu anaapa kutokuchangia chochote cha shida au kufika hata msiba wa familia yenu kisa wewe lofa hukumchangia kaharusi kake au nduguye kanakomhusu!!!

Umaskini mbaya sana
 
jamii yetu bado ina changamoto nyingi zinazohitaji pesa kutatuliwa. Japo sherehe ni sehemu ya maisha ila suala la michango ya harusi ni cancer kwenye jamii.

Watu wanapotaka kuoana watenge kiasi cha pesa kufanikisha jambo lao kama ambavyo mambo mengine kwenye maisha yanavyofanyika. Kisha huyo mtu awaite ndugu na jamaa zake bila kuwadai michango. Wakiamua kuja na zawadi ni sawa tu ila wenye harusi wasiweke tarajio kubwa.

Kama huna uwezo wa kugharamia harusi yako fanya iwe tukio la kawaida kama yalivyo mambo mengine. Isitoshe hizi harusi za mbwembwe nyingi zinaishia kwenye kufarakana tu na ndo hazidumu. Hili nimechomekea tu lakini.

Jambo ambalo nilishafuta kwenye kumbukumbu za ubongo wangu ni kuchangisha michango ya harusi, iwe kwangu mwenyewe ama watoto wangu. Watoto itabidi wajue kabisa kuwa wakitaka mambo ya harusi waanze kufanya savings kufanikisha jambo lao bila kutegemea michango. Kwanza watu wengi wanatoa kwa kulalamika tu.

Sijaona watu wanaotoa kwa moyo wote, kwanini tuendelee kulazimisha jambo ambalo tunalazimisha watu na tena katika jamii maskini kama hii?
 
Masikini na anayatembeza bakuli la mchango huku akituma meseji za ususmbufu kukumbusha watu kila siku.
Na wewe kwa nini utumiwe meseji ya kukumbushwa kama ni mtu wa karibu? Itakuwa na wewe lofa.Tajiri akiambiwa mchango huu hahitaji reminder anaandika kwenye diary lini atoe au phone alert I'm alert ku.mre mind kuwa una obligation ya mchango wa harusi hahitaji meseji au phone call milofa ndio inahitaji phone call na meseji

Lofa kutoa mchango shida sana hasa ya Harusi
 
jamii yetu bado ina changamoto nyingi zinazohitaji pesa kutatuliwa. Japo sherehe ni sehemu ya maisha ila suala la michango ya harusi ni cancer kwenye jamii.

Watu wanapotaka kuoana watenge kiasi cha pesa kufanikisha jambo lao kama ambavyo mambo mengine kwenye maisha yanavyofanyika. Kisha huyo mtu awaite ndugu na jamaa zake bila kuwadai michango. Wakiamua kuja na zawadi ni sawa tu ila wenye harusi wasiweke tarajio kubwa.

Kama huna uwezo wa kugharamia harusi yako fanya iwe tukio la kawaida kama yalivyo mambo mengine. Isitoshe hizi harusi za mbwembwe nyingi zinaishia kwenye kufarakana tu na ndo hazidumu. Hili nimechomekea tu lakini.

Jambo ambalo nilishafuta kwenye kumbukumbu za ubongo wangu ni kuchangisha michango ya harusi, iwe kwangu mwenyewe ama watoto wangu. Watoto itabidi wajue kabisa kuwa wakitaka mambo ya harusi waanze kufanya savings kufanikisha jambo lao bila kutegemea michango. Kwanza watu wengi wanatoa kwa kulalamika tu.

Sijaona watu wanaotoa kwa moyo wote, kwanini tuendelee kulazimisha jambo ambalo tunalazimisha watu na tena katika jamii maskini kama hii?
Ulichoandika naunga mkono Kifupi usimchangishe maskini mchango wa harusi ana changamoto nyingi za ulofa wake lofa mkubwa

Changisha matajiri achana na maskini hata kama ni kikarani serikalini au taasisi zake
 
Asante sana Mkuu. Michango wachangishane wenye uwezo. Kumchangisha maskini ni unyanyasaji kifikra. Unakuta kabisa mtu hata kula yake ni taabu ila analazimishwa kuwekwa kwenye group la familia kwamba nayeye achangie sijui 100K. Ambapo huyo mtu hajui hata kesho anakula nini. Huu ni unyanyasaji mkubwa dhidi ya watu maskini. Isitoshe hata watu wenye maisha ya kati na wao hawapaswi kuchangishwa maana na wao wanalalamika tu kila siku huko maofsini. Wachangishane wenye uwezo (matajiri) kama hiyo michango ni muhimu sana.
 
Kuna jamaa moja kachangisha mchango wa harusi kanisani akapata kwa heshima zote, akaishia kufunga ndoa bomani badala ya kanisani, michango ya harusi yake akaigeuza mtaji wa biashara na akafungua duka
 
Kwa kweli hizi harusi za gharama kubwa wafanye tu wenye hela za kufanyia starehe za kula na kunywa. Ni aibu kufanya harusi ya gharama kubwa kwa kutegemea mifuko ya watu wakati kipato chako hakifikii gharama ya harusi unayopanga. Aibu zaidi ni kuomba uchangiwe kitu ambacho ni sherehe tu, bora uchangiwe mahari kuliko sherehe
 
Kama huna fanya tu maisha yako
Usijiwekee ugumu kwenye maisha yako sababu ya mchango wa harusi,
NB.
Nachanga pale ambapo mambo yangu mengi yako sawa
 
Back
Top Bottom