jamii yetu bado ina changamoto nyingi zinazohitaji pesa kutatuliwa. Japo sherehe ni sehemu ya maisha ila suala la michango ya harusi ni cancer kwenye jamii.
Watu wanapotaka kuoana watenge kiasi cha pesa kufanikisha jambo lao kama ambavyo mambo mengine kwenye maisha yanavyofanyika. Kisha huyo mtu awaite ndugu na jamaa zake bila kuwadai michango. Wakiamua kuja na zawadi ni sawa tu ila wenye harusi wasiweke tarajio kubwa.
Kama huna uwezo wa kugharamia harusi yako fanya iwe tukio la kawaida kama yalivyo mambo mengine. Isitoshe hizi harusi za mbwembwe nyingi zinaishia kwenye kufarakana tu na ndo hazidumu. Hili nimechomekea tu lakini.
Jambo ambalo nilishafuta kwenye kumbukumbu za ubongo wangu ni kuchangisha michango ya harusi, iwe kwangu mwenyewe ama watoto wangu. Watoto itabidi wajue kabisa kuwa wakitaka mambo ya harusi waanze kufanya savings kufanikisha jambo lao bila kutegemea michango. Kwanza watu wengi wanatoa kwa kulalamika tu.
Sijaona watu wanaotoa kwa moyo wote, kwanini tuendelee kulazimisha jambo ambalo tunalazimisha watu na tena katika jamii maskini kama hii?