Michelle Obama: Ndoa haina usawa wa 50/50, lazima mmoja akubali kujitoa

Michelle Obama: Ndoa haina usawa wa 50/50, lazima mmoja akubali kujitoa

Mwanamke wa kibongo ikifikia mahala ambapo anafanya 70% wewe uko 30% huo huo ndio unakuwa mwanzo wa dharau na kebehi hata kama awali mume alikuwa akifanya 100% mwenyewe, mpasuko wa familia unaanzaga humo
Wapo wanawake wa kibongo wanaofanya hivi tena ni wasomi wenye vyeo vikubwa serikalini. Wanawake wazuri wapo braza, sema huwezi kuwapata kirahisi, na mara nyingi huwezi kukutana nao sehemu ambazo vijana wengi tunapenda kushinda. Ila yote tisa, kizazi hiki kufika miaka 15-20 mbele namba tutaisoma.....
 
Nakubal kweli wanawake wapo ila sio rahisi kuwapata
 
Mwanamke mjuaji (mwanaharakati) kamwe hawezi kuyamudu maisha ya ndoa. Ndoa haijawahi kuwa na usawa.

Ni wanawake wanyenyekevu, werevu, wavumilivu, wenye hekima na busara, waungwana, wapambanaji, wacha Mungu, na wenye maono pekee ndiyo hudumu kwenye ndoa.
 
Swadakta mkuu. Unakuta bint hana kitunalafu anataka 50 kwa 50 sasa unabaki na mshangao. Mama amewapa kitu
juzi kuna bint ni jobless alafu anataka yeye akipika mmewe afue,sasa nkawa najiuliza huyu hana hata kazi vipi akipata kazi?
Nilimchana lakini na bahati nzuri alielewa make nilimwambia jifunze kwangu nina kazi,hela ya mboga si haba alafu angalia nnavyofanya majukumu yangu ya kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni mke wa Rais Mstaafu Barrack Obama!

Huyu ni mwanamke mweusi aliyewahi kushika nafasi kubwa zaidi kisiasa hapa duniani, THE FIRST LADY OF USA. Lakini, pia ni msomi ambaye alibahatika kusoma vyuo vikubwa duniani kama Harvard University na Princeton.

Ukimsikiliza kwenye mahojiano yake haya kuhusu maisha yake ya familia hasa ndoa na malezi, utafahamu fika kwamba huyu mama ana kitu cha ziada ambacho kizazi cha leo hatuna. Kwenye ndoa kasema kuna wakati utakuwa unafanya zaidi kuliko mwenzako, na kama hutakuwa makini unaweza kukata tamaa na kuacha ndoa. Lile la 50/50 huwa haliji ghafla tu kama ambavyo wengi tunajarajia.

Amesema kazi kwa mwanamke ni muhimu sana, lakini pia ni lazima mtu ajifunze kuweka uwiano baina ya maisha na kazi yake binafsi. Haya utayapata vizuri kuanzia dakika ya tano (5) uzuri ni kwamba, mahojiano hayo yamewekea vipande hivyo unaweza kuangalia ambacho amekisema.

Baada ya kumsikiliza, nisema tu kwamba mimi siyo shabiki wa Michelle lakini, ukweli ni kwamba Raisi Obama alihitaji mwanamke mwenye hulka na akili kama Michelle ili aweze kufika pale alipofika. Huyu mama ana kitu cha ziada, ndiyo maana hata MUNGU akamfanya kuwa FLOTUS.

She's ethical, humble, emotional stable and matured: Simply Phenomenal.....

Haya Mambo ya 50/50, uwanaharakati katika ndoa na ndoa za "kisasa" za kushindana na kuoneshana ubabe tunaletewa sisi tuharibiwe familia na jamii zetu. Watu wanaotaka kuzihifadhi familia/nasaba na jamii zao hawaendekezi hayo mambo na hawaachi asili.
 
Tatizo siyo bongo mkuu, duniani kote ukipata LIFE PARTNER ambaye hajielewi lazima utakumbana na matatizo. Japo, lazima tuseme ukweli ambao vijana wengi wa leo hasahasa wanawake hatupendi kuusikia ni kwamba hata kama utapata mtu sahihi, ndoa imejaa changamoto kibao hivyo ni lazima ujifunze kuwa mvumilivu.

Sasa kama huyu mama anasema yeye mwenyewe alihisi kabisa kuna wakati anafanya 70% huku Obama akiwa anafanya 30%, lakini bado akaendelea mbele. Nadhani kuna somo kubwa la kujifunza hapa mkuu.
Sahihi kabisa boss...hapo kwenye uvumilivu sio jambo jepesi.

Uvumilivu hutakiwi kupindukia maana itageuka mateso au maumivu na saa nyingine uwe wa pande zote sio mmoja tu.
 
Ukipata ukashiba utajisahau na kiburi juu!

Nimeliona hilo Sana with personal experience!

KOSA uka risk na kumtengenezea sehemu ya kujipatia kipato kidogo kidogo tajifanya yuko bize Hadi moyowe utapasuka!yaani no time with you!!
Kipato na Ke = Mafuta na maji.

Ke wengi wakishakamata chapaa tu hutaacha kuona rangi zao halisi kitabia, nadhani sababu kuu ni nature kuwa;

Me atafute kwa jasho & Ke azae kwa uchungu; Yani Me hana shida akiwa mmiliki wa pesa na msimamizi wa bajeti ktk familia & Ke anapaswa kuzaa watoto, kuwalea na kupokea matunzo ya familia tu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke mjuaji (mwanaharakati) kamwe hawezi kuyamudu maisha ya ndoa. Ndoa haijawahi kuwa na usawa.

Ni wanawake wanyenyekevu, werevu, wavumilivu, wenye hekima na busara, waungwana, wapambanaji, wacha Mungu, na wenye maono pekee ndiyo hudumu kwenye ndoa.
Si ktk ndoa pekee, bali hata ktk urafiki wa kawaida pia hapajawahi kuwa na matokeo chanya ikiwa kila Mtu atakuwa ndiye mwenye maamuzi kwa kila jambo, lazima pawepo na Mtoaji ushauri na Msikilizaji/Mtekelezaji mipango (Kamwe mafahari wawili hawakai zizi moja na wakapatana).

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Inaonekana hata E1TZ naye pasua kichwa
Wacha hiyo,inaonekana hata ww hujitambui tatua shida zako kwanza kwani huyo uliyemtaja hapo juu anajitambua na kujielewa vizuri na ndio maana kampuni iko vizuri pia changamoto haziwezi kwisha kwa siku moja
 
juzi kuna bint ni jobless alafu anataka yeye akipika mmewe afue,sasa nkawa najiuliza huyu hana hata kazi vipi akipata kazi?
Nilimchana lakini na bahati nzuri alielewa make nilimwambia jifunze kwangu nina kazi,hela ya mboga si haba alafu angalia nnavyofanya majukumu yangu ya kike

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakikisha umefunga piemu maana si kwa kasi hii watavyokujia huko wale MARIOO [emoji87]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Wacha hiyo,inaonekana hata ww hujitambui tatua shida zako kwanza kwani huyo uliyemtaja hapo juu anajitambua na kujielewa vizuri na ndio maana kampuni iko vizuri pia changamoto haziwezi kwisha kwa siku moja
Sawa mama mdogo
 
Back
Top Bottom