Miezi sita ya kwanza ya Rais Samia uwekezaji Tanzania ulikua mara sita zaidi katika kipindi kama hicho FY2020|21

Uchumi ni imani.

Watu wakikosa imani na kesho yao, hawawezi kufanya uwekezaji.

Nimepitia Masaki, ghafla naona miradi mingi iliyosimama imeanza upya, na mingine mipya imeanza kuchipuka.

Jiwe alikuwa anatumaliza kabisa.
 
Impact yake Kitaa ipoje....

Kwa huyu na yule aliyepita maswali ni yale yale, uchumi / uwekezaji wa kwenye makaratasi bila kuleta impact yoyote mtaani ni maigizo tu...

Watu kipato cha kubahatisha na ajira bado ni msamiati.. Si bora kipindi ambacho uchumi ulikuwa so called duni lakini watu wana ajira / kipato....
 
Unajipendekeza hv unadhani watu wenye akili timamu hawaoni......!!??
 
Watanzania wanadanganyika sana,,yaani mwekezaji kaja kaandikisha mrdi kwenye makaratasi wenyw thamani ya dolla 3billion harafu akaondoka,watu wanashangilia..Ingekuwa nikweli hizo fedha zimeingizwa nchini kwenye uwekezaji..ungeona reserve ya fedha za kigen ingekuwa kubwa na thamani ya sh ya Kitanzania ingepanda ..na tungeona ajira zinakuwa nyingi sana kwani hiyo fedha nikubwa kulikobujenzi wa Bomba la mafuta ya Uganda..unlesa mseme hizi pesa ndo zile za ujenzi wa bomba la mafuta.
 
Uzuri wa siasa za wakati huu upinzani wa CCM uko ndani ya CCM hukohuko...
Tuwaachie uwanja team mwendazake vs team mama wanyooshane wao kwa wao
 
Toa upuuzi wako, huwezi fananisha huyu na mwamba JPM, huyu mama yenu mwisho 2025, aende kucheza na wajukuu.
kwa katiba hii unafikiri CCM inaweza kupindua meza aliyoikalia kote kote - yaani ndani ya CCM na ndani ya Dola ?
 
Utaumia sana, JPM yupo kuzimu, Mama ndio habari ya mujini mpaka 2030 inshallah.

Usijitafutie maradhi ya moyo kwa kumchukia the choosen one, ukisikia chaguo la Mungu ndip mtu kama Samia.

Hakugombea Urais ila Mungu amependezwa naye.
Na watakuja wawekezaji wengi tu.
Na hivi ule wizi wa IPTL Mwamba aliufumua na kuanzisha ujenzi wa Bwawa la JK Nyerere.
Alale pema Mbinguni!
 
Unalalamika nini?

Unapingana na serikali?

Njoo na wewe na takwimu zako kukanusha,

Otherwise elewe nchi inakwenda vizuri,
 
Na watakuja wawekezaji wengi tu.
Na hivi ule wizi wa IPTL Mwamba aliufumua na kuanzisha ujenzi wa Bwawa la JK Nyerere.
Alale pema Mbinguni!


IPTL imefanyaje?

Unataka Mama anegotiete ili alipwe nayeye,

SG lazima ikamilike mwaka huu,
 
Uzuri wa siasa za wakati huu upinzani wa CCM uko ndani ya CCM hukohuko...
Tuwaachie uwanja team mwendazake vs team mama wanyooshane wao kwa wao
Chadema acha kujidanganya,

CCM hakuna kundi,

CCM ni moja daima, na mama yetu ni Mmoja Samia Suluhu Hassan
 
Impact huwezi kuiona kwa muda huu mfupi

Watu ndio kwanza wako kwenye ujenzi wa miradi hiyo mikubwa,

Baada ya mwaka mmoja nadhani kila Mtanzania atakuwa amepata majibu,
 
Uchumi ni imani.

Watu wakikosa imani na kesho yao, hawawezi kufanya uwekezaji.

Nimepitia Masaki, ghafla naona miradi mingi iliyosimama imeanza upya, na mingine mipya imeanza kuchipuka.

Jiwe alikuwa anatumaliza kabisa.
Fact
🙏🏿🙏🏿🙏🏿 Utukufu ni kwa Mungu
 
Impact huwezi kuiona kwa muda huu mfupi

Watu ndio kwanza wako kwenye ujenzi wa miradi hiyo mikubwa,

Baada ya mwaka mmoja nadhani kila Mtanzania atakuwa amepata majibu,
Tumekuwa tukisubiri hizo impact miaka nenda rudi.., sio kwamba hatujui haya mambo yanachukua muda bali kilichokuwa kikitokea huko nyuma kinatufanya kuwa sceptical...

Nikupe mfano mdogo tu mradi wa Bandari ya Bagamoyo au Gesi ya Mtwara.., mara tuliambiwa tunapigwa mara ni mradi mzuri n.k., kwahio miradi hii bila transparent hatuwezi kujua kama tunaokota au tunaokotwa....

By the way tunashindwa madogo, ya kuhakikisha wakulima wetu mahindi yanapata wateja au na haya tunasubiri wawekezaji
 
Huyu na yule marehem kaka yake waongo sana. Bado hatuna masoko ya uhakika ya mazao yetu, viwanda na uwekezaji migodini bado ni tatizo na serikali hailipi madeni yake lakini bado wanadanganya macho makavu kwamba wanafanya mambo makubwa.
 
Very true....

Hakuna nchi duniani imeendelea kwa kugombana na watu kila siku, narudia tena haipo.

Hata Vietnam waliopigana vita vya moto na "mabeberu" kwa miaka zaidi ya 20 baadae walijua ukweli huu muhimu. To move forward you need more friends than enemies.

Tuvutie uwekezaji, watu wapate ajira. Huu upumbavu wa kunyanyua mabega na umaskini wetu ulikuwa unaenda kutuua.
 

Mbona hizi project mnazo kwenye makaratasi tu hazionekani popote Tanzania? Mnamdanganya nani?
 
Umenena yaliyosahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…