Wasalaam.
Habari za kusikitisha ni kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliuwawa na kundi la Hamas katika shambulio la Oktoba 7.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba inaeleza kuwa Ndg Joshua, alienda katika mafunzo ya Kilimo nchini Israel. Baada ya kutekwa na kundi hilo aliuwawa kikatili.
Waziri Makamba anaeleza kuwa mwili wa Mtanzania huyo bado unashikiliwa na kundi hilo nchini Palestine. Jitihada zinafanywa na serikali za kumsafirisha Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua pamoja na sehemu ndogo ya familia kwendq nchini Israel kwendq kupata taarifa zaidi za marehemu.
Ikumbukwe kuwa Mtanzania mwingine, Clemence Mtenga pia aliuwawa na baadae mwili wake kusafirishwa nchini kwa ajili ya maziko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.