Miili miwili bado inashikiliwa na HAMAS, upo wa kijana Mtanzania Joshua Mollel

Miili miwili bado inashikiliwa na HAMAS, upo wa kijana Mtanzania Joshua Mollel

Naona hawa vijana wetu walitumwa kufanya kazi nyingine huko Israel, yaani kweli ameenda kufuga ng'ombe wa maziwa?

Inaumiza sana.

Hiyo wizara ya nje nayo ina tatizo, inaruhusu tena mzazi kwenda kufuatilia mwili wa mwanae, wizara inafanya nini.
nashukuru umeandika jambo la ukweli, waisrael wanaingiza maspy kwa kutumia raia wa nchi nyingine halafu baadae wanatumika kwa propaganda.
 
Wasalaam.

Habari za kusikitisha ni kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliuwawa na kundi la Hamas katika shambulio la Oktoba 7.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba inaeleza kuwa Ndg Joshua, alienda katika mafunzo ya Kilimo nchini Israel. Baada ya kutekwa na kundi hilo aliuwawa kikatili.

Waziri Makamba anaeleza kuwa mwili wa Mtanzania huyo bado unashikiliwa na kundi hilo nchini Palestine. Jitihada zinafanywa na serikali za kumsafirisha Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua pamoja na sehemu ndogo ya familia kwendq nchini Israel kwendq kupata taarifa zaidi za marehemu.

Ikumbukwe kuwa Mtanzania mwingine, Clemence Mtenga pia aliuwawa na baadae mwili wake kusafirishwa nchini kwa ajili ya maziko.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Ngoja waje wavaa kobazi na misuli uone povu hapa

USSR
 
RIP, mtanzania mwenzetu.... Ila Isreal ndo imesababisha hao matekwa wasio kua na hatia kufa inarushwa mabomu hovyo na kuua watu wake waliko fichwa, majuzi tu wanajeshi wa Isreal 10 walikufa, isreal imexhanganyikiwa kuhusu hiyo vita.
 
Waziri wa Mambo ya Nje @jmakamba amesema kuwa kijana wa Kitanzania Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel, ambaye alikuwa akitafutwa tangu Oktoba 7, 2023 mara baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel, imebainika kwamba aliuawa mara tu baada ya kutekwa na wanamgambo hao.

Waziri Makamba ameyabainisha hayo leo Desemba 14, 2023, kupitia ukurasa wake wa X na kusema taarifa hizo amezipata kutoka kwenye serikali ya Israel

"Nimeongea na Mzee Mollel, baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa serikali ya Israel, tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada, kwa ridhaa ya familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo," imeeleza taarifa ya Waziri Makamba.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Mungu wangu, msiba wa nyumbani kabisa huu!
R.I.P

Sasa hao wanaotaka kwenda huko na ingali mapigano yanaendelea ni sawa? Usijezuka msiba mwingine!
Political instability hizo nchi hazifai hata kidogo....Hao jamaa kila siku kumalizana washazoea ona kijana alikuwa na ndoto zake .
 
Inna li Llahi wa inna Ilayhi Rajiun, wawekwe popote wanapostahili.

, wapo wengi sana hao kutoka nchi mbali mbali duniani waliouliwa na mazayuni wenyewe na mazayuni wamekiri kuuwa.

Ni mpumbavu tu ambae atapeleka mwanawe akasome israel, hivi huwa hamuelewi kuwa hiyo nchi ipo vitani kuanzia mwaka 1948?

Halafu cha kujiuliza, huyo mpumbavu alienda kusoma au kucheza disco?
Comment kama hii inatolewa na mtanzania.. kwenye mauaji ya kinyama ya mtanzania mwenzake..

Daah hizi dini zina tufikisha pabaya
 
Back
Top Bottom